Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

Wanabodi

Vinyweoeo vya mwili vyanisimama nikisikia haya, nadhani ni wakati sasa serikali kufanya jambo dhidi ya hawa wazushi mwitu. Wanamapinduzi wa kwenye keyboard, waliokimbilia ughaibuni na sasa wanataka tutifuane ili wao walipwe unono na waliowatuma.

Sawa bwana sisi hatupingi kila kitu na pale tunapoona kuna jambo haliendi sawa tunatafuta namba sahihi ya kuliwasilisha na sio kwa tungo kama zetu watu wa ughaibuni.

Kuna watu watatu katika list na wote mko ughaibuni, Chahali, Ansbert Ngurumo na Mange Kimambi hapo huyu ni mbea zaidi kkuliko mwanaharakati
 
Unaona? Hata maana ya Dikteta yenyewe huijui. Nenda Syria ukapigane kama unataka. Huko ndiyo utakutana na dikteta wako Asad. Usimpake matope kiongozi wetu kwa vile mfuasi wenu Lissu kamwita dikteta uchwara. Nyie ni waathirika wake.

Saud Arabia inawatafuta watu kama nyie wa kwenda kwenye vita dhidi ya Iran na Isbolah. Mtalipwa hela nyingi dhidi ya hata hizo mnazo zisotea kwa CHADEMA!

Sisi hatuna mpango huo. Sisi tuna taka maendeleo. Nchi yetu imekuwa inaibiwa na kudhulumiwa. Hata wakenya watu ambao wana ubaguzi wa makabila mpaka karne hii ya 21 wana tushinda, wakati hawana kitu, halafu wewe unakuja na mawazo ya kimasikini ya kuona kuwa una nyanyaswa na Magufuli kwa kukuambia tu ufanye kazi kwa bidii na kuwa na nidham?

Kama umeshindwa maisha walaumu wazazi wako kuto kukupeleka wewe shule. Mimi nilipata bahati ya kusomeshwa na Nyerere mpaka advanced level. Sijui kama una mjua. Namshukuru Mungu. Mengine mpaka kwenda kusoma Ulaya ni jitihada zangu mwenyewe.

Kwa taarifa yako tu mkuu, mimi ningekuwa kijana mwenye nguvu kama wewe na ukaniuliza mfumo upi wa maisha ningependa Tanzania uwe nayo kati ya ule wakati wa Kikwete na ule wa Magufuli automatically ningependelea maisha katika mfumo wa Magufuli hata kama ni Dikteta uchwara kama wewe unavyo m-regard.

Mimi nime ishi Bongo na nimepata bahati pia kuishi Europe na kufanya kazi huko. Sio kazi ya kubeba ma-box. Na sasa nimerudi Bongo tena. Na nina uwezo wa kwenda Ulaya wakati wowote ule ninao utaka kulingana na uwezo wangu. Huo ni uthibitisho tosha kuwa mimi hizi systems mbili nazijua na naweza zilinganisha. Sijui kama na wewe mwenzangu nawe umebahatika hivyo kama mimi.

Nachoweza kukuambia ni kuwa Magufuli sio dikteta. Magufuli ni mzalendo wa kupindukia, lakini anashindwa kuelewa kwa nini sisi watanzania pamoja na neema yote hii tuliyopewa na mungu tumeshindwa jitegemea wenyewe na kujilisha wenyewe badala yake tulikuwa omba omba?

Zingatia kuwa omba omba yetu ndiyo hali iliyo ifanya nchi yetu isiwe na nguvu ya kuzuia dhulma ambazo zilikuwa zina fanywa na mabepari kwa kuwatumia watantanzania wenzetu. Ilikuwa weak.

Nchi yetu ilikuwa imevamiwa na wezi wa kila aina. Wazungu, wahindi, wapakstani, wabangladeshi, wamasirilanka na waarabu na wakaja wa kutoka Kongo na Kenya pia. Hawakuwa na una nzuri walikuwa na madhumuni ya kutufirisi sisi.

Utakumbuka kuwa wakati wa ubinafsishaji wa viwanda vyetu na mashirika yetu ya umma kama Railway, TTCL, baadhi ya mabenki na kadhalika ambavyo ndiyo vilikuwa vitega uchumi wa nchi yetu ambavyo Mwalim Nyerere alivianzisha wahindi wengi wakishirikiana na watanzania wenzetu wali vinunua kwa misingi ya kuviendesha kwa ufanisi mkubwa.

