Kansiime Anne ni mchekeshaji kutoka Uganda
ambae amesomea Sayansi ya saikolojia
kwenye chuo kikuu cha Makerere Kampala
Uganda ambako alianzia kuchekesha kama
utani kusambaza video zake mitandaoni lakini
kwa sasa anaingiza mamilioni baada ya
kukubalika kwenye nchi za Afrika Mashariki
ikiwemo Kenya.
Kupenyeza kwake kwenye soko la uchekeshaji
nchini Kenya ni jambo ambalo hata yeye
anasema hakulitegemea kwa kiasi hicho lakini
sasa amezidi kuwa maarufu kutokana na show
yake ya TV iitwayo Dont mess with Kansiime
inayoonekana CitizenTV Kenya ambapo amezidi
kupokelewa na Wakenya wengi wakiwemo
ambao hubaki kwenye maeneo ya starehe mjini
kumtazama kila Jumatano huku wakisubiria
foleni ya magari ipungue ndio warudi
nyumbani.
Anne anasema baada ya mda mrefu wa
kukubalika na watazamaji wake youtube,
kulimfanya siku moja apokee simu kutoka kwa
mkurugenzi mkuu wa CitizenTV Washira
Waruru aliempa dili la kuanza kuonyesha show
zake kwenye station hii.
Mbali na CitizenTV Kenya, kansiime pia
ameangukia dili ya mamilioni ya hela kama
balozi wa bidhaa za kampuni ya bima na pia
ameonekana kwenye tangazo la kibishara la
Old mutual kuhusu kuwekeza akiba kwa ajili ya
siku za usoni hasa bima ya watoto kwa ajili ya
masomo ya shule ya upili, madili yote hayo
yakiwa ya Kenya.
Unaweza kutazama moja ya video zake hapa
chini, alivyoiba simu mtaani utacheka