Anne Makinda kusema 93% wamehesabiwa umetambuaje? Ulikuwa na idadi kabla ya sensa?

Taifa la pingapinga.. hata science inapingwa. We hujahesabiwa!??
 
Ndio maana hii nchi tumegeuzwa mazuzu kweli, mimi sielewi kabisa Mama Makinda anapata wapi hizi figure za %,sensa ya kufikia kiwango hicho ni record ya dunia na sijui margin ya error ni %ngapi
Hujahesabiwa!?
 
Zoezi la sensa ni la kidijitali siyo analojia. Hivi hawana center ya mawasiliano ambayo inatumika kupokea ripoti kutoka kona zote za nchi? Kama ripoti zinawasilishwa wanashindwaje kujua hizo data? #Teknoloji.🙏🙏🙏
 
Sensa na Makazi unajua maana yake nini

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 

Vema kuomba msaada wa uelewa kuliko kuwa judgemental. Unapofanya masuala ya takwimu lazima uwe na unapojipimia ili kuona kama umefanikiwa au laah. Lazima kuwa na estimation (makadirio) vs actual (uhalisia).

Hizo 93% ni actual dhidi ya estimation. Na ili uone umefanikiwa ni lazima hizo data zisiwe 100% ni lazima izid kidogo au kupungua. Very rare estimation ikawa sawa na actual.

Njia kadhaa zinaweza kutumika katika kupata hizo estimation. Mfano birth and death rate with reference na population ya sensa ya mara ya mwisho.

Wanaweza kupata data kupitia kukusanya taarifa za makadirio ya kaya na wana kaya kupitia maeneo madogo madogo ya serikali za vitongoji, vijiji/mitaa.

Lengo ni nini?
Lengo ni kujua idadi sahihi ya watu waliopo hata kama sensa ikaisha wakawa wamefika 97% tafsiri yake hiyo ndio idadi sahihi ya watu waliopo na hizo 3% zilizobakia zitakua ni overestimation.

Jitahidi kujijengea uelewa kwanza kabla ya kukosoa. Hapa ulijikita kukosoa kwanini walifanya na kuona kama wanapoteza muda na rasilimali fedha.

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
KWANI TANZANIA INA IDADI YA KAYA NGAPI MPAKA IPATIKANE HIYO ASILIMIA?
 
Anajua Mama Makundi ambaye alijua idadi ya kaya kabla ya zoezi kuanza
 
"Hili nalo muende mkalitizame Dada yangu Anneh Makinda na Mdogo wangu Albina Chuwa pamoja na timu yako"
 

Kipindi wanaweka anuani kila mtaa, walipata idadi ya Kaya
 
Bora umeuliza ufafanuliwe maana naona huelewiii
 
Magufuli yuko ofisini anachapa kazi, mlitaka mmuone Kariakoo?
 
Ni kamishina au kamisaa?.
 
Watu wengi hawajahesabiwa ikiwemo mimi binafsi kutokana na wingi wa maswali nyeti ya makarani yanayoingilia faragha za watu, ni intelijensia gani hiyo serikali inayokusanya!? Unaniuliza vitu nnavyomiliki ili iweje!? Hata smartphone! Ili serikali ipate data ina mbumbumbu wangapi wasioelewa hili wala lile. Ijue namna ya-kudeal/kucheza na akili za watanzania. sensa ya hovyo kabisa kupata kuishuhudia!
 

Angalia vizuri jezi za yanga utaziona hizo kaya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…