Mambo lakini hayakwenda kama watanzania tulikuwa tumetarajia. Kiwanda kimoja baada ya kingine kilikufa na mashirika yetu ya umma kama TTCL, Bandari na mengineyo ku-perform vibaya sana.

Hao walio jiita wadau walijikuta wakifanya biashara za ovyo za kuingamiza nchi yetu kiasi kwamba hakuna kitu kilikuwa kinaenda bara bara. Baadhi ya watanzania wetu ndiyo walikuwa wako tayari kutuangamiza. Unafikiri kama vita ingetokea ungewaona? Wangekimbilia kwao au kuomba ukimbizi nchi nyingine na kula pesa ambazo wametuibia. Wewe na mimi kama wewe ni mtanzania kweli tungehangaika hapa na familia zetu. Au kuuana wenyewe kwa wenyewe.

Aisee! Tulikuwa katika hali mbaya sana kitaifa. Kama wewe binafsi ulikuwa katika hali nzuri na sasa kwa ajili ya Magufuli umeporomoka basi nakupa pole. Kiinchi tuliangamia sana. Na maisha hayakuwa bora. Uliyaona bora kwa vile labda wengi wetu walihisi wana pesa lakini country wise tuliangamia sana.

Hatukuwa na utawala wala system bora. Kila mmoja alifanya alivyotaka.
Vyombo vya dola vilikuwa kwa ajili ya viongozi tu. Umesha ona au kusikia mtu kakamatwa na polisi huyo mtu akimkemea polisi? Hiyo ilikuwa Tanzania tu. Hata polisi walikuwa hawana wajibu.

Kwa nini nakueleza hayo ni kwamba nchi nyingi za Ulaya na Amerika sisi watanzania tukisafiri nje walikuwa wanatu-suspect sana kuwa ni wauza unga au manjangili wa namna fulani. Hawakuwa na imani na sisi. Sijui kama hayo mambo wewe binafsi ume ya experience?

Sina haja ya kukueleza mengi, nafikiri umeshuhudia mwenyewe mambo yaliyo kuwa yanatokea bandarini kwa mfano.

Any way! Kama mifano yangu kwako ni irrelevant basi sijui nini cha kukusaidia. Maana itakuwa sawa na kumpigia mbuzi gitaa akakutazama tu unacho fanya.

Ila najua kwa jinsi mishipa yako ilivyo komaa kuwa Magufuli ni dikteta wakati huna referances zozote zile international wise ni tatizo kweli kweli. Inaonyesha jinsi gani umekuwa clever.

Unajua kumwita Rais dikteta sio kitu rahisi. Ni upuuzi na ignorant wa hali ya juu. Inaonyesha elimu uliyo nayo ni ya aina gani. Ungekuwa una elimu mzuri usinge tumia neno hilo. Mimi binafsi siwezi tumia hilo neno. Ni neno zito sana. Ukimwita Rais dikteta inabidi utoe visibitisho kuwa kweli yeye ni dikteta.

Kusema tu nani kapotea na nani kapigwa risasi basi Rais amehusika hiyo ni verry cheap.
 
Kitu gani majuzi alikisema kikatokea?
 
Wewe fala ujue ni kilaza sana hiyo shule ulifuata nini? Mbona Ubongo wako ni mdogo kama wa gendere? Unajiita msomi lakini wewe ni bonge la mbumbu fulani na zuzu la kutupwa na CCM inafeli kwa kuwakumbatia majuha kama nyie, mifano yako ya Nchi zenye vita umeshindwa kutambua kuwa huko vita vilianzishwa baada ya serikali kubaka Demokrasia na kufanya Udikteta wa kishamba kama wenu na wakoloni wasukuma wawili washamba toka kolomije na chato, Chanzo cha ujinjifu wa Amani ya Tanzania ni upumbavu wenu CCM na nyie Madalali wa siasa mliojazana huko CCM mnatengeneza miladi ya kuvuna pesa kwa kisingizio cha kuzitumia kudhoofisha, kuua upinzani ili mpate cha juu 10% matokeo yake mnaifanya CCM kuvuruga Aman alafu unakuja na mifano yako ya kijuha juha hapa, Tambua kuwa watanzania wameamka hawana mda wa kuendelea kuwaamini CCM tena wapo busy kubuni mbinu za kujinasua toka kwenye Ukoloni wenu unaoongozwa na Naibu Rais Maliyamungu idd Amin Bashite na Mtukufu malaika toka chato, hakuna mabaya yasiyo na mwisho, walikuwepo akina Bokasa, Sadam Husein, Mabutu, Abacha, Chiluba, Gadafi, idd Amin Dada wapo wapi sasa? hata wewe fanya ufala wako na Heri Kisanduku Makapero lakini mwisho wenu haupo mbali.
 
