Mkuu sijaona ushahiidi pahala popote unaooonesha kwamba maandiko ya dini yamepindishwa.
Nilichoona ni maelezo tu ambayo watu wameandika,na kila mtu anaweza kuweka maelezo yake ayatakayo akatafuta hoja mbili tatu akaweka.
Mfano hivi leo mtu akisema alimfuata magufuli akaongea nae kuhusu chanjo magufuli akasema kwamba chanjo ni nzuri ila anataka watanzania wasipate chanjo wapungue kwa kufa,
mtu akiandika hivyo Kuhusu magufuli bado sio ushahidi hayo ni madai tu na maelezo ya kawaida.
Mkuu mimi naendelea kuuliza.
Kwani bila hayo maandiko uliyoyasoma unadhani ungejua vipi kwamba sisi tumeumbwa na annunaki?
Unadhani hayo mafuvu pekee,na hizo nyayo zingetosha kuonesha kwwmba sisi tumeumbwa na annunaki bila ya msaada wa maandiko ?
Kuwepo kwa hao giants katika vitabu vya dini bado haioneshi kwamba hao annunaki ndio wamemuumba mtu.
Kwa sababu mpaka leo kuna majitu ambayo yakizikwa hapo baadae watu watashangaa wakiona mifupa yake.
Mfano yule jamaa anayeitwa
Robert Wadlow ambae alikuwa na zaidi ya
272.cm,yaani mimi naweza kufika mapajani au karibu na kiuno chake tu,huyu mtu wa miaka kadhaa hapo nyuma,je tukirejea malaki ya miaka huko why isiwe kwamba watu wa zama hizo ndio walikuwa majitu ya kawaida tu kwa zaman hizo.
SAsa uwepo wa hayo mafuvu na mabaki bado haijawa uthibitisho wa kwamba sisi tumeumb2a na anunaki kwa sababu wapo pia watu wa kawaida kama sisi wenye mamiili makubwa sana.
Kuna ushahidi gani unaoonesha kwamba sisi tumeumbwa na anunaki zaidi ya ushahidi wa maandiko ?