mifano yako na maswali yako ni ya kishamba shamba hakuna haja ya kukujibu wewe kilaza fala nenda kalale msiba akupe mimba, hizo Roho zenu mbaya za kutetea Udikteta na upumbavu wa CCM na Maliyamungu Bashite zina mwisho wake, walikuwepo madikteta wanyama kuliko hao boss zako wapo wapi leo?
Unaona? Hata maana ya Dikteta yenyewe huijui. Nenda Syria ukapigane kama unataka. Huko ndiyo utakutana na dikteta wako Asad. Usimpake matope kiongozi wetu kwa vile mfuasi wenu Lissu kamwita dikteta uchwara. Nyie ni waathirika wake.
Saud Arabia inawatafuta watu kama nyie wa kwenda kwenye vita dhidi ya Iran na Isbolah. Mtalipwa hela nyingi dhidi ya hata hizo mnazo zisotea kwa CHADEMA!
Sisi hatuna mpango huo. Sisi tuna taka maendeleo. Nchi yetu imekuwa inaibiwa na kudhulumiwa. Hata wakenya watu ambao wana ubaguzi wa makabila mpaka karne hii ya 21 wana tushinda, wakati hawana kitu, halafu wewe unakuja na mawazo ya kimasikini ya kuona kuwa una nyanyaswa na Magufuli kwa kukuambia tu ufanye kazi kwa bidii na kuwa na nidham?
Kama umeshindwa maisha walaumu wazazi wako kuto kukupeleka wewe shule. Mimi nilipata bahati ya kusomeshwa na Nyerere mpaka advanced level. Sijui kama una mjua. Namshukuru Mungu. Mengine mpaka kwenda kusoma Ulaya ni jitihada zangu mwenyewe.
Kwa taarifa yako tu mkuu, mimi ningekuwa kijana mwenye nguvu kama wewe na ukaniuliza mfumo upi wa maisha ningependa Tanzania uwe nayo kati ya ule wakati wa Kikwete na ule wa Magufuli automatically ningependelea maisha katika mfumo wa Magufuli hata kama ni Dikteta uchwara kama wewe unavyo m-regard.
Mimi nime ishi Bongo na nimepata bahati pia kuishi Europe na kufanya kazi huko. Sio kazi ya kubeba ma-box. Na sasa nimerudi Bongo tena. Na nina uwezo wa kwenda Ulaya wakati wowote ule ninao utaka kulingana na uwezo wangu. Huo ni uthibitisho tosha kuwa mimi hizi systems mbili nazijua na naweza zilinganisha. Sijui kama na wewe mwenzangu nawe umebahatika hivyo kama mimi.
Nachoweza kukuambia ni kuwa Magufuli sio dikteta. Magufuli ni mzalendo wa kupindukia, lakini anashindwa kuelewa kwa nini sisi watanzania pamoja na neema yote hii tuliyopewa na mungu tumeshindwa jitegemea wenyewe na kujilisha wenyewe badala yake tulikuwa omba omba?
Zingatia kuwa omba omba yetu ndiyo hali iliyo ifanya nchi yetu isiwe na nguvu ya kuzuia dhulma ambazo zilikuwa zina fanywa na mabepari kwa kuwatumia watantanzania wenzetu. Ilikuwa weak.
Nchi yetu ilikuwa imevamiwa na wezi wa kila aina. Wazungu, wahindi, wapakstani, wabangladeshi, wamasirilanka na waarabu na wakaja wa kutoka Kongo na Kenya pia. Hawakuwa na una nzuri walikuwa na madhumuni ya kutufirisi sisi.
Utakumbuka kuwa wakati wa ubinafsishaji wa viwanda vyetu na mashirika yetu ya umma kama Railway, TTCL, baadhi ya mabenki na kadhalika ambavyo ndiyo vilikuwa vitega uchumi wa nchi yetu ambavyo Mwalim Nyerere alivianzisha wahindi wengi wakishirikiana na watanzania wenzetu wali vinunua kwa misingi ya kuviendesha kwa ufanisi mkubwa.
Mambo lakini hayakwenda kama watanzania tulikuwa tumetarajia. Kiwanda kimoja baada ya kingine kilikufa na mashirika yetu ya umma kama TTCL, Bandari na mengineyo ku-perform vibaya sana.
Hao walio jiita wadau walijikuta wakifanya biashara za ovyo za kuingamiza nchi yetu kiasi kwamba hakuna kitu kilikuwa kinaenda bara bara. Baadhi ya watanzania wetu ndiyo walikuwa wako tayari kutuangamiza. Unafikiri kama vita ingetokea ungewaona? Wangekimbilia kwao au kuomba ukimbizi nchi nyingine na kula pesa ambazo wametuibia. Wewe na mimi kama wewe ni mtanzania kweli tungehangaika hapa na familia zetu. Au kuuana wenyewe kwa wenyewe.
Aisee! Tulikuwa katika hali mbaya sana kitaifa. Kama wewe binafsi ulikuwa katika hali nzuri na sasa kwa ajili ya Magufuli umeporomoka basi nakupa pole. Kiinchi tuliangamia sana. Na maisha hayakuwa bora. Uliyaona bora kwa vile labda wengi wetu walihisi wana pesa lakini country wise tuliangamia sana.
Hatukuwa na utawala wala system bora. Kila mmoja alifanya alivyotaka.
Vyombo vya dola vilikuwa kwa ajili ya viongozi tu. Umesha ona au kusikia mtu kakamatwa na polisi huyo mtu akimkemea polisi? Hiyo ilikuwa Tanzania tu. Hata polisi walikuwa hawana wajibu.
Kwa nini nakueleza hayo ni kwamba nchi nyingi za Ulaya na Amerika sisi watanzania tukisafiri nje walikuwa wanatu-suspect sana kuwa ni wauza unga au manjangili wa namna fulani. Hawakuwa na imani na sisi. Sijui kama hayo mambo wewe binafsi ume ya experience?
Sina haja ya kukueleza mengi, nafikiri umeshuhudia mwenyewe mambo yaliyo kuwa yanatokea bandarini kwa mfano.
Any way! Kama mifano yangu kwako ni irrelevant basi sijui nini cha kukusaidia. Maana itakuwa sawa na kumpigia mbuzi gitaa akakutazama tu unacho fanya.
Ila najua kwa jinsi mishipa yako ilivyo komaa kuwa Magufuli ni dikteta wakati huna referances zozote zile international wise ni tatizo kweli kweli. Inaonyesha jinsi gani umekuwa clever.
Unajua kumwita Rais dikteta sio kitu rahisi. Ni upuuzi na ignorant wa hali ya juu. Inaonyesha elimu uliyo nayo ni ya aina gani. Ungekuwa una elimu mzuri usinge tumia neno hilo. Mimi binafsi siwezi tumia hilo neno. Ni neno zito sana. Ukimwita Rais dikteta inabidi utoe visibitisho kuwa kweli yeye ni dikteta.
Kusema tu nani kapotea na nani kapigwa risasi basi Rais amehusika hiyo ni verry cheap.