SEHEMU YA PILI.
Wanyama waliokuwepo(Homo erectus), kilikuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa Nefilim kuweza kutimiza mpango wake. Hivyo aliitaji kutengeneza kiumbe mwingine atakayeweza kutembea, kuinama na kusimama kama yeye, mwenye akili zaidi, mwenye uwezo wa kutafsiri mambo kwa haraka na kutekeleza maagizo yake. Hali hii ilimfanya kutengeneza kiumbe mwingine (binadamu wa leo) kutoka Homo erectus-Homo sapiens(modern man) kwa kutumia "genetic manipulation".
Kutoka Summerians imethibitishwa kwamba Annunaki alikuwa na tecknolojia za hali ya juu, aliweza kufanya space travel zaidi ya miaka 450,000 iliyopita na walikuwa wame endelea sana kwenye tasnia ya sayansi ya maisha kuliko sisi binadamu wa leo. Vile vile walikuwa na uelewa mpana kuhusu kuunganisha chromosomes na kupata genetic results kwa kutumia cloning, cell fusion, genetic transplant na njia nyingine ambazo hatuzijui sisi. Sio kwamba waliweza kufanya hivyo kwenye maabara tu, bali hata kwa viumbe hai wengine.
Uthibitisho wa kutumia mbinu hizo umethibitishwa kwenye vitabu vya kale, kimoja wapo ni Berossus, ambacho kimeweka wazi ya kwamba deity Belus (lord) ambaye kwa neno lingine ni Deus(god) aliweza kutengeneza viumbe wengine tofauti kwa kutumia njia mbili:
Njia ya kwanza.
Viumbe(watu) walitokea wakiwa na mabawa mawili, wengine manne na sura mbili. Walikuwa na mwili mmoja ukiwa na vichwa viwili, kimoja cha mwanaume na kingine cha mwanamke, walifanana viungo vya mwili, wakiwa na vya kike na kiume.
Njia ya pili.
Wengine walionekana wakiwa na miguu na pembe za mbuzi. Wengine walikuwa na miguu ya farasi, wengine walionekana wakiwa na miguu ya farasi nyuma ila kwa mbele ni sura mtu wakifanana hippocentaurs, huku wengine wakiwa na mikia ya samaki. Kiufupi walitengenezwa viumbe wengine wengi wa kila species ya mnyama.
Inaelezwa kwamba kabla ya kumtengeneza mtu kwa mfano wake, Nefilim alifanya majaribio mengi ya kutengeneza viumbe tofauti tofauti(ape-man-animal).Baadhi ya viumbe hao waliishi muda mfupi huku wakishindwa kuzaliana (reproduce).
Kupatikana kwa bull-men na sphinxes katika Near East ya kale inaweza kuthibitisha kwamba actual creatures walitokana na maabara za kibaiologia za Nefilim kama ilivyo andikwa kwenye vitabu vya sumerians.
Sumerians texts pia zinasema kwamba Enki na Ninhursag (mother goddess) walitengeneza deformed Humans ili awe kijakazi wao. Mother Goddess anaonekana akimuuliza Enki:
"How good or how bad is Man's body?
As my heart prompts me,
I can make it's fate good or bad".
Sumerians texts zinasema kwamba katika kujaribu jaribu kutengeneza mtu, Mother Goddess alizaa mtu ambaye asingeweza kuzuia mkojo, mwanamke ambaye ansigeweza kuzaa mtoto, kiumbe asiye na viungo vya mwili vya kike wala kiume. Kiujumla zaidi ya deformed humans sita zilitolewa na Mother Goddess.
Enki aliadhibiwa na Nefilim kwa kutoa kiumbe asiye sahihi. Baada ya majaribio hayo, akaja kupatikana kiumbe waliomkusudia (Tutaona mbeleni ilikuwaje na waliweza vipi).
Hapa chini nimeambatanisha picha ya kwanza inayo onyesha apes-humans, waliopatikana wakati wa majaribio yao.
Norshad
View attachment 2101515
View attachment 2101584
View attachment 2101585
View attachment 2101587
View attachment 2101729
View attachment 2101734