Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

, Mama Zahara akatoroka nyumbani na kumuachia mtoto bibi yake, bibi nae kwa hofu ya kumkosa mtoto kutokana na lishe duni akampeleka kituo cha kulea watoto yatima na kuomba msaada wampokee mtoto, atakufa kwa njaa,
Kama aliweza kumtelekeza, maana yake hakujali kama ataishi au la. Anapata wapi ujasiri wa kutaka kuongea nae sasa hivi, ingekuwaje kama angekufa?

Huyo mama atulie tu kwasasa, asubirie siku mtoto atakapotaka kujua chimbuko lake, pengine ndio watafahiana.
 
Angelina Jolie aliadopt mtoto wa kwanza wa kiume nchini Cambodia, akaja kuadopt mwengine wa kiume nchini Vietnam, akaja kuadopt mtoto mwengine wa kike nchini Ethiopia, hakua peke yake kwenye safari hiyo alikua na aliyekua mumewe Brad Pitt waliadopt wote,

Kwa mtoto wa Ethiopia jina lake Zahara, Angelina alimkuta kituo cha kulea watoto yatima akiwa ana miezi 7 tu, wahusika wa kituo wakamwambia mtoto yule ni yatima wazazi wake walifariki kwa virusi vya Ukimwi, huruma ilimjaa Jolie na kuamua kumchukua kwa taratibu zote stahiki,

Ukweli ukaja kujulikana miaka mitatu baadae, mama mzazi wa Zahara alikua hai, ni binti aliyepata ujauzito kwa kubakwa, huku akiishi na bibi yake na mjomba wake wakiwa katika maisha ya ufukara, baada ya kumzaa Zahara hali ilizidi kua mbaya, Mama Zahara akatoroka nyumbani na kumuachia mtoto bibi yake, bibi nae kwa hofu ya kumkosa mtoto kutokana na lishe duni akampeleka kituo cha kulea watoto yatima na kuomba msaada wampokee mtoto, atakufa kwa njaa,

Mama mtoto alichokiomba ni kuongea na mwanae hata kwa njia ya simu, kumjulisha kua ana familia Ethiopia na mama yake hajafa pia anampenda sana.

Wala hakutaka kumchukua ampeleke wapi na umaskini bado umemtawala.
Jolie ana nafasi yake ktk thamani ya binadamu.
Apewe maua yake.
 
Ndiyo Cuzoo...
Sasa hivi Anamuita Mond Daddy na Zuch ni Mumy[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hii Dunia ni ngumu sana Wallah...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila sis Una nn wee lakini??
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Nimechekaa sana Cuzo, hii Dunia au tuimarinate na tangawizi Nini mbona ngumu hivi???
Sasa baba kama yule kuendekeza njaa Hadi kujitoa akili maana yake Nini?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umaskini hauna adabu kiranga. Mimi simlaumu mama yake kwa kumtelekeza kwa bibi.
Na Ethiopia kuna dhiki kali hakuna mfano.
Nimekumbuka kuna binti wa kihabeshi alikua mzuri mithili ya ajabu..alikua anabembeleza aolewe na ndugu yangu apate kubaki bongo akimbie dhiki za kwao. Noma sana haya maisha.
Tupe namba ya uyo bint
 
Huyo Mama ni mpumbavu tu.
Sana sana ambacho angeweza kufanya ni kumuomba msamaha Binti yake tena hadharani, na Mengine amuachie Binti mwenyewe.

Ila kwa ujumla Mama wa kweli na WA halali wa Binti ni Anjela.
usemalo ni kweli kabisa, mwenye maamuzi ya mwisho ni binti mwenyewe, biological mama wake anaposema binti ana familia africa na inampenda huo ni unafiki mkubwa. huwezi kumpenda mtu ukamtelekeza, ingekuwa mama yake mzazi ndo alimchukua na kumpeleka kwenye kituo cha kulelea watoto kutokana na maisha magumu ningemwelewa, lkn kitendo cha kumtelekeza kwa bibi yake siwezi kumwelewa kabisa. mama akae kwa kutulia, amwombe binti msamaha na asubiri reaction ya binti, asilazimishe uhusiano aliouvunja mwenyewe.

#mamahalaliwabintiniangelina
 
Back
Top Bottom