Angekuwepo Hayati Rais Magufuli Kamwe Asingekubali Haya Yatokee

Mi natamani Mungu amchukue ili tuanze na upya.yaani huu mfumo wa maisha yawatanzania ubadilike,tunakoelekea kilo ya mchele itakuwa 5000
Ili likitimia Phillip mpango ni mtu na nusu ataweza anajua kupanga bajeti ya maendeleo halafu ni mkali hasiyependa wizi na kucheka na mafisadi
 
Kwaiyo unataka serikali isiweke Tozo? Nchi gani duniani inaendeshwa bila kodi? Labda nchi yenu takatifu israel huko
Namba moja. jifunze kuandika maneno rahisi kabisa ya kiswahili. 'Kwaiyo ni nini? Namba mbili: Sijasema nchi iendeshwe bila kodi, jifunze kusoma kwa ufahamu. Namba tatu: Una habari mtu akipokea mshahara serikali inakata kodi? Sasa kwanini anapotaka kumtumia kwa mfano mzazi wake fedha za matumizi akatwe tena ''tozo''? Namba nne: Kuna matumizi mengi ya serikali yanaweza kuondolewa na zikapatikana fedha badala ya kutoza watu kila wanapotuma fedha. Mfano ununuzi wa magari ya kifahari, utitiri wa viongozi wasio na umuhimu n.k.
 
Natofautiana kidogo na wewe katika suala zima la miradi kuwa ni ya kifahari.

Huwezi kusema SGR inayokwenda mpaka magharibi ya TZ ni mradi wa kifahari wa kuendekeza utukufu wake, kama unaujua uchumi vyema na kukua kwake utaelewa nini maana ya ule mradi.

Huwezi kusema ununuzi wa ndege zote za ATCL ni uendekezaji wa ufahari binafsi wa JPM, hata kidogo. Hawa watalii wanaoletwa na watakaoletwa na hizi ndege wanakuja kuifungua nchi mazima.

Labda alichokosea JPM ni namna alivyojenga hoja za kuitangaza miradi yake, katika mawasiliano yake na umma ndio lilipokuwepo tatizo la uongozi wake wote, hakujaliwa lugha yenye ushawishi kwa watu aliokuwa akiwaongoza.

Alijawa kiburi na majivuno yetu ya kanda ya ziwa.
 
Wakat wa jiwe ulikuwa unabinua kwa kudemka kumtukuza kwa kila jambo, sasaivi ndio mnajifanya wapingaji hodari
 
Wakat wa jiwe ulikuwa unabinua kwa kudemka kumtukuza kwa kila jambo, sasaivi ndio mnajifanya wapingaji hodari
Mazee vipi? Hata kama bado wewe ni mgeni lakini fanya research kabla ya kuandika. Mimi nilikuwa namtukuza Magufuli? Pengine uko kwenye ndoto!
 

Toeni mikorosho yenu hapa tumwache mzee Magufuli apumzike.
 
Ukilinganisha na haya yanayoendelea, mwamba alikosea kuwa mpole sana, alitumia lugha ya kuremba remba! Haya mang'ombe ukiyazungumzisha huwa hayaelewi, ni viboko na mbwa tu ndo wanajua njia ya kupita!
 
Nakukumbusha kuwa bei ya pembejeo (hasa mbolea) ilipanda wakati wa JPM baada ya kuzuia waagizaji binafsi wa mbolea. Aidha bei ya mbolea imepanda duniani kote

Hajawahi kuwa na uwezo wa kushusha bei ya mafuta pale inapopanda ktk soko la dunia.


Bei ya mafuta imepanda duniani kote, labda utuambie hapa afrika mashariki ni wapi huko bei imeshuka ya mafuta?

Suala la kupanda bei ya bidhaa za chakula pia siyo Tanzania pekee.

Mama Samia alikuta kibubu empty (limerembwa).. alikuwa na kazi ngumu ya kujaza kibubu (kuiamarisha uchumi mbovu) hili alilisema ktk sherehe za mei mosi.

Na kuimarisha uchumi siyo overnight process na inakwenda sambamba na maumivu ikiwemo kodi na tozo.

Kwa muda mfupi Rais Samia amefanya kazi kubwa ambayo inahitaji kujitoa ifahamu ili KUMBEZA
 
Alifany vile kwa manufaa yako we mtanzania masikini, Alifanya vile kwa matajir wezi na mafisadi waliokubuu we know babako Ni miongoni bhas aliguswa na changamoto, Pia alifany vile ku deduct gap between the rich and poor people , especially those corrupt politicians also those that conducted flourished illegal business as a residue of tax money from the natives, hereby he got traumatized with patriotic perception
 
Kachunguze utajiri wa watu kama Makonda, Mnyeti, Sabaya na wengine

Na alipokuwa akiwajengea akina Kikwete Mwinyi na Mkapa mahekalu na kuwateua wake zao na watoto wao kwenye vyeo vya kisiasa nao ni kupunguza gap la masikini na tajiri?
 
