Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

Mimi mwenyewe nina mpango wa kuasili yatima kabisa. Ninaishi na watoto wa ndugu zangu na wengine wako chuo ila wana baba zao na mama zao, wakishafika malengo yao wanarudi kwa wazazi.
 
Mama yake wa kumzaa ana haki bado... maisha yanampiga kila mtu kikumbo ndo maana watu tunaamua ku escape kwa namna ile.

Japo naunga mkono mtoto aendelee kuwa mama mlezi ila kwa kweli afanye namna hata amsaidiea mama yake
 
Nikujibu ndugu mtoa thread. Yupo professor alikua udsm enzi hizo. Bwana mkubwa na mke wake waliaadapt mtoto akapataga ajali yule. Na wimbi la na professor wengi walifanya adoption enzi zile. Baaadae yule professor alikuja kumzalisha mtoto wa mama mdogo wa mkewe.
Adoption mbona zinafanyika sana bongo haswa miaka ya karibuni.
Waliosoma wanamfahamu yule mzee wetu wa ununio.
 
kweli inasikitisha kama alibakwa ila hapaswi kumshobokea mwanae sababu alimkimbia!
wakina mama wana nguvu kubwa sana ya kuwarubuni watoto, Jolie akilogwa tu akamruhusu Zahara aongee na ***** kwa simu IMEKULA!
 
mkuu huo uongo hata hapa kwetu unafanywa sana, mtoto ana wazazi wote wawili ila anapelekwa kituo cha watoto yatima.
hii tabia ya kuona watoto kama mtaji wa kutokea kimaisha ni mbaya sana. Usishangae hata baba aliyebaka akajitokeza kudai mwanae
 
Waongee ni watu wa dunia 2 tofauti
 
mkuu huo uongo hata hapa kwetu unafanywa sana, mtoto ana wazazi wote wawili ila anapelekwa kituo cha watoto yatima.
hii tabia ya kuona watoto kama mtaji wa kutokea kimaisha ni mbaya sana. Usishangae hata baba aliyebaka akajitokeza kudai mwanae
mkuu upo sahihi kabisa kuna mchungaji mmoja wa haya makanisa ya kiroho aliwadanganya wafadhili kuhusu watoto waliokuwa wanataka msaada, badala ya kupeleka wenye uhitaji akapeleka watoto wake, watoto wakawa wanasomeshwa english medium za hela ndefu, wanoko wakaenda kutibua mchezo, watoto wakasitishiwa ufadhili, ikabdi mchungaji awarudishe st kayumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…