Ansbert Ngurumo: CHADEMA Kinafanya kila jitihada kukwepa lawama hata kwa mambo ambayo kimekosea hadharani

Huyu ngurumo aliandika makala kwenye mwanahalisi kuwa,

Watu walilipwa pesa nchi nzima kumlilia Magu Ili aonekane kwamba allipendwa.

Tangu siku hiyo nilimtilia mashtaka utimamu wake na msimamo wake binafsi Katika fikra huru.
Watu walimiminika kuhakikisha kama DIKTETA amekufa
 
Shida ya Chadema ya sasa ndio hii,wanataka kila wanachosema watu waseme ndio,wanajiona wana akili kuliko yeyote.Ni madkIteta ambao wakiipata nafasi tutaomba poo
Huyo ni mwana CCM, yeye kila Leo akipewa ni Chadema

Tunawajua hao wametumwa, wanataka kuwajaza hofu watu ili washinikize Chadema waingie kwenye uchaguzi wa kitapeli

Msimamo wa CHADEMA ni No Reform No Election
 
Yeye Ansbert Ngurumo aanzishe chama chake afanye atakavyo.

Au ahamie chama kinachofanya vizuri.

Kama ilivyo kwa kila mtu anautashi kwenda kokote na kufanya tofauti na chadema kwa maslahi yake ya kuwa prove chadema kwamba wamekosea.

Tangu 2019, 2020, 2024 matokeo zero, bao anataka chadema washiriki 2025 ili kumfurahisha nani yeye?
 
View attachment 3395064

Mwandishi wa habari mwandamizi, Ansbert Ngurumo, ameibua mjadala mpana kuhusu mwenendo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akikitahadharisha dhidi ya kile alichokiita “ubinafsi wa kitaasisi” na “ukanushaji wa makosa ya wazi.”

Kupitia andiko lake linalosambaa mitandaoni, Ngurumo amesema kuwa CHADEMA @ChademaTZ2 inaelekea kutoonesha dalili za kuvumilia upungufu wa ndani na kushindwa kujisahihisha, hata pale ambapo ushahidi na hoja dhahiri zinawekwa mezani na umma au wanachama wake wenyewe.

“Chama kinafanya kila jitihada kukwepa lawama hata kwa mambo ambayo kimekosea hadharani kwa kauli au matendo. Hakiamini kwamba kinaweza kukosea,” ameandika.

Ngurumo Ngurumo ameeleza kuwa hali hiyo ya kukataa kukosolewa au kupotosha mitazamo ya wakosoaji ni hatari kwa ustawi wa chama chochote kinachotaka kuaminiwa na wananchi.

“Hata pale kinapokosolewa kwa mifano hai na ushahidi, kama katika hili la "kuzuia uchaguzi," ambayo ni kauli ya mwenyekiti, kinakana. Viongozi hawataki kukiri kuwa walikosea au wanakosea”, ameongeza.

Akiwa na mtazamo wa kisayansi na wa kitaasisi, Ngurumo amefafanua kwamba mwenendo huo unaashiria hali ya organizational narcissism (ubinafsi wa taasisi), institutional denial (ukanushaji), na institutional manipulation (udanganyifu wa kimfumo).

Katika maelezo yake, amesisitiza kuwa hali hiyo ni kiashiria cha mtafaruku wa kiuongozi au kiutawala, na kwamba mashabiki wa chama hicho wanajitahidi “kutafuta huruma ya jamii kwa kupotosha maoni ya wakosoaji wao.”

Ngurumo anaonya kuwa endapo hali hiyo itaachwa bila kushughulikiwa, inaweza kuigharimu taasisi hiyo kisiasa na kijamii. Ametahadharisha pia kuwa tayari baadhi ya watu wamejipanga kumshambulia binafsi kwa kutoa maoni hayo badala ya kutafakari hoja zenyewe.

“Nayasema sasa ili kesho wasije wakatokea watu wakasema tulitelekeza taasisi, tukaiacha ifanye makosa ya wazi, tukashindwa kuishauri. Kesho si mbali. Tutakumbushana maneno haya,” ameandika.
Sasa yeye anasemaje kuhusu uuchaguzi? Je, CHADEMA washiriki hivyo hivyo tu bila kujali mapungufu yaliyopo kwenye taratibu za uchaguzi? Hili la CHADEMA kutoshiriki uchaguzi wako sahihi!
 
