Jerlamarel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2021
- 843
- 2,525
1. Kamwe asingekubali Mita za LUKU kutumika kukata kodi za majengo. Hapa waathirika wengi ni wapangaji ambao wengi wao ni masikini na sio wamiliki wa hayo majengo/nyumba.
2. Kamwe asingekubali Tozo za miamala ya simu. Hili asingelikubali abadani asilani. Maana miamala tayari ilikuwa na VAT, sasa kuongeza tozo ni kama unamminya mwananchi mpaka aishiwe kabisa. Tena tozo zenyewe zinakatwa kwenye kutuma na kutoa😪.
3. Kamwe asingekubali Gharama za maisha kupanda kiholela. Ndio hatukatai kuna mfumuko wa bei ila siyo katika kiwango hiki. Kuna bidhaa ambazo hazina scarcity lakini kwa sababu ya poor market control basi watu wameamua kujipandishia kiholela kwa visingizio visivyo na mashiko.
4. Kamwe asingekubali Watumishi kudanganywa kuhusu maslahi yao. Ijapokuwa yeye mwenyewe hakuwaongezea watumishi chochote kwa kipindi kirefu, lakini angalau alikuwa mkweli na ndio maana watumishi walimvumilia kwa kipindi kirefu.
5. Kamwe asingekubali Bei ya mafuta kuzidi kupanda wakati kwenye soko la dunia yameshuka. Hapa naamini kwa spirit aliyokuwa nayo ya kutetea wananchi basi angefanya lobbying yoyote ile ili kupunguza ukali wa bei ya mafuta. Nchi imezungukwa na bahari hii, tungeweza kuagiza mafuta hata Urusi kama angekuwepo mzee wetu maana hakuwa muoga kufanya chochote as long as ni for the benefit of his country.
Angalia hii chart hapa chini, utaona ni mwezi wa 3 sasa mafuta yanashuka bei wakati huku kwetu yanazidi kupaa bei. Hizo bar 3 nyekundu kwenye kibox zinaonesha mafuta yapo downtrend ila cha kushangaza sisi huku tupo uptrend.
6. Kamwe asingekubali bei za vifurushi vya simu viwe vinabadilika kiholela. Katika dunia ya sasa ambayo inaenda na sayansi na teknolojia, huduma ya internet ni moja ya basic need. Sasa unapowaminya watu wasiweze kupata internet unawaweka kwenye njaa ambayo ni sawa na njaa zingine. Bahati mbaya Waziri anayejusika na yeye anaonekana kama amebariki maana kwa mdomo wake amesema kabisa "Gharama zitaendelea kupanda".
7. Asingekubali kamwe wamasai kuhamishwa kwa lazima kutoka kwenye ardhi yao. Japokuwa inawezekana kulikuwa na nia njema kwenye hili, lakini naamini mzee angelishughulikia vizuri zaidi kuliko ambavyo imefanyika sasa. Ukiona wamasai walikuwa wanagoma kuhama ujue kuna kitu hakikuwa sawa.
8. Kamwe asingekubali Bei za pembejeo za kilimo kupanda kiholela. Moja ya eneo ambalo mzee alikuwa hapendi kabisa lichezewe basi ni kilimo. Kwenye utawala wake bei za vyakula zilikuwa nafuu sana na ndio maana raia hatukupata shida sana pamoja na hali mbaya ya uchumi iliyokuwepo. Lakini kwa sasa bei za pembejeo zimepaa, kitu ambacho kinapelekea hata bei za vyakula ziwe juu pia.