Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

modeators huu upuuzi umekuwa ukiletwa mara kwa mara unafutwa analeta tena/Unaona kabisa uzushi moderators dont tolerate vitu kama hivi

Unaonaje kabisa kwamba "huu ni Uzushi"?

Unapouita Uzushi ni Vyema wewe ukaweka ukweli wenye kuthibitisha kuwa huo ni Uzushi otherwise huo wako nao unakuwa ni uzushi wenye lengo la kujitetea tu.
 
Liongo hili jamaa. We ushakimbia nchi unawashwawashwa na nini. Mambo ya huku tuachie sie wenyewe maadam we yashakushinda.
Wenye akili tumeshamshtukia zaidi, anajenga mazingira ya kupata hifadhi ya kudumu ya ukimbizi kwa kuichokoza serikali kwa kuandika habari za uzushi.
Ni wazi akiandika habari za kizushi, serikali itamtafuta na yeye atatumia hilo gepu kudai anatafutwa, ila wa nchi za magharibi sio wajinga kama anavyodhani.
 
serikali na CCM naona sasa ina masemaji mpya ndugu cyprian msiba kwa heli dkt abbas,msigwa na polepole
 
Watu wajinga kufanya mambo ya kijinga kwa watu welevu. ni sawa na kutembea uchi.
 
Wenye akili tumeshamshtukia zaidi, anajenga mazingira ya kupata hifadhi ya kudumu ya ukimbizi kwa kuichokoza serikali kwa kuandika habari za uzushi.
Ni wazi akiandika habari za kizushi, serikali itamtafuta na yeye atatumia hilo gepu kudai anatafutwa, ila wa nchi za magharibi sio wajinga kama anavyodhani.
Halafu linaonekana linaamini sana ushirikina
 
Inamaana amezipata hizi taarifa akiwa huko ugaibuni? Kama ni hivyo sasa nihatari,nani amemfikishia taarifa za kikao hicho? Kwa kifupi kuna uvujaji mwingi sana wa taarifa kama ni hivyo,haiwezekani mtu yuko ugaibuni akaqeza kudukua siri za vikao hapa kwetuu
Sio kila mtu anakubaliana na udhalimu Hata uko serikalini wako wengi wanaoitakia mema nchi yetu Ndo mana wanatoa hizo taarifa ili huo ushetani usifanikiwe
 
Alikuwa Wakwanza kutujuza maazimio ya Kikao kilichoketi (Ukumbi wa BOT) na kuazimia Viongozi wakuu wa CHADEMA wakamatwe wapelekwe mahakamani na kunyimwa dhamana.

Ikatokea exactly sawa na vile alivyoeleza kabla.


Hivyo anafaa kuaminika!
 
modeators huu upuuzi umekuwa ukiletwa mara kwa mara unafutwa analeta tena/Unaona kabisa uzushi moderators dont tolerate vitu kama hivi
Vp kuhusu ule upuuzi wa Musiba?? Mimi nionavyo tulikofikia sasa kila mmoja aseme imetosho bila kujali ni waupande gani. Tusipofanya hivyo tukabaki kuwashangiliaji na wandaaji wa maovu dhidi ya Wtz wenzetu basi huko mbeleni tusihangaike kumpata mchawi.
 
Hakuna siri tena. Leo tarehe 30:03:2018, saa tisa kamili (9:00) alasiri, saa ambayo Bwana Yesu Kristo alikata roho msalabani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika muda ule ule, Paul Makonda, alikuwa anafungua kikao maalumu cha kupanga mambo maovu dhidi ya viongozi waandamizi wa Chadema na wakosoaji wengine wa serikali. Kikao hicho, ambacho alikiita kikao cha “ulinzi na usalama,” katika ukumbi wa polisi Kurasini, kiliahirishwa saa moja kamili (1:00) usiku.
Katika kikao hicho, yalijadiliwa mambo mengi mazito.

Nimechagua machache tu yafuatayo, ndiyo nitaweka bayana, ili kuonyesha dunia jinsi kiburi, jeuri, sifa na madaraka ya watu wawili (JPM na Makonda) vinavyohatarisha usalama wa taifa letu. Mengine yanafanyiwa kazi na vyombo muhimu.

1. Mbali na Freeman Mbowe na viongozi wenzake walio gerezani Segerea, wengine waliojadiliwa na kikao hiki, ambao watakamatwa muda wowote kuanzia sasa ni wabunge: Godbless Lema (Arusha), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Esther Bulaya (Bunda), Joseph Selasini (Rombo), na kiongozi wa Jumuiya za Kiislamu, Ustadhi Rajab Katimba. Eti hawa ni "majasusi wa Chadema!"

2. Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Bw. Cyprian Musiba, ambaye amekuwa anakutana na waandishi wa habari na kutoa matamko ya shari na tuhuma kali dhidi ya watu wanaokosoa serikali. Alikuwa kikaoni - kikao cha “ulinzi na usalama” mkoa wa Dar es Salaam. Katika moja ya hoja zake, alisema Ansbert Ngurumo anachafua serikali akiwa huko Ulaya; na kwamba ingekuwa vema serikali iweke utaratibu wa kumfuatilia huko aliko na kumdhibiti. Baadhi ya wajumbe walisema hakuna haja, bali serikali ibane hawa hawa waliopo nchini, hasa Heche na Lema. Hasira dhidi ya Lema zilitokana zaidi na kauli yake kutaja Dk. Modestus Kipilimba kwamba anashinikizwa na kushirikishwa katika kupanga mateso dhidi ya wapinzani. Mbali na kusaka fursa ya kumtesa, wanatengeneza “mabomu” dhidi ya mbunge huyo wa Arusha.

3. Wamekerwa na suala la ugonjwa wa Abdallah Mtulia (mbunge wa Kinondoni) kujulikana, wakadai kwamba ugonjwa wake umesababishwa na Chadema. Mtulia ana hali mbaya hospitalini. Makonda na Musiba wamejiapiza kuwa watapambana na Chadema kwa mbinu zote kwa kutumia dola na "uchawi."

4. Kesi ya Mbowe inawapasua kichwa, inawatia hofu (kwa sababu ni ya kubumba); hata mawakili wa serikali wamesema wanalinda hadhi ya taaluma yao, hawataki kuchafuka au kuchafua taaluma zao kwa kesi za kubumba za polisi.

5. Serikali inakerwa mno na taarifa za vikao vyao vya siri kuvuja, na jambo hili linawafanya wachelewe kutekeleza uovu wao wanaopanga dhidi ya Mbowe. Wamesema zamu hii watakuwa makini zaidi.

Yapo mengi, lakini haya ndiyo nimeona vema niyaanike hapa, ili Watanzania na dunia nzima ijue kinachoendelea nyuma ya pazia, wajue aina ya “viongozi” walionao, na wajue nani anahatarisha usalama wa nchi. Hivi ndivyo Bashite na kikosi chake walivyoadhimisha Ijumaa Kuu – kwa kumkejeli Mungu!

MASWALI MAGUMU:
a) Bado Watanzania mnajiuliza nani anamtuma Musiba kufanya press conferences na kutoa matamko ya kushambulia watu kwa tuhuma za ajabu ajabu?
b) Bado mnataka kujua mamlaka inayomlinda Musiba?
c) Idara ya Usalama wa Taifa haijui haya au imenyosha mikono, inafuata maagizo, na imeamua kuacha hatima ya usalama wa nchi hii mikononi mwa watu wawili?
d) Kuna mtu anadhani Makonda anafanya haya kwa hiari yake tu, bila idhini na baraka za Rais Magufuli anayesema maneno ya ajabu dhidi ya wapinzani na wakosoaji wake, hadharani bila aibu, kwamba, “sijaribiwi…. nitawavunja miguu?”
e) Kwa mikakati hii, kwa kuhatarisha badala ya kulinda uhai na usalama wetu, rais anadhani nchi iko salama, na yeye mwenyewe yuko salama?
f) Wakati uovu huu unapangwa rasmi, Rais Magufuli alikuwa kanisani kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, “anasali.” Je, naye alibusu msalaba? Kama ndiyo, busu lake lina tofauti gani na busu la Yuda kwa Bwana Yesu – busu la usaliti kwa Watanzania alioapa kuwalinda?
g) Mateso na vifo vya wapinzani na wakosoaji wake ndiyo zawadi ya Pasaka ambayo rais anaandalia Watanzania mwaka huu 2018?
h) Kama utawala wa Kaisari uliangukwa kwa sababu ya kiburi, jeuri na ulevi wa madaraka, utawala wa Magufuli utanusurika vipi ukiwa na sifa zile zile?

Mengine nabaki nayo. Tuendelee kutafakari haya.

Ansbert Ngurumo
MHARIRI BILA MIPAKA (MBM)
Endelea kudanganya...wenzio.
Ni kweli siasa sio kama zamani
Na maisha ni magumu mtaani
Ila hayo uyasemayo ni ya kuzua.na anayekutumia taarifa hizo ...mtilie shaka
 
Watu wajinga kufanya mambo ya kijinga kwa watu welevu. ni sawa na kutembea uchi.
Msiba anawadharau watanzania sana, anadhani watanzania ni wajinga kiasi anachofikiri anadhani kila Uzushi anaotengeneza wataukubali, kusadiki na kuamini, Watanzania wa sasa wapo makini na idadi kubwa wanajielewa na wanajua kutafakari kila propaganda ya wapambe wa Naibu Rais ndugu Bashite na kuzipima kisha kutulia kuwachora wakihangaika kuichafua chadema, hakuna ubaya usiokuwa na mwisho na sasa pengine ubaya inaelekea mwisho kwani Adui wa chadema wameanza kuanikwa live na Mungu ni bahati kubwa waliokuwa wakifanya gizani sasa wanaongea live.
 
Back
Top Bottom