Ni vizuri akajibiwa hoja zake lakini. Tusikimbilie kumtuhumu kila mtu ni mamluki!!
Hoja gani aliyotoa!!
Anasema ubinafsi wa kitaasisi, ukanushaji na udanganyifu wa kimfumo, lakini hajaeleza ni vipi CHADEMA wamefanya hayo, sasa utamjibu nini!!??

Nikisema Fanton Mahal ni mwizi, lazima nionyeshe wizi wake u wapi ili hoja yangu iwe na mashiko.
 
Ukitaka kujua kua watu kama Hawa wanatafuta kulamba Asali

Hauwezi Ukamsikia akitoa maoni au Ushauri Kwenye Swala utekaji/watu lupotra na kuuawa
 
Mwandishi wa habari mwandamizi, Ansbert Ngurumo, ameibua mjadala mpana kuhusu mwenendo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akikitahadharisha dhidi ya kile alichokiita “ubinafsi wa kitaasisi” na “ukanushaji wa makosa ya wazi.”

Kupitia andiko lake linalosambaa mitandaoni, Ngurumo amesema kuwa CHADEMA inaelekea kutoonesha dalili za kuvumilia upungufu wa ndani na kushindwa kujisahihisha, hata pale ambapo ushahidi na hoja dhahiri zinawekwa mezani na umma au wanachama wake wenyewe.

“Chama kinafanya kila jitihada kukwepa lawama hata kwa mambo ambayo kimekosea hadharani kwa kauli au matendo. Hakiamini kwamba kinaweza kukosea,” ameandika.

Ngurumo ameeleza kuwa hali hiyo ya kukataa kukosolewa au kupotosha mitazamo ya wakosoaji ni hatari kwa ustawi wa chama chochote kinachotaka kuaminiwa na wananchi.

“Hata pale kinapokosolewa kwa mifano hai na ushahidi, kama katika hili la "kuzuia uchaguzi," ambayo ni kauli ya mwenyekiti, kinakana. Viongozi hawataki kukiri kuwa walikosea au wanakosea”, ameongeza.

Akiwa na mtazamo wa kisayansi na wa kitaasisi, Ngurumo amefafanua kwamba mwenendo huo unaashiria hali ya organizational narcissism (ubinafsi wa taasisi), institutional denial (ukanushaji), na institutional manipulation (udanganyifu wa kimfumo).

Katika maelezo yake, amesisitiza kuwa hali hiyo ni kiashiria cha mtafaruku wa kiuongozi au kiutawala, na kwamba mashabiki wa chama hicho wanajitahidi “kutafuta huruma ya jamii kwa kupotosha maoni ya wakosoaji wao.”

Ngurumo anaonya kuwa endapo hali hiyo itaachwa bila kushughulikiwa, inaweza kuigharimu taasisi hiyo kisiasa na kijamii. Ametahadharisha pia kuwa tayari baadhi ya watu wamejipanga kumshambulia binafsi kwa kutoa maoni hayo badala ya kutafakari hoja zenyewe.

“Nayasema sasa ili kesho wasije wakatokea watu wakasema tulitelekeza taasisi, tukaiacha ifanye makosa ya wazi, tukashindwa kuishauri. Kesho si mbali. Tutakumbushana maneno haya,” ameandika.
See translation
Huyu ni mpumbavu sana, hajui anachokipigania
 
Huyu ni Ngurumo yupi, mimi namjua yule wa Msondo ngoma na naamini ni hayati kwa sasa
 
ANSBERT NGURUMO BADO NI MTUMWA NDANI YA SANDUKU LA SIASA ZA URAFIKI WA KAIZARI MBOWE

Screenshot_20250705_193205_Chrome.jpg

Ansbert anaikosoa Chadema ya Lissu.

Hajawahi kuikosoa Chadema ya Mbowe.

Sababu ni kwamba Ansbert alikuwa Timu Mbowe na bado yuko Timu Mbowe.

Sijaona mahali amekiri na kumpongeza Lissu kwa ushindi zaidi ya kumsimanga kwa kutumia ujanja wa maswali ya kifalsafa.

Hajakubali kwamba Lissu alishinda kihalali tena katika mazingira magumu ambapo baadhi ya watu wa system walishirikiana na Mbowe kumlima ngwara Lissu.

Hivi haelewi kuwa diachronic incoherence refers to a lack of consistency or logical connection between an agent's beliefs, intentions, or actions across different points in time?

