Akhsante sana mama,hoja ya msingi kabisa. Mimi niliwahi kupata wazo kwa ajili ya kuchangia elimu kwa watoto wetu.
Kama serikali inashindwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaostahili,basi tuweke taratibu,sheria au kanuni ambazo zitalazimisha halmashauri husika ambapo mwanafunzi anatoka kuhakikisha mwanafunzi huyo anasomeshwa nao. Na hili kuna Halmashauri wanafanya tayari. Pia kama tunaweza kuchangia sherehe mbalimbali ( mpaka arobaini ya mtoto) na kupatikana mamilioni,kwa nini tusichangishane kwa hawa watoto ambao wamekosa mikopo? Utengenezwe utaratibu tu hata wa kutoa asimilia fulani za michango ya sherehe kwa ajili ya kusaidia hawa vijana. Hili kimsingi ni jukumu la serikali,lakini kama pamoja na kelele zote zilizokwisha pigwa kuhusu wanafunzi wote wenye sifa za kupewa mikopo wapewe,bado wahusika hawaonyeshi kujali. Sasa tuache kuwasaidia vijana wetu kusoma kisa tu si jukumu letu ni la serikali au tuwasaidie ili kujenga Tanzania bora ya kesho.