TANZIA Anne Rwigara afariki dunia. Ni dada wa Diane aliyejaribu kugombea Urais dhidi ya Kagame. Mama asema kifo hicho ni fumbo

TANZIA Anne Rwigara afariki dunia. Ni dada wa Diane aliyejaribu kugombea Urais dhidi ya Kagame. Mama asema kifo hicho ni fumbo

Kifo cha huyo Dada, hakiwezi kutenganishwa na mambo ya siasa!!!
Kagame anaachaje kuhusishwa hata kama kifo cha kawaida kwa namna huyo dada alivyokuwa treated na serikali yake??
Na huu ndio uzuri wa mauaji ya kijasusi unabakia kubunia bunia ila huna uthibitisho.

Na hakuna chombo Cha habari Cha Rwanda kimethubutu kuripoti
 
Kumbe ndiyo maana Watanzania wengi ( japo siyo Wote ) MNADHARAILIWA EAC ( Afrika Mashariki ) nzima kuwa HAMNA AKILI kabisa.

Yaani Mtu KAFARIKI kwa SHIDA zake haraka sana kwa CHUKI ZENU kwa Rais Kagame upesi sana mmeanza KUZUSHA na KUMCHAFUA kuwa KAMUUA.

Yawezekana CHUKI zenu Watanzania wengi kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame ikawa ama ni kutaka AZAE nanyi ili nanyi muwe na AKILI KUBWA kama zake na za Wanyarwanda ( hasa Watutsi ) au awe SHEMEJI yenu kwa Dada zenu kwani siyo kwa KUMCHUKIA Kwenu huku.

Mnakera mno tu na haivumiliki tena.
Popoma.Majitu yenye Asili ya Utusi yatakuwa yamefurahia.

Bahati mbaya sana hapa Duniani Majitu makatili ndio yanadumu,hata Kwa Mwendazake ilikuwa ni Ajali tuu ila Huwa hayafi kirahisi.
 
Niliwahi kusikia kuwa PK ni pandikizi la CIA! Analinda maslahi ya US kule Congo. Na hata siku moja hutasikia US imemsema PK!

Kwa wale wanaomfahamu sijui kama ni kweli.
Amepata Mafunzo USA,amesomesha mwanae mambo ya ujasusi USA na Sasa ni Mkuu wa kikosi Cha ulinzi wa Rais.

Kiufupi ni kibaraka wa Mabeberu na ndio maana hawana Cha kumfanya .
 
Mdada mzuri kama huyu kuwa mwanaharakati ni kujitakia balaa. The same nawaambia kina Maria Sarungi na Acheni mambo ya kujifanya wanaharakati wakati hao mnaowapigania wenyewe hawajui kujipigania.
Huyo dada ameteseka sana yeye na familia yake yeye na mama yake wamekaa ndani muda mrefu lakini pale Rwanda hakuna mwananchi aliyepaza sauti kuwatetea.
Hawa kina Mwabukusi pia nawaasa nchi hii unapoteza muda kujifanya unatetea sijui haki sijui nini wewe pambania familia yako na ndugu zako tena wa karibu. Mambo ya kufanya unatetea haki za wanyonge kwa hizi nchi za kusini mwa jangwa la sahara bado sana utaumia utakufa unaacha familia yako iliyokuwa inakutegemea.
Lissu na Mbowe wameanza kugundua hili, siku hizi wanafanya siasa kwa afya sio kujitesa.
Lazima Afrika ipitie tanulu la moto kabla ya kuja kupata ustaarabu.

Bahati mbaya ni kwamba hao unaowashauri wamezaliwa.kuwa hivyo ,dhamiri zao zinawatuma.na kuwasukuma hivyo kama.wewe.unavyofanya kazi Yako.

Walisema wapuuze wanaumia nafasi so wao wanakuwa sadaka badala ya wengi na ukombozi huletwa na wachache ,jamii ikiwa na watu wengi watata haiwezi kutawalika.

Kwa hiyo Wacha waendelee kupambana ndio wito wao huo hakuna namna.
 
Mdada mzuri kama huyu kuwa mwanaharakati ni kujitakia balaa. The same nawaambia kina Maria Sarungi na Acheni mambo ya kujifanya wanaharakati wakati hao mnaowapigania wenyewe hawajui kujipigania.
Huyo dada ameteseka sana yeye na familia yake yeye na mama yake wamekaa ndani muda mrefu lakini pale Rwanda hakuna mwananchi aliyepaza sauti kuwatetea.
Hawa kina Mwabukusi pia nawaasa nchi hii unapoteza muda kujifanya unatetea sijui haki sijui nini wewe pambania familia yako na ndugu zako tena wa karibu. Mambo ya kufanya unatetea haki za wanyonge kwa hizi nchi za kusini mwa jangwa la sahara bado sana utaumia utakufa unaacha familia yako iliyokuwa inakutegemea.
Lissu na Mbowe wameanza kugundua hili, siku hizi wanafanya siasa kwa afya sio kujitesa.
Umeandika pumba kabisa[emoji706][emoji706][emoji706]
 
Watu wengi wamefanikiwa kifedha ila hawajui namna ya kuishi huku duniani. Duniani ukikosea hata kidogo namna gani utaadhibiwa tu na pengine hiyo adhabu ikagharimu hata uhai wako.

