Sawa Mkuu tuendelee,
(MOJA),
Unasema haujakubaliana na mimi either ni katika (Physical/Spiritual) . Unahoji kwanini Mungu awe na uwezo wa kuumba na yeye asiumbwe?
Hivyo hoja yako imejikita kutaka kujua kwanini Mungu asiumbwe.
Jibu,
(1) Mungu ndio chanzo cha ulimwengu usioonekana kwa macho(Spiritual) na ulimwengu unaoonekana kwa macho(Physical). Mungu alianza kwanza kuumba ulimwengu usioonekana kwa macho(Spiritual) kisha akaumba ulimwengu unaoonekana kwa macho (Physical)
Hivyo basi, Mungu hana chanzo bali YEYE MUNGU NDIYE CHANZO CHA ULIMWENGU WOTE USIOONEKANA KWA MACHO (SPIRITUAL) NA ULIMWENGU WOTE UNAOONEKANA KWA MACHO (PHYSICAL)
Kwa muktadha huo,
Ikiwa Mungu ndiye chanzo cha uhai na uwepo wote wa ulimwengu usioonekana kwa macho na ulimwengu unaoonekana kwa macho, YEYE MUNGU ANAWEZAJE KUWA NA CHANZO IKIWA YEYE NDIYE CHANZO?
Hivyo, Mungu hana chanzo bali yeye ndiye chanzo.
(2) Nakukumbusha Mungu hayupo physical in shape, huwezi kumuona wala kumgusa katika ulimwengu huu unaoonekana kwa macho (Physical). Chochote chenye mwili wa nyama lazima kiwe kimeumbwa na muumbaji (Scientifically). Hivyo Mungu yeye ndiye Muumbaji wa viumbe vyenye mwili katika ulimwengu huu unaoonekana kwa macho.
(MBILI),
Manifest ya yeye kuumba ametoa wapi?
Jibu, Huo ni uweza wake Mungu yeye pekeee mwenye uwezo huo wa kuumba. Hivyo ni uweza ambao anao yeye mwenyewe.
(TATU),
Unahoji kwanini wanaosema "ANU" na "KI" ni Beyond physical world tunakataa na tunataka science proof?
Jibu,
Nakataa kwa sababu kwa mujibu ya maelezo yako viumbe "ANU" na "KI" NI VIUMBE WENYE MWILI. hivyo:-
(i) Kiumbe chochote chenye mwili ni lazima kiwe kimeumbwa na MUUMBAJI wa kiumbe hicho. (Scientifically) hakuna kiumbe chenye mwili kinachoweza kujiumba chenyewe. Hivyo "ANU" na "KI" ni viumbe walioumbwa na MUUMBAJI.
(ii) Viumbe hao "ANU" na "KI" kwa mujibu wa maelezo yako ni wanafanana vina saba na binadamu, kwa maana wanazaliana. Kiumbe ambacho kina mwili, kimeumbwa na kinazaliana KINAWEZAJE KUWA MUNGU? KINAWEZAJE KUUMBA KIUMBE MWINGINE?(Scientifically)
(iii) Kwa mijibu wa maelezo yako ni kwamba viumbe hao "ANU" na "KI" ni viumbe waliotoka katika sayari nyingine. Hata utoke Sayari gani Sayari zote zipo kwenye ulimwengu unaoonekana kwa macho (Physical) ulioumbwa na MUNGU. Ndio maana vimeundwa vyombo ambavyo vimeweza kwenda sayari zingine na kuona yaliyomo kwenye sayari zingine na kuendelea kufanya utafiti. Sasa kama Sayari nyingine zingekua hazionekani vyombo vingeweza kufika na kucapture pictures? Inamaanisha kinachotofautisha kufikika na kuona yaliyomo kwenye sayari zingine ni UMBALI TU na NAMNA YA KUFIKA kwenye sayari hizo. Hivyo sayari zote zipo ulimwengu unaoonekana kwa macho. Kwa maana hiyo kwa mujibu wa maelezo yako hao viumbe Anu na Ki ni viumbe wa kufikirika. Hakuna ushahidi wa KISAYANSI unaokubali kwamba wao wameumba kiumbe BINADAMU. Kwa sababu kiumbe chenye mwili wa nyama na uhai hakiwezi kuumba kiumbe mwingine mwenye uhai na mwili wa nyama na pia kiumbe chenye mwili wa nyama na uhai hakiwezi KUJIUMBA chenyewe, (This is pure scietifically).
(NNE) MUNGU YUPO BEYOND (SPIRITUAL&PHYSICAL) HIVYO MUNGU NI MKUU, MWENYE UWEZA YEYE PEKEE WA KUUMBA VIUMBE WOTE KWENYE ULIMWENGU USIOONEKANA NA UNAOONEKANA KWA MACHO.
KUSHINDWA KUMPROVE KISAYANSI, HII NDIO INADHIHIRISHA UKUU WAKE KWAMBA YEYE NI ZAIDI YA KILA CHENYE UHAI NA MWILI.
Kwanini?
Kwa sababu yeye ni MUNGU. Ndio maana hata hao viumbe wa kufikirika Anu na ki nimewaprove tu kwa urahisi kisayansi ni kwa mujibu wa maelezo yako annunaki ni viumbe wenye mwili na HATA MABAKI YAO YA MIFUPA IPO, hivyo hao viumbe annunaki ni lazima wawe wameumbwa na hawawezi kuumba kiumbe chenye mwili. (Scietifically Proved)