Tetesi: Ansbert Ngurumo: Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, wamejivua uanachama wa CCM

Tetesi: Ansbert Ngurumo: Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, wamejivua uanachama wa CCM

Status
Not open for further replies.
Drama hizi za ccm sio za kuamini sana.. Kuna wakati hao wazee wakiwa madarakani walikuwa untouchables lakini pia wana tuhuma lukuki kama viongozi wengine wote wa ccm... Tusubiri yatokanayo

Jr[emoji769]
Bora wewe una akili, yale yale enzi za Lowasa alafu wapinzani watayadaka kama kawaida yao na mwisho kuachwa solemba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SAUTI KUBWA wamechafua na kudhalilisha jina lao na kada nzima ya uandishi huru.

Vyanzo vyao vimewaambia Bwana Mkubwa amefedheheka mpaka kutafuta watu wa kwenda kuwabembeleza kina Makamba.

Na vyanzo hivyo hivyo vimewataarifu Mzee alishapanga kuwapiga paranja uanachama na hivi vikao ni ghereaha tu, na wakileta mbwai watafanyiwa mbwai za utakatishaji, usanifu, uratibu na ufadhili wa genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi.

Mwandishi si tu anafika aya ya tano keshasahau aya ya pili alidanganya nini bali hata kupitia andiko kabla ya kurusha hewani anasahau.
nacheka huku naogopa
 
Duh! Bora angalau angalau Makamba! Lakini Kinana? Kinana ni fisadi mkubwa aliyepora na kujilimbikizia mali kwa kofia ya Katibu mkuu wa CCM! Safishasafisha ya Magufuli ndani ya CCM ilimuacha hoi bin taabani na kuanza fitna! Maji yamewafika shingoni! Kuondoka CCM sio dawa! Dawa ni kurudisha Mali za Chama na hela za umma na kuwaomba wananchi msamaha madharara waliyowasababishia kwa wizi huo! Chini ya JPM kila jiwe litapinduliwa. Lowassa, Kingunge na Sumaye sasa hivi wako wapi! Usicheze na CCM!
Wewe utakuwa umeanza kufuatilia siasa baada ya Musiba kuanziasha kipeperushi chake.

Kinana kaomba kujiuzuru kwa zaidi ya mara tatu,kila alipoomba aache ukatibu Mkuu ,chama kilikataa,angekuwa anaakili za takataka na mpenda pesa asingeomba kujiuzuru bila shinikizo lolote.

Kinana aliondoka wana CCM wakiwa hawajaridhia,maana tangu Kinana ameondoka CCM ilikufa na kubaki dola iliyobeba CCM.
Kinana ni think tank sio ya Tanzania tu,ni Afrika mashariki na kati ,huyo jamaa ni heavy weight.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
'Kinana ni think tank sio ya Tanzania tu,ni Afrika mashariki na kati ,huyo jamaa ni heavy weight'.

Labda think tank wa kuiba pembe za faru wetu/ujangili.
Wewe utakuwa umeanza kufuatilia siasa baada ya Musiba kuanziasha kipeperushi chake.

Kinana kaomba kujiuzuru kwa zaidi ya mara tatu,kila alipoomba aache ukatibu Mkuu ,chama kilikataa,angekuwa anaakili za takataka na mpenda pesa asingeomba kujiuzuru bila shinikizo lolote.

Kinana aliondoka wana CCM wakiwa hawajaridhia,maana tangu Kinana ameondoka CCM ilikufa na kubaki dola iliyobeba CCM.
Kinana ni think tank sio ya Tanzania tu,ni Afrika mashariki na kati ,huyo jamaa ni heavy weight.

Sent using Jamii Forums mobile app

dodge
 
Hii ni vita ya kimkakati na ushindi lazima upatikane kimkakati.

Tujaribu kuunganisha dot za aya za Mwandishi: Membe na Kinana umepanga kuwafuta uwanachama kisha Makamba umpe onyo, sawa maana target hapa ni Membe kimkakati.

