Swali gumu Sana hilo kwake, Mtu anaweza kusema me sijaumbwa nimetokea tu from no where, labda nimetokana na mabadiriko ya hali ya hewa au labda nimetokea kwenye evolution of Man au nimeumbwa na Aliens ila watapinga Sana na kuleta hoja ya uumbaji wa Mungu ila ukiwauliza kuhusu kuthibitisha uwepo wa Mungu ndio ugumu unapoanzia
watakwambia we unadhani Dunia imetokea wapi? Unadhani binadamu ametokea wapi? Pumzi imetokea wapi? Sayari zinaelea vipi huko juu? Wanamaliza na kusema hakuna kitu kisichokuwa na mwanzo wake/mtengenezaji wake so Kila kilichopo Duniani kiliumbwa
Sasa we waulize swali kama lako, kama unajua kuwa hakuna kitu kinatokea tu from no where, je Una uhakika gani Mungu ye alitokea tu from no where? Inakuaje ye hakuumbwa Wala kuzaliwa? Muonekano wake au umbo lake lilitokana na reference Gani? Maana ye katuumba Kwa mfano wake Sasa ye alitokana na mfano wa nani?
Utaishia kupata majibu mepesi kwenye maswali magumu Mkuu