Kachunguze utajiri wa watu kama Makonda, Mnyeti, Sabaya na wengine

Na alipokuwa akiwajengea akina Kikwete Mwinyi na Mkapa mahekalu na kuwateua wake zao na watoto wao kwenye vyeo vya kisiasa nao ni kupunguza gap la masikini na tajiri?
Sasa hii case yk Ni tofauti hao unaowataj makonda,sabaya, Ni wanufaika wa utawala wake, yeye Ali deal na mafisadi ya serikali zilizopita maan yalijilimbikiza Mali sana
 
Sasa hii case yk Ni tofauti hao unaowataj makonda,sabaya, Ni wanufaika wa utawala wake, yeye Ali deal na mafisadi ya serikali zilizopita maan yalijilimbikiza Mali sana
Sasa kama alifuga mafisadi kwenye utawala wake utasemaje alifunga mafisadi? Mafisadi gani ambao Magufuli aliwafunga? Kikwete aliwafunga Mramba na Yona, yeye alimtia mwanasiasa kigogo gani hatiani akafungwa
 
Ni kweli mkuu maana angegawa mafuta bure,vyuma vilivyokaza angeleta greese,machinga aliokuwa anawalipisha 20,000 angeacha na salary angeongeza na mikopo angeacha Kukopa maana Nchi hii nintajiri na tunajenga kwa pesa zetu.

... kamwe asingekubali masikini wa nchi hii like Rostam, GSM, Mo, etc. walipishwe vitambulisho vya 20,000 kufanya biashara zao pembezoni na katikati ya barabara kwani wanajitafutia mlo wao na familia zao.
Hizo ni kejeli tu. Watu kama hao ndio namba moja kuomba vya bure...Complimentary of'
Cha muhimu ni kua KAFA

Yule muuaji na mbaguzi aliyeharibu uchumi wa Tanzania
Una nung'unika na kifo chake, Pole.
Ndio, alikuwa mbaguzi, aliweza kuwabagua "maharamia wa kiuchumi" wafuja nchi, wafanyakazi wafojaji na wengine wote wanaodondokea kwenye kopo la"Wahujumu Uchumi'....ni kweli uchumi wa wahujumu hao "uliharibika" tofauti unavyotaka ionekane, wakati wake Uchumi wa Tanzania ulipaa! halina ubishi hili!
, kupora wafanyabishara fedha, kupora wakulima mazao, kujaza bungeni vilaza, kukopa mikopo mikubwa kwa pupa, uanzishwaji wa miradi mfululizo mingine isiyo na faida
Hizo juu ni propaganda ya hali ya juu, pamoja na uasi...

vilevile
Unachosahau, yote hayo uliyoyataja ni sera za CCM.
Mbaguzi, laghai, roho mbaya..."
...hapo ni kama mabeberu vile. Bila uroho mbaya hawakuelewi, wao(mabeberu) hiyo ni hulka ya kawaida tu...
Pinde kwa Upinde? Kweli alikuwa Bullrozer!







Duh. Haya yote? Alikuwa halali huyu🤓

🤓🤓
 
...hao walikuwa "wamesha Rakebisha" hao ndio walikuwa mstari wambele kuomba rushwa, hao ndio wenye waliowaajiri..."wamachinga" hawakuwa na njaa!
Sera na ubinadamu ni tete.Makatili wataalamu.
Uongozi unaojinasibu kuwa umechaguliwa na watu kamwe hauwezi kufanya hivyo.
Hapa tunaweza kufikia kukubalina, ni kweli hata hivyo hazikuwa chaguzi zote?
Magu hakuwa kiongozi wa kuchaguliwa bali ni mtu aliyewekwa na mfumo uliojimilikisha nchi yetu. Magufuli alithamini mapato ya serikali zaidi kuliko ustawi wa raia mmoja mmoja.
Kwa mbinu alizokuwa amebakia nazo, ni kuhakikisha Serikali ina mapato kukabiliana na "vita ya uchumi" aliyekuwa akipigana. Ni jukumu la kila Mtanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi, na afanye. Kama Raisi, Ustawi wa nchi,hua linachukua kipaumbele mkubwa kuliko mmoja, mmoja...kama vile Mmasai?

Taarifa?
Watu makini wa nchi watakuwa wamebaini kuwa mpango wa kuhamisha Wamasai wa Ngorongoro kama ulivyobuniwa na Magu ulilenga kuwaondoa wote kwa nguvu badala ya hiari.
....hilo halimeguki kutoka kwa awamu hii, halimeguki CCM hata ikipindishwa vipi!
Ingawa haya ni maamuzi yaliyokwishafanyika Serikali ya sasa imeendelea nayo huku ikifanya marekebisho kila ilipobidi. Magu alitaka kuigeuza Ngorongoro kuwa Hifadhi ya Taifa ili aweze kuhodhi mapato yake yote.
Bila taarifa ya uhakika, utakuwa unakisikisia, au una laghai laghai ili kupindisha ukweli wa nini kinachoendelea. Kitaeleweka.

I beg to differ.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…