Haelewi kuwa synchronic coherence, in the context of beliefs, refers to the logical consistency and closure of an agent's beliefs at a single point in time?

Kama anelewa kwa nini anataka tujadili diachronic incoherence ya Lissu badala ya kujadili synchronic coherence ya Lissu kwa sasa, ambayo ndio ajenda muhimu?

Haoni kuwa anatuondoa kwenye hoja iliyo mezani ili kuipa unafuu serikali inayokosolewa na Lissu?

Lakini nina tatizo kubwa zaidi na umakini wa mtazamo wa Ansbert dhidi ya Lissu.

Napendekeza kwamba Ansbert ni mnafiki asiyekubali kujisahihisha hata anapopewa ushahidi mpya.

Ni kama vile ni mhanga wa Kripkean dogmatism.

Yeye Ansbert anamuunga mkono Mbowe kwa sababu kwamba Mbowe ni bora kuliko Lissu?

Alitaka Mbowe aendelee kuongoza chama na agombee Urais Kwa sababu hiyo?

Hapana. Kuna tatizo katika mtirirko wa fikra za Ansbert. Ni tatizo la unafiki dogmatika.

Ansbert alisafirishwa na Mbowe hadi Ulaya alikokuwa anasoma Mbowe. Akapangiwa hoteli na kulipwa DSA kwa muda wote aliokuwa huko.

Akapewa ajira ya kufanya Homework zote za Mbowe. Mbowe akawa anasaini na kufanya submission chuoni.

Hatimaye Mbowe akapa degree kutokana na akili ya Ansbert.

Ikapatikana degree ya Ansbbert Ngurumo aka Freema Mbowe.

Sasa Ansbert anatwambia Mbowe ni bora kuliko Lissu. Eti Lissu hawezi chochote, Mbowe ni mweza yote.

Ansbert anahangaika kumchafua Lissu na kumtakasa Mbowe mwenye vyeti vya degree feki.

Huu ni unafiki wa hatari nisioukubali.

Simkubali Ansbert katika unafiki huu.

Anamkosoaje kiongozi hajakaa ofisini hata kwa miezi mitatu?

Kwa kutumia ushahidi gani?

Yeye Ansbert kama anajua siasa mbona aligombea ubunge na kupata kura za rasha rasha?

Au anasahau sababu iliyomkosesha kura za kutosha?

Ansbert alikuwa anakaa hotelini Bukoba mjini, wakati site ya kampeni ni Muleba jimboni kwake.

Wapiga kura wake wa Muleba wakasema hawamtaki mbunge anayekaa hotelini Bukoba mjini.

Naona hadi sasa hajabadilika kifikra.

Kwa sasa chadema wanahitaji think tank makini. Yeye bado yuko huko Ulaya anaruka ruka.

Badala ya kuongea kuhusu mambo kama haya Ansbert anabaki kwenye masimango, kejeli na majigambo ya kifalsafa kupitia mitandao ya kijamii.

Sio sawa.

Hapana.

Screenshot_20250705_211541_Chrome.jpg
 
Huyo Mhaya ni mjuaji na mnafiki sana. No reform No election ilikuwa ni slogan ya Makengeza kupiga hela ya CCM .
Pumbavu zake na Mbowe wake.
Mkerewe huyo, hakuna mhaya mjinga hivyo.
 
Huyu ni Ngurumo yupi, mimi namjua yule wa Msondo ngoma na naamini ni hayati kwa sasa
Huyu ni ngurumo aliyekuwa mseminari akisomea upadri; alifukuzwa akiwa seminari kuu, na kuukosa upadri.

Sababu za kufukuzwa sizifahamu.
 
Mbowe ni Mwanafunzi mwenye akili aliyegomea kushirikiana na wenzake akaamua kukaa pembeni akiombea mwanafunzi aliyemfunika siku moja tu afeli,
Kisha ithibitike kuwa heye Mbowe alikuwa juu sana.
Hiyo si sawa,
Huyu mwanafunzi mtundu aliwajibika sana kwenye assignment zilizombeba Mbowe.

ieleweke mwanafunzi huyu mtundu hatashindwa!
 
Sasa yeye anasemaje kuhusu uuchaguzi? Je, CHADEMA washiriki hivyo hivyo tu bila kujali mapungufu yaliyopo kwenye taratibu za uchaguzi? Hili la CHADEMA kutoshiriki uchaguzi wako sahihi!
Huwezi kuishinda CCM nje ya bunge
 
Back
Top Bottom