Anne Makinda anunua nyumba kwa Tsh. Milioni 900, Dar


Kweli unayoyasema nyumba yake seaview palw karibu na bahari miaka mingi sana mwanzo mwa 90 or mwishoni mwa 80s yes nimekulia mitaa hiyo pia ila nilikua mdogo sana
 

Tena yuko kwenye shughuli za serikali huku akiwa amevuka muda mrefu muda wa kustaafu. Ifahamike yeye ni spika mstaafu bado analipwa mpaka afe. Hawa walaji wa hii nchi ndio huwa wanajiita system, utasikia Cdm haiwezi kuchukua nchi eti kwakuwa haikubaliki na system. Fuatalia hao system sasa, utakuta ni wale wote wanaoendelea kula cake ya taifa mpaka wafe! Wanaogopa ukija utawala mwingine ulaji unaweza kusitishwa maana wengi walikuwa wezi walipokuwa madarakani.
 
Acha wivu mshamba wewe. Kwani Anne Makinda amezuiwa kufanya biashara?
 
Ukweli MTUPU Mkuu! Angalia zile nyumba za mabilioni kila moja wanazojengewa Marais wastaafu ambao wote ni ni mabilionea on top of that wanawekewa na furniture nyumba nzima za mamilioni. Ndiyo sababu hawa wahuni wana hofu kubwa ya kupoteza madaraka.

 

🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ni Mkulima mzuri wa miti Njombe hategemei pensheni wala marupurupu
 
Milioni 900?aisee huyo mana ni tajiri sana kwa hiyo hela huwezi hata kumsema na utajiri wake umenyooka
Hiyo hela ni ya kawaida sana kwa kiongozi
Wa nchi hii mzee

Ova
 
Kazi gani anayofanya USA ambayo inafanya dola laki nne kuwa kama hela ya mboga?

Amandla...
 
Ni vema Madai Kama haya yakaambatanishwa na ushahidi (nakala ya maktaba au hati ya mauziano kuthibitisha madai) .
Ninashauri tuwe tunaweka akiba ya maneno, kulinda heshima ya mlengwa mbele ya jamii,
Huyu mama ameshika nyadhifa mbalimbali toka enzi za Mwalimu Nyerere, mpaka hivi sasa,huenda amejenga kutokana na akiba (savings) zake na pensheni.
 
Acha wivu,pambana na maisha
 
Huyu mama tunazaliws tuna soma mpaka nasi tunaelekea kupata wajukuu mama bado yupo serikalini, fanya kazi kwa bidii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiinua mgongo Cha Mbunge wa kawaida 250m.kila baada ya miaka 5 je Cha Spika?jumulisha miaka yote alivyokuwa Mbunge.

Mimi tangu nipo s/msingi nilikuwa namsikia huyu mama Mara RC,kweli asiwe na pesa?
Halafu Spika mstaafu si analipwa nusu ya mshahara wa Spika wa sasa? Isitoshe uwaziri tangu awamu ya Nyerere akiwa kabinti kadogo chuchu saa sita. Kweli atashindwa kumiliki hela ya mboga kama hiyo.
 
Miradi yote hiyo alafu nasikia hana hata mtoto...
Inauma sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…