Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

Umaskini hauna adabu Kiranga. Mimi simlaumu mama yake kwa kumtelekeza kwa bibi. Na Ethiopia kuna dhiki kali hakuna mfano.

Nimekumbuka kuna binti wa kihabeshi alikuwa mzuri mithili ya ajabu, alikuwa anabembeleza aolewe na ndugu yangu apate kubaki bongo akimbie dhiki za kwao. Noma sana haya maisha.
Nitafanya mpango kwenda kuopoa mke huko Ethiopia.

Ngoja nijifunze Ki Amharic...[emoji1]
 
Tunaomba picha za kutosha za Zahara akiwa na miaka 18 tumwone vizuri
Pisi ya kihabeshi
FB_IMG_1699531689655.jpg
 
Angelina Jolie aliadopt mtoto wa kwanza wa kiume nchini Cambodia, akaja kuadopt mwengine wa kiume nchini Vietnam, akaja kuadopt mtoto mwengine wa kike nchini Ethiopia, hakuwa peke yake kwenye safari hiyo alikuwa na aliyekua mumewe Brad Pitt waliadopt wote.

Kwa mtoto wa Ethiopia jina lake Zahara, Angelina alimkuta kituo cha kulea watoto yatima akiwa ana miezi 7 tu, wahusika wa kituo wakamwambia mtoto yule ni yatima wazazi wake walifariki kwa virusi vya Ukimwi, huruma ilimjaa Jolie na kuamua kumchukua kwa taratibu zote stahiki.

Ukweli ukaja kujulikana miaka mitatu baadae, mama mzazi wa Zahara alikuwa hai, ni binti aliyepata ujauzito kwa kubakwa, huku akiishi na bibi yake na mjomba wake wakiwa katika maisha ya ufukara, baada ya kumzaa Zahara hali ilizidi kuwa mbaya, Mama Zahara akatoroka nyumbani na kumuachia mtoto bibi yake, bibi nae kwa hofu ya kumkosa mtoto kutokana na lishe duni akampeleka kituo cha kulea watoto yatima na kuomba msaada wampokee mtoto, atakufa kwa njaa.

Mama mtoto alichokiomba ni kuongea na mwanae hata kwa njia ya simu, kumjulisha kuwa ana familia Ethiopia na mama yake hajafa pia anampenda ningekuwwwala hakutaka kumchukua ampeleke wapi na umaskini bado umemtawala.
Kisheria haki hiyo hana ya kulazmisha kuongea naye kwa sababu Mwenye haki ya kumruhusu ni mama yake zahara ambaye ni Angelina jolie (Kisheria) alikuwa wapi miaka yote hiyo? Aje arudi sasa hivi
 
Ukichunguza hapo huyo mama mzazi itakuwa keshakutana na wajanja wa mjini na kumwambia kuwa kuna uwezekano akapata bingo.

Huyo mtoto kama angeishia kwenye ufukara wa Ethiopia nina hakika mama wala asingekuwa na haja ya kutaka kumjua mtoto.

Ila kwa sasa hakuna anachoweza kuambilia hata kama akitaka kuleta janja janja. Binti tayari keshatimiza miaka 18.
Hii kesi asubuhi tu anashindwa
 
Baba yako anajisikiaje kumtelekeza mtoto?
Hakuna chochote, hakumtekekeza mtoto, yule mama aliondoka bara akiwa na mimba changa kurudi pwani kwao baadaye, wakaondoka ng'ambo na mama yake kaolewa na mmarekani, na mzee alihamishwa bara kuja mkoa mwingine, na Wala yule mama hakutafuta baba wa mtoto wake, mawasiliano zamani ya shida, na yule mama yake kamueleza story yote ilivyokuwa, ndomana kaenda wizara x, kuangalia kahamishiwa sehemu fulani na ye kufatilia, ye kataka kukutana na baba yake na kutufahamu basi na si kingine, nachowasilisha damu nzito kuliko maji.
 
Ana roho nzuri sana tu
 
Back
Top Bottom