ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Na huu ndio uzuri wa mauaji ya kijasusi unabakia kubunia bunia ila huna uthibitisho.Kifo cha huyo Dada, hakiwezi kutenganishwa na mambo ya siasa!!!
Kagame anaachaje kuhusishwa hata kama kifo cha kawaida kwa namna huyo dada alivyokuwa treated na serikali yake??
Atakufa yeye mmja ila atakuwa ameua na kutesa wengi.Siku yake naye itafika tu.
Popoma.Majitu yenye Asili ya Utusi yatakuwa yamefurahia.Kumbe ndiyo maana Watanzania wengi ( japo siyo Wote ) MNADHARAILIWA EAC ( Afrika Mashariki ) nzima kuwa HAMNA AKILI kabisa.
Yaani Mtu KAFARIKI kwa SHIDA zake haraka sana kwa CHUKI ZENU kwa Rais Kagame upesi sana mmeanza KUZUSHA na KUMCHAFUA kuwa KAMUUA.
Yawezekana CHUKI zenu Watanzania wengi kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame ikawa ama ni kutaka AZAE nanyi ili nanyi muwe na AKILI KUBWA kama zake na za Wanyarwanda ( hasa Watutsi ) au awe SHEMEJI yenu kwa Dada zenu kwani siyo kwa KUMCHUKIA Kwenu huku.
Mnakera mno tu na haivumiliki tena.
Amepata Mafunzo USA,amesomesha mwanae mambo ya ujasusi USA na Sasa ni Mkuu wa kikosi Cha ulinzi wa Rais.Niliwahi kusikia kuwa PK ni pandikizi la CIA! Analinda maslahi ya US kule Congo. Na hata siku moja hutasikia US imemsema PK!
Kwa wale wanaomfahamu sijui kama ni kweli.
Lazima Afrika ipitie tanulu la moto kabla ya kuja kupata ustaarabu.Mdada mzuri kama huyu kuwa mwanaharakati ni kujitakia balaa. The same nawaambia kina Maria Sarungi na Acheni mambo ya kujifanya wanaharakati wakati hao mnaowapigania wenyewe hawajui kujipigania.
Huyo dada ameteseka sana yeye na familia yake yeye na mama yake wamekaa ndani muda mrefu lakini pale Rwanda hakuna mwananchi aliyepaza sauti kuwatetea.
Hawa kina Mwabukusi pia nawaasa nchi hii unapoteza muda kujifanya unatetea sijui haki sijui nini wewe pambania familia yako na ndugu zako tena wa karibu. Mambo ya kufanya unatetea haki za wanyonge kwa hizi nchi za kusini mwa jangwa la sahara bado sana utaumia utakufa unaacha familia yako iliyokuwa inakutegemea.
Lissu na Mbowe wameanza kugundua hili, siku hizi wanafanya siasa kwa afya sio kujitesa.
Umeandika pumba kabisa[emoji706][emoji706][emoji706]Mdada mzuri kama huyu kuwa mwanaharakati ni kujitakia balaa. The same nawaambia kina Maria Sarungi na Acheni mambo ya kujifanya wanaharakati wakati hao mnaowapigania wenyewe hawajui kujipigania.
Huyo dada ameteseka sana yeye na familia yake yeye na mama yake wamekaa ndani muda mrefu lakini pale Rwanda hakuna mwananchi aliyepaza sauti kuwatetea.
Hawa kina Mwabukusi pia nawaasa nchi hii unapoteza muda kujifanya unatetea sijui haki sijui nini wewe pambania familia yako na ndugu zako tena wa karibu. Mambo ya kufanya unatetea haki za wanyonge kwa hizi nchi za kusini mwa jangwa la sahara bado sana utaumia utakufa unaacha familia yako iliyokuwa inakutegemea.
Lissu na Mbowe wameanza kugundua hili, siku hizi wanafanya siasa kwa afya sio kujitesa.
Ni Siasa Kagame anatuma watu waue huko SA wapinzani wake unazungumzia USA pana viongozi karibu wanne wameua wakiwa nje ya Rwanda nae anakiri kuwa adui yake atamfata popote alipo huyo alipewa sumu ya muda mrefu alipokua jela..Ni kweli amefia Marekani but sio sahihi kuhusisha kifo chake na mambo ya kisiasa kama anavyo taka kushawishi mtoa mada.
