Angekuwepo Hayati Rais Magufuli Kamwe Asingekubali Haya Yatokee

Angekuwepo Hayati Rais Magufuli Kamwe Asingekubali Haya Yatokee

Sasa kama alifuga mafisadi kwenye utawala wake utasemaje alifunga mafisadi? Mafisadi gani ambao Magufuli aliwafunga? Kikwete aliwafunga Mramba na Yona, yeye alimtia mwanasiasa kigogo gani hatiani akafungwa
Ckia we makonda, sabaya Ni wanyang'anyi sawa waliwapora mafisad,wazung wa unga, pesa na Mali na hii ndio sabab waliachukiwa na matajir wa taifa,
Hakuna aliefisad nchi kwa kutumia pesa kwa manufaa binafs kpnd Cha magufuli na angetokea angefungwa maan weng waliojarib walifunguliwa kesi za uhujum uchumi na kusimamishwa au kufukuzwa kabsa
 
Magufuli ndo alipandisha bei na ada za huduma maradufu ya alizoacha kikwete.

Magufuli ndo alikuja na kikokotoo cha kinyonyaji kwa wafanyakazi...

Ni magufuli aliyeleta 15% ya makato kutoka 8% aloacha kikwete

Ni Magufuli aliyeta kizaazaa NHIF...

Yule mshamba ameiharibu sana nchi.
Achana NAO wafuga Ngombe
 
Hili ndilo tatizo kubwa la Tanzania. Watu milioni 60 wanakuwa kama nyumbu na kutegemea mtu mmoja awafanyie kila kitu. Thread yako inaakisi tabia za watanzania wengi. Namna hii wataweka mpaka tozo ya sehemu nyeti! Waogopeni nini wakati wananchi wamelala na hawajui kudai haki zao?
Haki zao ndio zipi Jiwe alipoteka kuua kupora ulilalamika wapi Wacha CHUKI Kwa mama Jiwe NI alikua Dikteta WA Zama HIZI
Kiufupi MUNGU KAMALIZA UGOMFI FULL STOP
 
Cha muhimu ni kua KAFA

Yule muuaji na mbaguzi aliyeharibu uchumi wa Tanzania, kupora wafanyabishara fedha, kupora wakulima mazao, kujaza bungeni vilaza, kukopa mikopo mikubwa kwa pupa, uanzishwaji wa miradi mfululizo mingine isiyo na faida
Mbaguzi, laghai, roho mbaya iliyojawa na kiburi...ataketee milele

Hata mafuta yakifika 5000 ni afadhali kuliko kutawaliwa na yule mpuuzi aliyekuwa akiteua majambazi, na yeye angekuwepo maisha ndio yangekuwa balaa maana angelazimisha jeshi kuingilia biashara ya mafuta kama alivyofanya kwenye korosho na fedha za kigeni alivyo na akili fupi
Una kanyangwa wewe

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
 
1. Kamwe asingekubali Mita za LUKU kutumika kukata kodi za majengo. Hapa waathirika wengi ni wapangaji ambao wengi wao ni masikini na sio wamiliki wa hayo majengo/nyumba.

2. Kamwe asingekubali Tozo za miamala ya simu. Hili asingelikubali abadani asilani. Maana miamala tayari ilikuwa na VAT, sasa kuongeza tozo ni kama unamminya mwananchi mpaka aishiwe kabisa. Tena tozo zenyewe zinakatwa kwenye kutuma na kutoa😪.

View attachment 2313646

3. Kamwe asingekubali Gharama za maisha kupanda kiholela. Ndio hatukatai kuna mfumuko wa bei ila siyo katika kiwango hiki. Kuna bidhaa ambazo hazina scarcity lakini kwa sababu ya poor market control basi watu wameamua kujipandishia kiholela kwa visingizio visivyo na mashiko.
4. Kamwe asingekubali Watumishi kudanganywa kuhusu maslahi yao. Ijapokuwa yeye mwenyewe hakuwaongezea watumishi chochote kwa kipindi kirefu, lakini angalau alikuwa mkweli na ndio maana watumishi walimvumilia kwa kipindi kirefu.
5. Kamwe asingekubali Bei ya mafuta kuzidi kupanda wakati kwenye soko la dunia yameshuka. Hapa naamini kwa spirit aliyokuwa nayo ya kutetea wananchi basi angefanya lobbying yoyote ile ili kupunguza ukali wa bei ya mafuta. Nchi imezungukwa na bahari hii, tungeweza kuagiza mafuta hata Urusi kama angekuwepo mzee wetu maana hakuwa muoga kufanya chochote as long as ni for the benefit of his country.
Angalia hii chart hapa chini, utaona ni mwezi wa 3 sasa mafuta yanashuka bei wakati huku kwetu yanazidi kupaa bei. Hizo bar 3 nyekundu kwenye kibox zinaonesha mafuta yapo downtrend ila cha kushangaza sisi huku tupo uptrend.
View attachment 2313653

View attachment 2313654

6. Kamwe asingekubali bei za vifurushi vya simu viwe vinabadilika kiholela. Katika dunia ya sasa ambayo inaenda na sayansi na teknolojia, huduma ya internet ni moja ya basic need. Sasa unapowaminya watu wasiweze kupata internet unawaweka kwenye njaa ambayo ni sawa na njaa zingine. Bahati mbaya Waziri anayejusika na yeye anaonekana kama amebariki maana kwa mdomo wake amesema kabisa "Gharama zitaendelea kupanda".
View attachment 2313657

