Sidhani kama hoja hapa ni pesa kapata wapi...iwe amepewa au amefanya biashara lakini hiyo dhamira tu ya kutamani kumiliki jumba la mamilioni ya pesa ni aibu kwa Kiongozi wa kaliba yake.
Mambo kama hayo afanye Mfanyabiashara, Msanii au Mwanamichezo sio tatizo lakini sio Mtu aliyewahi kupwa dhamana kubwa ya Nchi ambayo Wananchi wake wengi bado hawana uhakika wa hata mlo mmoja kwa siku au matibabu.
Ukisikiliza vipindi kama 'ushauri wako' cha RFA kila jumapili asubuhi au 'njia panda' cha Clouds jumapili mchana, kuna Watu wanakosa laki tatu tu ya matibabu na wanaishia kuzunguka mitaani kuomba michango na kukimbilia huko redioni kutafuta msaada.
Hivi Mwalimu angepewa hizo pesa angejenga au kununua nyumba ya gharama zote hizo?.
Mtu ukiutaka uongozi basi uwe tayari kupoteza.
Kama hii habari ina ukweli basi Mama huyu kaniangusha sana na sikutegemea hili kutoka kwake.