Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katika kipindi hiki cha vuguvugu la kisiasa nchini Tanzania, sakata la kukamatwa na kupigwa kwa viongozi na wanachama wa Chadema waliokusanyika Mbeya Agosti 11, 2024, lilizua gumzo kubwa. Mchungaji Anthony Lusekelo, maarufu kama Mzee wa Upako, naye hakuachwa nyuma katika kutoa maoni yake kuhusu tukio hilo, nakuzungumza kwa ujasiri na kuonesha msimamo wake kwa wazi.
Mzee wa Upako, alieleza kuwa endapo angekuwa na mamlaka kama ya Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadhi Haji, ambaye alihusika katika hatua ya kuwakamata na kuwapiga viongozi na wanachama wa Chadema waliokusanyika siku hiyo, angefanya sawa na Kamishna huyo.
"Kama mimi ningekuwa na jukumu la oparesheni maalum, ningefanya kama alivyofanya Awadhi Haji. Serikali ilishatoa agizo kuwa wasiende Mbeya, lakini bado wakaenda. Ningewakamata pia, ila nisingewafunga kwa muda mrefu. Badala yake, ningewatandika tu, lakini si sana"
Chanzo: Jambo Tv