7. Asingekubali kamwe wamasai kuhamishwa kwa lazima kutoka kwenye ardhi yao. Japokuwa inawezekana kulikuwa na nia njema kwenye hili, lakini naamini mzee angelishughulikia vizuri zaidi kuliko ambavyo imefanyika sasa. Ukiona wamasai walikuwa wanagoma kuhama ujue kuna kitu hakikuwa sawa.
View attachment 2313663

8. Kamwe asingekubali Bei za pembejeo za kilimo kupanda kiholela. Moja ya eneo ambalo mzee alikuwa hapendi kabisa lichezewe basi ni kilimo. Kwenye utawala wake bei za vyakula zilikuwa nafuu sana na ndio maana raia hatukupata shida sana pamoja na hali mbaya ya uchumi iliyokuwepo. Lakini kwa sasa bei za pembejeo zimepaa, kitu ambacho kinapelekea hata bei za vyakula ziwe juu pia.
View attachment 2313673


View attachment 2313682


Asingekubali asingekubali !!!--- unawezaje kumsemea marehemu??!!, umejigeuza wewe Mungu na ujue yale yangalikuwepo ndani ya nafsi ya marehemu kama angekuwa hai??!!, wewe umejuaje kama angefanya hivyo unavyodhani??!😏

kukufuru sio lazima umkanushe Mungu bali hata kujivika sifa zake usizostahili ni kufuru pia.
 
Naam, Mungu alikuwa na kusudi kubwa kumleta Magufuli na kumchukua kwa wakati aliyomchkua. Pamoja na kuwa Mungu alituamulia huo ugomvi, huo miradi yake mingi ya kifahari aliyoanzisha kwa wakati mmoja bila kujali uwezo wa nchi ndiyo iliyomfanya asimamishe maendeleo mengine mengi ikiwa ni pamoja na maslahi ya watumishi na kuelekeza sehemu kubwa ya mapato ya nchi kwenye miradi ya utukufu wake.

Ni hiyo miradi ya utukufu ndiyo inayoendelea kuitesa serikali ya SSH na kuifanya kuchagua fedheha iliyo nafuu: kati ya kuendelea kuwaumiza watumishi wote na kuwatuliza angalau wale wa kipato cha chini kabisa.

Hii ni kwa sababu ni ukatili mkubwa sana kuwaacha watumishi wa umma kwa miaka saba bila kuwarekebishia maslahi yao.

Uongozi unaojinasibu kuwa umechaguliwa na watu kamwe hauwezi kufanya hivyo. Magu hakuwa kiongozi wa kuchaguliwa bali ni mtu aliyewekwa na mfumo uliojimilikisha nchi yetu. Magufuli alithamini mapato ya serikali zaidi kuliko ustawi wa raia mmoja mmoja.

Hii ni kwa sababu alihitaji fedha za kutekeleza miradi yake ya kifahari kwa utukufu wake binafsi. Kwa hali hiyo tozo zote za sasa zingekuwepo tu na pengine zingekuwa nyingi, kubwa na mbaya zaidi. Mipango ya kuwapora Wamasai ardhi iliandaliwa wakati wake na bila shaka yoyote JWTZ ndiyo wangetekeleza kama ilivyokuwa kwenye korosho.

Watu makini wa nchi watakuwa wamebaini kuwa mpango wa kuhamisha Wamasai wa Ngorongoro kama ulivyobuniwa na Magu ulilenga kuwaondoa wote kwa nguvu badala ya hiari.

Ingawa haya ni maamuzi yaliyokwishafanyika Serikali ya sasa imeendelea nayo huku ikifanya marekebisho kila ilipobidi. Magu alitaka kuigeuza Ngorongoro kuwa Hifadhi ya Taifa ili aweze kuhodhi mapato yake yote.
Oneni mwendawazimu huyu!

Halafu hii nchi ina watu wa ajabu sana ukimuondoa Mangi Kimambi basi namba mbili ni wewe!

Hivi umesoma kwa kina huu uzi na ukauelewa???

Haya hao wafanyakazi unaowasema leo wananini? Gharama za maisha zimepanda mara dufu hakuna anayechukua hatua ila kusingizia vita sijui nn.
 
Ukilinganisha na haya yanayoendelea, mwamba alikosea kuwa mpole sana, alitumia lugha ya kuremba remba! Haya mang'ombe ukiyazungumzisha huwa hayaelewi, ni viboko na mbwa tu ndo wanajua njia ya kupita!
Kinyume chake, mwamba mpaka kesho watu wanamsema vibaya humu jamvini. Hakucheka na kima hata kidogo hakutaka ujinga katika taasisi za kiserikali.
 
Wameongeza Tozo kwenye kutoa pesa bank yaani huyu jamaa alietumbuliwa Kigoma na kurudishwa kupewa sekta nyeti anaharibu Nchi na huku Mama akimuangalia inaumiza sana kwa kweli...
 
Haki zao ndio zipi Jiwe alipoteka kuua kupora ulilalamika wapi Wacha CHUKI Kwa mama Jiwe NI alikua Dikteta WA Zama HIZI
Kiufupi MUNGU KAMALIZA UGOMFI FULL STOP
Dega, Dega, Dega. ID name yako ni tofauti kabisa na mawazo yako. Mimi ni miongongozi ya wengi waliopiga kelele sana kuhusu udiktekta na uongozi mbovu wa Magufuli. Infact bado natamani hata sasa iundwe tume huru kuchunguza na kila aliyehusika apate haki yake. Mama Samia sina chuki naye kabisa ila huwa nakosoa penye kasoro ili tusudi tena kule tulikotoka. Anachotakiwa kufanya ni kufumua na kusuka upya mfumo wetu wa uongozi ASAP! Wakati wa kuanza ni sasa na siyo kesho! Historia imetuonyesha kuwa hatujui ya kesho (rejea Magufuli).
 
Back
Top Bottom