Tujifunze kwa manabii walikuwa wanatumwa na Mungu kwenda kukemea wafalme waliozingua ipa japo walikuwa na kibali na nguvu ya Mungu bafo walikuwa wanyenyekevu. Kuna lakujifunza sana hapo.

Zipo namna.

Apumzike kwa amani binti Rwigara.
 
Mtume Muhamad (saw) anatufundisha baada ya Mwenyezimungu tunapaswa tuziheshimu mamlaka, sio mtu unapata viji cent kidogo tu unahis unapaswa kutawala,.
Utawala unatoka kwa Mungu, na huja kwa machoz, jasho na damu. We jiulize maching za kagame akiingia kigali kuchukua madaraka akitoka porini alisucrifice watu wangapi then pisi kali moja inqtaka imtoe kwa vijembe na matusi.
 
Ni kweli amefia Marekani but sio sahihi kuhusisha kifo chake na mambo ya kisiasa kama anavyo taka kushawishi mtoa mada.
Ni Siasa Kagame anatuma watu waue huko SA wapinzani wake unazungumzia USA pana viongozi karibu wanne wameua wakiwa nje ya Rwanda nae anakiri kuwa adui yake atamfata popote alipo huyo alipewa sumu ya muda mrefu alipokua jela..
 
Usimlinganishe Amin na vitu vya kijinga.

Amin hakuwa muuaji wala dikteta. Zile zilikuwa propaganda tu za wapinzani wake akina Obote na Museveni waliopewa hifadhi Tanzania na Mwalimu.

Hawa wapinzani walipewa kila aina ya msaada ili kumpindua Amin na pindi Amin alipokuwa anawashughulikia alikuwa akionekana muuaji.
Unamuongelea Idd Amini yupi?
 
Serikali yoyote ikitaka inaweza kukupata popote ulipo, hasa kwa watu kama hawa ambao makazi yao yanafahamika na shughuli zao zinafahamika hata baada ya kukimbia nchi

India ina mahusiano ya mashaka na Canada kwa kutekeleza mambo ya namna hiyo nchini Canada...

Russia imepigana na inapigana vita ya namna hii na mataifa mengi ya magharibi

Ni jambo la kawaida...!

Maybe back in the day but today zama hizi si kitu cha kawaida. To take out mtu just because ana oppose ideology za kiongozi.
Unless muhusika anahatarisha usalama wa nchi kikweli kweli na si kisiasa
 
View attachment 2856263
View attachment 2856340

Anne Rwigara wa Rwanda amefariki dunia huku Mamake Anne alinukuliwa akisema kifo cha bintiye kilikuwa "fumbo" kwani hakuwa mgonjwa.

Vyanzo kadhaa vinashiriki maelezo ya kuhuzunisha ya kifo chake, vikidai kwamba baada ya masaa nane ya kulalamika kuhusu maumivu ya tumbo, viungo vingi vya mwili wake vilishindwa kifanya kazi. Hatua hiyo inachochea uvumi wa sumu kuwa huenda aliwekewa sumu

Huku uchaguzi wa Rwanda ukikaribia, Watumiaji wengi wa mitandao ya Kijamii wanaelezea wasiwasi wao kwamba kifo chake kinaweza kuwa jaribio la kuzima sauti za upinzani kabisa, hata kama Jumuiya ya Kimataifa inaangalia kwa karibu maendeleo katika nchi ya Rwanda

Hii Familia ya Rwigara iliingia kwenye mgogoro mkubwa zaidi na Rais Kagame baada ya Diane ambaye ni Dada wa Anne kutangaza nia ya Kumpinga kwenye uchaguzi. Kwanza walikamatwa na kuwekwa gerezani, walinyang’anywa utajiri wa familia yao ikiwa ni pamoja na Kiwanda chao cha Tumbaku. Na wakowa gerezani inadaiwa walikuwa wakipatiwa mateso

Historia Fupi

Baba yake inadaiwa aliuawa katika ‘ajali ya gari iliyotengenezwa’ Mwaka 2015, baadaye dada yake mkubwa Diane Rwigara aliingia katika siasa za Rwanda na kutangaza kugombea urais; kwa bahati mbaya aliwekwa gerezani na Kagame kwa kujaribu kumpinga; baadae Mama yake na Anne mwaka 2017 pia waliwekwa gerezani kwa kusema juu ya mateso ya familia yao na baada ya hapo Waliachiwa na kukimbilia uhamishoni, Marekani.

Mwenyezi Mungu aipe haki familia ya Rwigara na Wanyarwanda wote wanaoteseka mikononi mwa utawala wa Kagame Rwanda.

View attachment 2856264
Kagame ni muoga sana. Anaogopa haka kamama
 
Back
Top Bottom