Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Nilikuwa nawaza juu ya kutosikia speech yoyote kutoka kwa mama mpendwa. Ni kama Taifa limekosa dira namna ya kuwasaidia watoto wetu, too much politics has drained all good plans and sustain High Education loans. Ni kweli tunahitaji mjadala unashirikisha wadau wote. Tupo pabaya hadi sasa
 
Nadhani sirikali inachoshwa na raia wake...wakulima wanakosa ruzuku,wafanyakazi hawatimiziwi haki kama madaraja kupanda nk. Wasanii hawasaidiwi kazizao kuwanufaisha,wanafunzi ndohivyo tena,elimu ya bure kwelikweli imekuwa sivyo michango inarudi. Hii ni sirikali ya watu kwaajili ya watu ama ya vitu na vituko?
 
Amina! Kila la kheri! And

We are behind you with full support.
Ningepependa kuzindua hii mapema ili mihula mipya inapoanza tuwe na kitu mkononi kwa wanafunzi wa awali...una mapendekezo yoyote? Tayari nina mwnafunzi mmoja mwenye tatizo sugu na tumejaribu kuchangishana na kumlipia term hii, na amefanikiwa kufanya mitihani baadhi. Bado deni ni kubwa, tusipomaliza atakataliwa mitihani mingine...kwa hiyo ni vizuri kuweka nguvu..ya ziada.
 
Natafuta, hii tunachangishana sisi raia na tunaikopeshea watoto wetu kwa riba ndogo ya mabadiliko ya fedha (devaluation of the Tshs)
Wataalam wa fedha na bima watatusaidia njia sahihi ya kufanya bila kuwaumiza.
 
Amina, tunaendelea vizuri na mipango inakwenda vizuri pia...asante kwa kuonesha moyo huu...tuendelee tusonge mbele. Nia yetu ni watoto wote kadiri iwezekanavyo wapate elimu, wapate ujuzi, wajitambue, wajiamini, wajitume. Nchi itasonga mbele tu. serikali imefanya kazi yake. sisi raia tuongeze nguvu pale panapopungua, tuache kulalamika tu.
 
Pendekeza tafadhali. Nina timu ndgo hapa arusha, lakini nguvu zaidi bora ni bora zaidi pia. Leta majina inbox if possible. email yangu ni aemghw@gmail.com
 
Miss, no problem tumeanza tutaendelea...Mungu atusaidie..
 
Ninakuelewa, nafuatwa na wanafunzi, anakuambia sijala tangu jana usiku...nilikopa elf 2 ya chakula, kesho sijui...tayari wapo tumeanza kuchanga na wanasoma hata kama hazijatimia zitafika tu na wao waone nuru hii...Mungu atuone atuonekanie katika hili.
 
tutatekeleza chini ya mradi wa shirika linalohudumia vijana na wanawake. Kwa hiyo ni sehemu ya kazi za shirika kwa mwaka huu, japo wazo ni jipya, tuna imani litafanikiwa.
 
Asante Analyst, hiyo ni sehemu ya kazi yenyewe. Tukianza tutatemblea Bodi na kujifunza kutoka kwao ili tujue tunaonezaje thamani ya kazi yao. Hii ni kazi yetu wote.Bodi ina kazi ngumu pia, tutoe mchango wetu.
 
tutatekeleza chini ya mradi wa shirika linalohudumia vijana na wanawake. Kwa hiyo ni sehemu ya kazi za shirika kwa mwaka huu, japo wazo ni jipya, tuna imani litafanikiwa.
Mungu awe nanyi!
 
Ni Jambo zuri ila kama likipata taswira ya kisiasa tu litakwama
Mkaruka, tujiepushe na siasa zinazorudisha nyuma malengo ya maendeleo! Angalau katika suala la elimu ambalo linabeba taswira ya nchi na utu wetu, tukatae aina ya siasa hizo, la sivyo hakuna haja ya kuwa na siasa hizo pia. Nimeamua kuingia siasa kuchangia maendeleo. Kama siasa itanizuia kuchangia maendeleo, nitapata shida kuendelea nayo. hebu tuliangalie jambo hili kwa namna hii kwanza tuone.
 
Mshauri na mhemiwa magufuli awepo hapa apitie maoni ya wadau asiwaombe malaika wafunge mitandao ataambulia mazur huku jf.
 
Wanasema

Wanasema kuwa mabadiliko unayoyataka: Tuanzie hapo. Tufanye sehemu yetu. Kila mtu akitimiza wajibu wake kikamilifu, ataongeza nguvu ya safari. Mungu atusaidie.
 
Amina, asante, Tuanze
 
Ninawashukuru sana kwa maoni yenu endelevu. Nitakuja na mapendekezo yaliyoratibiwa ili kwa pamoja tuone tutakavyo sogea mbele na jambo hili. Mbarikiwe wote na usiku mwema.
 
Mama kwanza nikusalimu shikamoo.pili niseme asante kwa kuliona hili na kulipa nguvu, kweli wanafunzi tunapata shida sana. Kwa mfano Mimi ni yatima sina wazazi wote na attachment ninazo, ila nimeomba mkopo nimekosa, nimeappeal pia nimekosa. Nimekwenda kuongea na Mkuu wa idara ya matangazo bodi ya mikopo lakn hakunisaidia. Na hii no kutokana sina MTU wa kunisaidia yaan kutia Maji bilikan pindi yachemkapo. Nimekwenda kwa Mkuu wa mkoa, nimekutana na wasaidizi wake lakn hawakunipa ushirikiano. Naomba mama nipe no yako ya simu nikutafute nije kuongea na ww. 0674010013
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…