Ni kweli amekufa huyo mdada inasemekana alilalamika tumbo lina muuma baada tu ya kula chakula.Naomba isiwe kweli, huyu dada namkubali sana jamani!
Ila amekaa ndani kipindi kirefu sana, hadi nilishasahau story yake.
Unamuongelea Idd Amini yupi?Usimlinganishe Amin na vitu vya kijinga.
Amin hakuwa muuaji wala dikteta. Zile zilikuwa propaganda tu za wapinzani wake akina Obote na Museveni waliopewa hifadhi Tanzania na Mwalimu.
Hawa wapinzani walipewa kila aina ya msaada ili kumpindua Amin na pindi Amin alipokuwa anawashughulikia alikuwa akionekana muuaji.
Serikali yoyote ikitaka inaweza kukupata popote ulipo, hasa kwa watu kama hawa ambao makazi yao yanafahamika na shughuli zao zinafahamika hata baada ya kukimbia nchi
India ina mahusiano ya mashaka na Canada kwa kutekeleza mambo ya namna hiyo nchini Canada...
Russia imepigana na inapigana vita ya namna hii na mataifa mengi ya magharibi
Ni jambo la kawaida...!
Kagame ni muoga sana. Anaogopa haka kamamaView attachment 2856263
View attachment 2856340
Anne Rwigara wa Rwanda amefariki dunia huku Mamake Anne alinukuliwa akisema kifo cha bintiye kilikuwa "fumbo" kwani hakuwa mgonjwa.
Vyanzo kadhaa vinashiriki maelezo ya kuhuzunisha ya kifo chake, vikidai kwamba baada ya masaa nane ya kulalamika kuhusu maumivu ya tumbo, viungo vingi vya mwili wake vilishindwa kifanya kazi. Hatua hiyo inachochea uvumi wa sumu kuwa huenda aliwekewa sumu
Huku uchaguzi wa Rwanda ukikaribia, Watumiaji wengi wa mitandao ya Kijamii wanaelezea wasiwasi wao kwamba kifo chake kinaweza kuwa jaribio la kuzima sauti za upinzani kabisa, hata kama Jumuiya ya Kimataifa inaangalia kwa karibu maendeleo katika nchi ya Rwanda
Hii Familia ya Rwigara iliingia kwenye mgogoro mkubwa zaidi na Rais Kagame baada ya Diane ambaye ni Dada wa Anne kutangaza nia ya Kumpinga kwenye uchaguzi. Kwanza walikamatwa na kuwekwa gerezani, walinyang’anywa utajiri wa familia yao ikiwa ni pamoja na Kiwanda chao cha Tumbaku. Na wakowa gerezani inadaiwa walikuwa wakipatiwa mateso
Historia Fupi
Baba yake inadaiwa aliuawa katika ‘ajali ya gari iliyotengenezwa’ Mwaka 2015, baadaye dada yake mkubwa Diane Rwigara aliingia katika siasa za Rwanda na kutangaza kugombea urais; kwa bahati mbaya aliwekwa gerezani na Kagame kwa kujaribu kumpinga; baadae Mama yake na Anne mwaka 2017 pia waliwekwa gerezani kwa kusema juu ya mateso ya familia yao na baada ya hapo Waliachiwa na kukimbilia uhamishoni, Marekani.
Mwenyezi Mungu aipe haki familia ya Rwigara na Wanyarwanda wote wanaoteseka mikononi mwa utawala wa Kagame Rwanda.
View attachment 2856264
Hivi wewe uko sawa kichwani kweli?angekuwa mama Yako mzazi kafinywa ungeandika huu ujinga?Kawaida ukiona mtu analeta hofu unamfinya tu kimtindo maisha yanaenda.
Ingabire atakuwa alitoka miaka miwili imepitaAlikaa kidogo akapata exile USA
Utakuwa unamsema Victoire Ingabire,Huyu yupo ndani bado
Dada yakeHuyu ndiye yule alikuwa amemweka ndani? Kagame naye anakaa na vinyongo