Huyu jamaa
Mshana Jr ni mtu tofauti sana yaani kifupi ukimfuata Pm kumuomba ushauri wa jambo flani huwa hana zile habari za kitapeli wala kuomba atumiwe pesa eti ndo akushauri kama anavyofanyaga jamaa flani hivi wa kwenye ule uzi wa meditation.
Mie binafsi kuna kitu kaka Mshana aliwahi kunishauri siku za nyuma kidogo sikufuatilia ila hivi karibuni nimegundua kulikuwa na maana kubwa sana kwenye maisha yangu mpaka natamani sana siku moja nionane naye live nimshukuru.
Ukweli Jf imejaa wapigaji wengi sana ambao huanzisha mada flani ambazo zikikugusa ukazama Pm ili upate maelekezo vizuri unaishia kuombwa hela
Ila kwa
Mshana Jr yeye ni tofauti sana na wengine.
Mungu ambariki sana huyu jamaa
Sent using
Jamii Forums mobile app