SEHEMU YA TATU
Hatimaye mtu aliweza kutengenezwa ambaye Enki alimuita Adapa, ambaye kwenye biblia ni Adam, ambaye ni Homo sapiens wa leo (binadamu wa leo). Kiumbe huyo alifanana sana na miungu kiasi cha kwamba andiko moja lilikwenda mbali zaidi na kusema Mother Goddess ametoa mtu kama yeye, aliyekuwa na ngozi kama yake, hana manyoya, tofauti kabisa na wale shaggy ape-man wa kwanza.
Nefilim alikuwa compatible na watoto wa kike wa mtu huyo aliyeumbwa, angeweza kuwaoa na kuzaa watoto nao. Lakini compatibility ingewezekana kama mtu angekuwa ametengenezwa kutokana na mbegu ya maisha kama ya Nefilim, ndivyo maandiko ya kale yanavyosema.
Kama mesopotanians texts zinavyosema na kama ilivyo kwenye biblia pia, mtu aliumbwa kwa chembe chembe za miungu(gods), damu ya miungu na udongo wa dunia. Kama ilivyo andikwa wakati wa uumbaji, mother goddess aliosha mikono yake, akachukua udongo na kuufinyanga na kuuchanganya kwenye steppe. Hapa unaona kabisa "aliosha mikono", hizi ni hatua ambazo tumekuwa tukizifanya kila siku, kama tunataka tusichafue kitu.
Mesopotamian text zinaelezea ya kwamba alichanganya udongo huo na damu ya uponyaji ili kutengeneza protype man. Enki hakuona tabu kukamilisha kazi ya kutengeneza vibarua wa miungu. Alimpa maelekezo Mother goddess kama ifuatavyo:
"Mix to a core the clay
from the Basement of Earth,
just above the Abzu and shape into the form of core.
I shall provide good, knowing your gods
who will bring that clay to the right condition.
Vile vile sehemu ya pili ya kitabu cha Genesis pia, imetoa maelezo kama hayo:
And Yahweh, Elohim, fashioned the Adam of the clay soil,
and He blew in his nostrils the breath of life,
and the Adam turned into a living soul.
Katika waebrania neno "nephesh" limetafsiriwa kama soul, soul ambayo inaweka uhai kwa viumbe hai walioumbwa, ambayo uiacha pale wanapofariki. Vitabu vitano vya kwanza vya agano la kale vimezungumzia "shedding of human blood" na "eating of animal blood" kwa sababu damu ni uhai na kwenye mistari ya Biblia inayoelezea uumbaji wa mtu, imegusia nephish (soul/sprit) na damu.
Agano la kale pia limeweka wazi kazi ya damu katika uumbaji wa mtu, ambaye kwenye biblia ameitwa Adam, neno adam alikumanisha udongo wa dunia moja kwa moja bali udongo mweusi-mwekundu. Adam katika waebrania ni adama (adom) (rangi nyekundu) na katika Akkadian ni adamatu (dark-red earth).
Katika kitabu cha Genesis neno Adam limeleta maana sawa na lugha ya sumerian. Adam ilimanisha ni "mmoja wa ulimwengu, aliyetengenezwa kwa udongo mwekundu na aliyetengenezwa kwa damu".
Uhusiano uliopo kati ya damu na uumbaji umeendelea kuonekana hadi mesopatamian. Nyumba iliyofanana hospitali ambayo Ea na Mother Goddess walikwenda kumchukua mtu, iliitwa shimti. Shimti maana yake "the house where the wind of life is breathed in".
Miungu walimuita Mother Goddesses(Midwife of the gods, the knowing Mami) na kumwambia:
Thou art the mother womb,
The one who Mankind can create.
Create the Lulu, let him bear the yoke!
Ea alifahamu mahitaji yote yanayohitaji, ili kumtengeneza mutu
"I will prepare a purifying bath.
Let one god be bled..
From his flesh and blood, let Ninti mix the clay".
Ili kumtengeneza mtu kutoka kwenye udongo, ilipaswa awepo mtu wa kubeba mimba na kuweza kuzaa, hivyo Enki akamtoa mke wake:
Ninki, my goddess-spouse, will be the one for labor.
Seven goddesses of birth will be near to assist.
Baada ya kuchanganya damu na udongo, epic of creation inaendelea kusema:
The newborn's fate thou shalt pronounce.
Ninki would fix upon it the image of the gods.
And what it will be is "Man".
Kuhusika kwa mke wa Enki, Ninki katika kutengeneza kiumbe mtu, inaturudisha sehemu ya kwanza na ya pili kuhusu Adapa, ambayo nimeshaelezea.
"In those days, in those years. The wise one of Eridu, Ea, created him as a model of men".
Watafsiri maandiko ya kale, wanasema kwa kumuhusisha Adapa kama mtoto wa kiume wa Ea, inamaamisha god alimpenda sana huyo mtu na aliendana naye. Kuhusika kwa Enki spouse(Ninki) katika kumtengeneza mtu ambaye ni Adapa(the model Adam) ilitengeneza"genealogical relationship" kati ya mtu mpya na muumbaji wake.
Hapa chini nimeambatanisha picha (2 za kwamza) kutoka Assyrian seals, zikimuonyesha Mother Goddess na Ea wakiandaa mchanganyiko wa kumtengeneza mtu na kushauriana jinsi gani wafanye. Picha ya tatu ni Ninki akimbariki kiumbe mpya na kumuwasilisha kwa Ea, vile vile inaonyesha goddess nyuma yake akiwepo mti wa maisha (Tree of Life) na zikiwepo flasks za maabara huku akiwa amembeba mtoto aliye zaliwa. Picha nyingine ni za kuonyesha Assyrian cylinder seals zinavyofanana.