POTOSHI Angelina Mabula na Juma Aweso ndiyo mawaziri pekee waliokaa wizara moja kwa zaidi ya miaka nane

POTOSHI Angelina Mabula na Juma Aweso ndiyo mawaziri pekee waliokaa wizara moja kwa zaidi ya miaka nane

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Wakuu nimeona Mbunge Angelina Mabula anasema ukitoa yeye na Waziri Juma Aweso hakuna waziri mwingine ambaye amekaa wizara moja kwa muda wa miaka minane mfulululizo, Je ni kweli?


1752661064365.png
 
Tunachokijua
Angelina Mabula ni mbunge wa jimbo la Ilemela, Mwanza anayemaliza muda wake 2025. Mabula mbali na ubunge amewahi kuwa Naibu waziri na Waziri wa Ardhi, nyumba na makazi ya watu ya Muungano wa Tanzania 2022-2023.

Madai

Katika mahojiano yake aliyofanyiwa na kituo cha Wasafi katika kipindi cha One on One, Mbunge anayemaliza muda wake Angelina Mabula alieleza kuwa hakuna Waziri aliyekaa muda mrefu katika wizara moja kwa miaka nane mfululuzo.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa Taarifa hiyo ya Mabula inapotosha.

Ufuatiliaji umebaini kuwa si Angelina Mabula wala Jumaa Aweso pekee ambao wamekaa kwenye wizara moja kwa muda mrefu.

Waziri mwingine ambaye alikaa kwenye wizara moja kwa muda mrefu ni Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete. Kikwete amekuwa waziri wa wizara ya mambo nje na ushirikiano wa kimataifa kwa muda wa miaka 10, yaani kuanzia 1995 hadi 2025.
Back
Top Bottom