Hata Idi Amini alikuwa na wafuasi.
 

HII POST IMEKAA KIKADA/ KICHAMA SANA
 
Kwa hiyo mnamuiga Msiba?
 
Kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano iliwapasa watawala wajue impact yake kwa matendo yao. Ni zaidi ya hiki kitu kinsitwa udalama wa taifa.
 
yakiandikwa na mwanakijiji au nyani ngabu unasappoti, ya ngurumo siyo??
Ukiamua kupigania uhuru kwa kuwatelekeza wenzako, halafu unajidai shujaa ukiwa nje ya nchi, thamani yako inakuwa ndogo sana! Mwambieni awe Mandela. Huo siyo umri wa kutimukia ulaya.
 
Utaninisamehe sana, siwezi poteza mda wangu kurumbana na primitive creature ambacho hata madhumuni ya kile anacho gombania hakijui.

Wewe baki na uelewa wako wa mapambano dhidi ya maendeleo, mwishoni tutajua nani ameshinda maendeleo au upuuzi wenu.

Nakutakia mafanikio mema!!!
 
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] Yaani wewe ni zezeta wa kupindukia. Kichwani naona in maluilui.
Ebu mtafute Dr akusaidie kwa tiba.

Uko nje Kabisa ya stream. Umeamka kutoka usingizini nini?
utachukua muda sana kumwelewa huyu great thinker kwa sababu una mental disorder
 
Amani ya nchi yetu Tanzania ni muhimu sana kuliko kitu chochote hivyo lazima ilindwe kwa gharama yoyote ile. Kamwe tusiwachekee wanao tamani tuingie ktk machafuko kwa hisia zao.
 
Huwezi kupoteza mda upi? wewe ni kula kulala bure kwa Le mutuz huku ukipakatwa na Msiba, mda unao mwingi kwani wewe ni fala huna kazi ya kufanya zaidi ya kukariri ujinga hapo Gheto, nani anapambana dhidi ya maendeleo? Vurugu za CCM kwa Wapinzani ndiyo sumu ya maendeleo, kikwazo cha maendeleo Nchini ni CCM, pesa za viwanda, pesa za Umma, pesa za walipa kodi, zote wanachukua kununua ndege kienyeji kulipa madeni ya uzembe wa magufuli pindi akiwa waziri wa ujenzi , kuwanunua wabunge, madiwani, kurudia uchaguzi kwa gharama kubwa, CCM wanatumia pesa za Umma kwa mambo ya hovyo hovyo sana, miaka 50 Nchi haina maendeleo pesa zote CCM wanazitumia kukandamiza Demokrasia, kuwabambikia kesi, kuwapiga Risasi, kuwafunga jela Wapinzani, ebu sema unatakaje? Unataka chadema wafumbie macho unyanyasaji wa CCM? Unataka chadema wakubali kila mnalotaka? Mmezuia mikutano ya siasa kwa Wapinzani lakini CCM wao wapo free kufanya mikutano hata usiku, jaribu kuwambia hao Boss zako kuwa watanzania wa sasa wameamka wanajua kila kitu hwadanganyiki kwa sera za kibabe za Naibu Rais Maliyamungu Bashite.
 
Amani ya nchi yetu Tanzania ni muhimu sana kuliko kitu chochote hivyo lazima ilindwe kwa gharama yoyote ile. Kamwe tusiwachekee wanao tamani tuingie ktk machafuko kwa hisia zao.
CCM ndiyo chanzo cha uvunjifu wa Amani ya Tanzania kwani bila CCM kuwafanyia virugu Wapinzani kusingekuwa na hizo tetesi na uoga wenu, na endapo ikitokea Aman kuvurugwa wa kulaumiwa atakuwa CCM kwani ndiyo chanzo cha ubaya wote nchini, bila CCM kuzuia mikutano ya siasa kuwanyanyasa wananchi kusingekuwa na lawama yeyote kwani Wapinzani wangetema nyongo Live na watanzania wangepima wenyewe kwa Amani.
 
Mkuu,jamaa anaumwa nini tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…