Rais Magufuli kakosea sana kwenye suala la PR kwa kudai COVID-19 haipo nchini.
Huwezi kudai kitu hakipo, hususan ugonjwa unaosababishwa na ki/virusi [ambavyo havionekani], bila ushahidi.
Rais Magufuli ni mwanasayansi wa wapi yeye?
Mimi bado naamini C-19 si kali wala hatari kama inavyotangazwa, lakini hiyo haina maana watu wasichukue tahadhari, hususan wale walio medically fragile.
Nani alisema watu wasichukue tahadhari? Rais hajawahi kusema kuwa Tanzania hakuna corona! Ndiyo maana mwaka Jana shule na vyuo vilifungwa.
Lakini anachokisema Rais Ni kwa sisi k ama Tanzania hatutaiga Wala kushinikizwa tufuate mbinu na taratibu za kupambana na corona za mataifa mengine. Tutatumia mbinu zinazoendana na Hali halisi ya mazingira yetu na hali yetu. Ndio maana tulikataa lockdown na tukaacha kutangaza data za Corona kwa sababu zilikuwa zinatumiwa kuleta hofu
na wazungu walikuwa wanasema kabisa kuwa tutaokota miili barabarani.
Utaratibu uliotumika kwanza ni kuomba Mungu aliyeumba mbingu na nchi ili atuponye na corona Kisha kuchukua tahadhari zinazoendana na Hali na mazingira yetu Kama kunawa mikono, kutumia barakoa za kujishonea wenyewe nk.
Matokeo yake Mungu alituponya na corona, shule na vyuo vikafunguliwa na maisha yakaendelea Kama kawaida.
Mwaka huu limekuja tena wimbi jipya la corona duniani. Virusi wa aina mpya toka Uingereza na Afrika ya kisini.
Rais akasema utaratibu tuliotumia mwaka Jana na Mungu akatuponya tuutumie Tena mwaka huu. Maombi yakaitishwa na tahadhari Kama mwaka Jana tunachukua. Kile tulichokikataa mwaka Jana na mwaka huu tumekikataa!! Kama Mungu alivyotuponya mwaka Jana na mwaka huu atatuponya!!
Huyo anayelia kuwa amefiwa na baba yake kwa tatizo la kupumua kwanza nampa pole. Kisha namwuliza swali unadhani Kama ungekuwa unaishi Marekani na ulaya wanakotangaza data za Corona na kufanya lockdown baba yako asingeumwa corona? Mbona huko unakosifia ndiko Kuna maambukizi na vifo vya Corona kwa mamia na maelfu kila siku?? Maana yake ni kuwa mbinu yao haijawasaidia wao, itawezaje kutusaidia sisi? Wapambane kivyao na sisi tutapambana kivyetu mwisho wa siku tutaona mbinu ambayo ilikuwa sahihi!
Lakini mpaka sasa Tanzania tuko salama Sana!! Hao wengine wanatuonea wivu! wanataka tutumie mikakati ambayo hata wao haijawasaidia!