Pre GE2025 Anna Tibaijuka: Kimfumo uwezekano wa kutangazwa mshindi ukitokea upinzani haupo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kauli nzito sana hii ya kuwafanya wapiga kura watafakari mara mbili mbili.
 
R.I.P Laigwanan EL

Machafuko tu ama mapinduzi ya kijeshi ndio yataleta mageuzi ya kweli hapa nchini. Tunaposema uchaguzi hapa nchini ni maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura hatukosei. Wafaidika wa huo mfumo ndio hao wanaanza kukiri hadharani kilio chetu Cha muda mrefu. Na yule muhalifu naye Jana anasema watu wasiende mahakamani maana huko hakuna uwezekano wa kupata haki. Ila wanaccm walikuwa wanasema kama cdm wanaona wameibiwa uchaguzi waende mahakamani!
Lucas mwashambwa
 
CCM KUACHIA MADARAKA INATAKA MACHAFUKO NDIO JIBU LAO
Hili jambo huwa nalisema Kila siku huku, ni aidha machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi. Kinyume na hapo ni kwenda kupoteza muda kwenye mstari wa kura kuwa inachagua kiongozi. Na udhibitisho wa uhuni kwenye chaguzi zetu, ni hii miswaada ya uchaguzi iliyopelekwa bungeni hivi karibuni.
 
🤣🤣kamanda we huwezi chafua kitu bana wala hayupo wa kuchafua chochote TZ acha kutufanya tushindwe kujizuia kucheka kwa mikwara yako ya vichekesho, watu tunaomboleza muda huu...

kwa ushauri zadi check me next week ee...

R.I.P Laigwanan Comrade EL
 
Mrema alipomshinda Mkapa uchaguzi ulifutwa na CCM ikaamuru urudiwe kwa mafungu, hata hivyo uliyeyukia njiani bila kupata matokeo baada ya watu kususa.
 
Katika nchi ambako chama tawala na usalama wa taifa ni kitu kimoja au vins uhusiano wa karibu, hali ndiyo hiyo. Itachukua muda kutenganisha vyama vya siasa na vyombo vya usalama - usalama wa taifa, jeshi, polisi nk
 
Hawa wanajua wanachokifanya nchi hii na hawatoacha.
 
Naanza kuamini kuwa ruzuku ndio tageti ya vyama vya upinzani tanzania
 


“….people of eminent stature.

Bongo hii hii ya wakwere?



Hii ni Bongo ya wana wa Pwani, kusutana na kuchambana ndio ustaarabu wao.

Kunguni, wahuni, wazuri hawafi, kamuulize mamako, nendeni mkalitazame..etc


Siku tano za maombolezo andaa notebook, I’m sure utanakiri vingi.
 
Uzuri wa tibaijuka huwa hakopeshi leo kaamuwa kulifunuwa kombe kazi kwenu watafta ruzuku
 
Ikiwa Hilo ni Kweli, kwanini hamtaki Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya?

Swali muhimu kuelekea uchaguzi,

CCM itakuja na mgombea Bora 2025 au Bora mgombea?
Zodumu fikra za Chifu Hangaya!
 


Kizazi hiki tulichopo sasa hakuna mwenye uwezo wa kuleta wala kuthubutu kuanzisha hayo machafuko, Alhamdulillah.

Na hakuna sehemu machafuko yamewahi kuwa suluhisho la kisiasa zaidi ya kuwa ni faida kwa wanasiasa wenyewe na wafanya biashara.

Kukaribisha machafuko ni kukaribisha roho ya umauti ambayo itadumu kizazi na kizazi na kuleta maafa hata yasioonekana kwa macho ya nyama. Ni laana kusababisha umwagikaji wa damu, hata ya adui.




Kuhusu Mahakama za Tanzania kuoza kwa rushwa na upindishwaji wa sheria hilo wala sio habari.

Amefanya kurudia tu maneno ya viongozi wengi tu kabla yake na wengine mpaka wakashauri sheria zetu na hukumu zetu ziwekwe kwenye lugha ya Kiswahili ili tu kukabiliana na huo ukiritimba.

Labda tujiulize tu Mbona yeye hajaambiwa kufuta kauli yake Kama Rostam? Ama wanasubiri maombolezo yapite?
 

Narudia tena, machafuko pekee ama mapinduzi ya kijeshi ndio yatatupatia mabadiliko ya kweli ya kiutawala hapa nchini. Kinyume na hapo tutaendelea kutawaliwa kwa shuruti na mambo yetu kuendelea hivi hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…