Samahani kwa kukosea jina. Lakini hiyo Nyani ndiyo inayonikwaza, hasa kwa kuangalia tabiia ya nyani kwa sisi wakulima wa nyanda za juu kusini.
Nakubaliana nawe kwa 100% juu ya wajibu wetu. Lakini ufahamu kuwa katika jamii luna watu wa aina zote. Ndiyo maana mpaka kwenye majumba yetu tunaweka na mageti kwa sababu kuna irresponsible citizens.
Katika jamii kuna watu ni werevu, hawahitaji hata kufundishwa, kuna wanaohitaji elimu kisha wanabadilika, kuna wenye uelewa mdogo ni lazima wasukumwe, na kuna wabishi ambao ni lazima walazimishwe.
Kama Serikali isipofanya kitu, bita hii itapiganwa na hilo kundi la kwanza pekee. Na hilo kundi pekee haliwezi kufanikiwa kwa sababu jitihada zake zitaharibiwa na haya makundi mengine.
Fikiria unaenda kwenye basi, umejitahidi kutazama basi ambalo halijajaza abiria, mnaanza safari, dereva anasimama kila mahali hata wakati basi limejaa, wapiga debe wanazidi kuita abiria, nao kwa kuw ni wa yale makundi mengine, wanazidi kuingia, wewe uliyeingia mwanzoni, utafanya nini? Mazingira kama hayo, unahitaji mkono wa Serikali.