Membe anaitikia wito wa kuhojiwa, Kinana na Makamba wanaamua kujiuzulu uwanachama nao wanafanya haya kimkakati

Hapa kichwa lazima kigonge kutafuta mbinu mbadala, huwezi tena kumnasa Samaki wako uliye mtarget bila (chambo)
kitakachofuata ni Membe kupewa onyo na si vinginevyo..
Plan imefeli, so mwenye chama chake lazima atafute plan nyingine ili amnase samaki wake, japo huyu samaki si mtu wa sport sport hasa kwenye vita za kimkakati.
 
Kumbe Jana ccm ilitimiza miaka 43 ya uchawi wacha walane wenyewe kwa wenyewe hii ni dalili ni kuwa ccm hakitatimiza miaka 50 kwa kuwa kitakuwa kimeshazikwa na maombi ya rc Chalamila kuanzisha jrp yaani jiwe ruling party yatatimia
Tume huru ya uchaguzi lazima CCM kiwe chama cha upinzani kama KANU ya kenya
 
CCM ni chama chenye usubutu na chenye kuamini kuwa hakuna aliye zaidi ya chama na chenye kutetea maslahi mapana ya Taifa Kama ni kweli acha waondoke kwani waliondoka wengi wakubwa zaidi yao binafsi niwatakie uzee mwema
Kama hawa wametoka je Kikwete bado ni mwanaccm ?
 
Ngumu kumeza hii kitu
Kinana, Makamba wajivua uanachama CCM

Ansbert Ngurumo8th February 20200 Comments

MAKATIBU wakuu wastaafu wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, wamejivua uanachama wa chama hicho.

Habari zilizoifikia SAUTI KUBWA zinasema Kinana na Makamba walijiondoa rasmi CCM kwa maandishi. Barua zao, kila mmoja na ya kwake, zilifikishwa ofisini kwa Katibu Mkuu wa CCM tarehe 7 Februari 2020.

Chanzo kinachoaminika kutoka CCM Makao Makuu kimeiambia SAUTI KUBWA: “Barua zao zimefika kwa nyakati tofauti, zimepokelewa. Lakini inaonekana kama walikuwa wameziandika muda mrefu baada ya kushauriana, maana zinafanana na zimewasilishwa siku moja. Taarifa hizi zilipofikishwa kwa Mzee (Rais John Magufuli) zilimvuruga kwa kweli.”

Kwa mujibu wa chanzo hicho, ambacho hakitatajwa hapa, Rais Magufuli, baada ya kupokea ujumbe wa Kinana na Makamba kujivua uanachama, aliwaomba wazee wawili waandamizi – Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Spika Mstaafu Pius Msekwa – wamsaidie kuzungumza na akina Kinana ili kuwashawishi wabadili msimamo wao.

Hata hivyo, Kinana na Makamba wamegoma kusikiliza ushawishi wa mtu yeyote. Katika barua zao za kujiondoa CCM, kwa mujibu wa chanzo chetu, Kinana na Makamba waliambatanisha pia kadi zao za uanachama.

“Tayari wameturudishia kadi zetu, maana yake wao si wanachama wetu tena,” kimesema chanzo hicho.

Kinana na Makamba ni miongoni mwa makatibu wakuu wanaoheshimika katika CCM, wenye ushawishi, na ambao wametumikia nchi katika nyadhifa mbalimbali kuanzia jeshini hadi serikalini na kwenye chama.

Siku ambayo walikabidhi barua na kadi zao na kutangaza rasmi kujiondoa CCM, ndiyo siku walipotarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM iliyoagizwa na Rais Magufuli katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), ili wajieleze kuhusu waraka walioanidika kwa Baraza la Wazee la chama hicho wakilalamikia kubezwa na kudhalilishwa na mhuni mmoja anayetumia jina la rais kudhihaki na kushambulia wakosoaji wa rais na serikali.

