Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Mikopo inatolewa kwa watoto waliosoma shule za Kata tu, huo ndiyo msimamo wa Serikali hii na ndiyo kigezo kikuu
na hao waliosoma kata na wenyewe hawapewi mpaka wawe hawana wazazi au walemavu.
elimu imekuwa biashara watoto wamaskini kupata elimu ni shida
 
Mungu akutangulie na ufanikiwe kwenye wazo lako.
Maana elimu ni msingi wa ukuaji wataifa,
binafsi Mimi ni muathirika kwa watu waliokosa mkopo mwaka jana.
maisha ni magumu mpaka unatamani kuahirisha mwaka
 
Natafuta, hii tunachangishana sisi raia na tunaikopeshea watoto wetu kwa riba ndogo ya mabadiliko ya fedha (devaluation of the Tshs)
Sasa kwa wazo hili, mwaka huu nitajiandikisha tena chuo kikuu. Nitakutembelea.
 
NI WAZO JENGEFU MAMA. KUNA WANAFUNZI WENGI WAMERUDI NYUMBANI WAMESHINDWA KULIPA ADA KWA KUKOSA MKOPO BODI YA MIKOPO.
SIFAHAM NCHI INAANDAA NINI? HATA HIVYO VIWANDA AU NDEGE ZITAENDESHWA NA NANI KAMA WASOMI WANASHINDWA KUSOMA!
ITISHA KUNGAMANO ILI TUANZIE HAPO.
 
Wazo zuri saana.
Jamani hili jambo lazima liangaliwe kwa jicho la pekee kwa maana wototo machuoni wanahali mbaya sn
Tunataka kutengeneza wataalam wa aina gani
Watoto machuoni wana hali ngumu, wazazi nyumbani ambao ni wakulima hali sio nzuri kuwahudumia watoto wachuo..ali haki ya nyumban pesa mtaani hakuna
Watoto wakike mpaka inafikia kurubunika kiurahisi
 

Ni kweli tunaweza kabisa kulimaliza tatizo hili...Tuweke mikakati mizuri, tutafika na Mungu atutangulie. Atusaidie kuona uhitaji huu tu.
 
Asante, tunalifanyia kazi tulete utaratibu. Asante.
 
Wazo zuri lakini litazuiwa ili uwekwe utaratibu mzuri wa kuchangia na CCM ndio watakuwa wasimamizi wa ugawaji wa hizo fedha .
Hii si ya chama chochote. Tufike mahali tuangalie uhalisia wa kila jambo. elimu ni suala nyeti, tukicheza nalo tunapoteza kizazi. Tutadaiwa sana.
 
Tuchange tu, tusaidie watoto wetu.
 
UHuru wa mawazo na maoni. Mwihso wa siku tjitahidi kumpa kila mtu hifadhi yake kijamii na kielimu. Ndilo lengo la jambo hili. Asante
 
Ndio chombo kinaundwa na kina mama kwa ajili ya watoto wao wote. Tumbo jalala, huokota vyote. Kuwa mama ni kubeba yote ya kwako na ya wenzako. tukisimama vizuri tutawasaidia sana vijana wetu.
 
Tu
lichukulie kama suala la kijamii, tuchange kuwachangia waliokosa mikopo. Tutimize wajibu wetu kama raia.
 
Amen!
 
Mikopo inatolewa kwa watoto waliosoma shule za Kata tu, huo ndiyo msimamo wa Serikali hii na ndiyo kigezo kikuu
wewe hivi unadhani waliokosa mkopo wote wamesoma private schools?.hebu kabla hujaropoka jaribu kufanya uchunguzi hata upate data za juu juu tuu#mimi ni mmoja wa wahanga takriban 30k
 
Mawazo mazuri mama..ubarikiwe sana kutukumbuka wanao tulioko vyuoni natumetoka katika familia za wasakatonge tukitegemea baraka za heslb.Hope they'll be a positive result that will be able to cover even the small number of students who are victim.[HASHTAG]#formeamonmywayhome[/HASHTAG] UE next week 1.8mil where will my streetfish vendor mother will get??
 
Tuchange tu, tusaidie watoto wetu.
Utachanga vipi hali unalipa kodi kubwa, maisha magumu unadhani serikali ingeweka maisha bora kwa wananchi wake kungekuwa na ulazima wa wanafunzi kupewa mikopo? Jibu ni hapana maana wazazi wengi wangemudu kulipia watoto wao ada. Unaingia gharama za kuwapeleka kidato cha sita jeshi kuwalisha na kuwavika halafu huna hela za kuwapa mkopo.Atleast wangekuwa basi wanaenda kulima ili chakula kipatikane hivi mchakamchaka wa miezi sita ndo unamfanya mtu kuwa mzalendo.
Nyie mlio katika nafasi za juu tusaidie kuondoa huu mzigo kwa wananchi, serikali iwajibike wananchi watawajibika bila hata kuweka hamasa. Mimi naona leo airport inajengwa chato, watu wameiba mali za umma na tunaambiwa makaburi hayafukuliwi hivi kweli nitakuwa na moyo wa uzalendo hata kama nimegharamikiwa kwenda jeshi kwa mujibu wa sheria?
Je ni mafisadi wangapi tunao walipitia jeshi?
Pili, serikali inaona haraka gani kuhamia dodoma na sio kusomesha wanafunzi wa elimu ya juu. katika kizazi hichi cha teknolojia watu sio lazima wafike ofisini physically kupata huduma, mambo yote ni kwenye mitandao je kipi kilikuwa muhimu Elimu kwa watoto au kuhamia Dodoma.
Naomba tena nyie weny nafasi ya kuishauri serikali wakumbusheni vipaumbele vyetu. Wananchi tunaumia hela zinavyotumika visivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…