Mbali na Kinana na Makamba, mwingine aliyeitwa kuhojiwa na kamati hiyo ni Bernard Membe, waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambaye aliunga mkono waraka wa wazee hao, na pia alidukuliwa akizungumza katika simu mambo ambayo hayakumfurahisha Rais Magufuli.

Yeye alikutana na kamati hiyo Mjini Dodoma Ijumaa tarehe 7, Februari 2020; na baada ya mahojiano alionekana mwenye kujiamini na mwenye furaha. Mmoja wa wajumbe walioshiriki mahojiano hayo amezungumza na SAUTI KUBWA kwa sharti la kutotajwa, akisema: “Tulijuta kumuita Membe. Kuna maswali amehoji na masuala amezungumza nasi hadi tukahisi yeye ndiye anayetuhoji. Ukweli ni kwamba chama chetu kinahitaji mabadiliko makubwa ya kimsingi, maana kuna shida mahali. Bwana mkubwa anatupelekesha, na watu jasiri wa kumwambia ukweli hawapo, tunaishia kuagizwa tu, hata kutenda mambo yaliyo kinyume cha misingi ya CCM. Membe ametukumbusha yote haya. Kwa kweli, sijui kinachoofuata.”

Hata hivyo, SAUTI KUBWA iliambiwa wiki iliyopita kuwa agizo la kamati kuwahoji wakongwe hao lilikuwa kama igizo tu, kwani Rais Magufuli na watu wake walishaamua kuwa Membe na Kinana wavuliwe uanachama, na Mzee Makamba apewe onyo kali.

Kwa Kinana na Makamba kujivua uanachama na kugoma kuhojiwa, wamewaza hatua mbili mbele ya Magufuli. Chama hakiwezi kuwahoji kwa kuwa wao hawafungwi tena na nidhamu wala maadili ya CCM kwa kuwa si wanachama CCM.

Ingawa barua zao zilipelekewa kimya kimya, na uongozi wa juu wa CCM umekuwa unahangaika kuzuia taarifa hizi kuvuja, zilivuja mapema mno; na kitendo chao cha kutofika mbele ya kamati kuhojiwa kimezua maswali na mjadala mpana ndani nanje ya CCM.

Baadhi ya wadau wa siasa za Tanzania wanasema inawezekana kitendo hiki kikawaingiza wote wawili, au mmoja wao, kwenye matata makubwa, kwani uongozi wa CCM ni wa visasi, unaweza kutaka kuwakomoa na kuwadhalilisha.

Profesa mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema: “Tusishangae sasa kusikia siku moja Kinana au Makamba wametiwa mbaroni na wanashitakiwa kwa utakatishaji fedha, maana hii ndiyo fimbo mpya ambayo inatumika kuumiza wanaotofautiana na watawala. Lakini iwapo watashitakiwa umma utajua kuwa sababu hasa si uhalifu wao bali ni hii barua yao na uamuzi wao.”

Kiongozo mmoja mwandamizi wa CCM ameiambia SAUTI KUBWA: “Kiukweli, Mzee Kinana na Mzee Makamba hawana cha kupoteza. Nadhani sisi ndio tuna cha kupoteza, maana ukisoma waraka unaowasababishia haya yote utagundua kuwa wao ni watetezi wa misingi ya chama chetu. Wanachotetea ndicho wanaCCM wote tunapaswa kutetea, lakini sasa tofauti iliyopo kati yetu na wao ni kwamba wao wameonyesha ujasiri ambao sisi hatuna. Wengi wetu tumebaki kutii maagizo ya bwana mkubwa, huku chama kinaporomoka!”

SAUTI KUBWA inatambua kuwa kuna mtifuano mkubwa ndani ya CCM ambao haujawahi kutokea tangu uwepo wa chama hicho, ingawa wanafanikiwa kuufunika kwa kutishana – kwa kutumia vuombo vya dola.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom