Anthony Lusekelo atoa msimamo mkali sakata la Chadema Mbeya

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Katika kipindi hiki cha vuguvugu la kisiasa nchini Tanzania, sakata la kukamatwa na kupigwa kwa viongozi na wanachama wa Chadema waliokusanyika Mbeya Agosti 11, 2024, lilizua gumzo kubwa. Mchungaji Anthony Lusekelo, maarufu kama Mzee wa Upako, naye hakuachwa nyuma katika kutoa maoni yake kuhusu tukio hilo, nakuzungumza kwa ujasiri na kuonesha msimamo wake kwa wazi.

Mzee wa Upako, alieleza kuwa endapo angekuwa na mamlaka kama ya Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadhi Haji, ambaye alihusika katika hatua ya kuwakamata na kuwapiga viongozi na wanachama wa Chadema waliokusanyika siku hiyo, angefanya sawa na Kamishna huyo.

"Kama mimi ningekuwa na jukumu la oparesheni maalum, ningefanya kama alivyofanya Awadhi Haji. Serikali ilishatoa agizo kuwa wasiende Mbeya, lakini bado wakaenda. Ningewakamata pia, ila nisingewafunga kwa muda mrefu. Badala yake, ningewatandika tu, lakini si sana"

Chanzo: Jambo Tv
 
hawa watumishi wa kutafuta kiki badala ya kuwahubiria watu injili waache dhambi na kutubu ni dalili tosha kuwa zile siku zimekaribia..

"mtawatambua kwa matendo yao"
 
Katika kipindi hiki cha vuguvugu la kisiasa nchini Tanzania, sakata la kukamatwa na kupigwa kwa viongozi na wanachama wa Chadema waliokusanyika Mbeya Agosti 11, 2024, lilizua gumzo kubwa. Mchungaji Anthony Lusekelo, maarufu kama Mzee wa Upako, naye hakuachwa nyuma katika kutoa maoni yake kuhusu tukio hilo, nakuzungumza kwa ujasiri na kuonesha msimamo wake kwa wazi.

Mzee wa Upako, alieleza kuwa endapo angekuwa na mamlaka kama ya Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadhi Haji, ambaye alihusika katika hatua ya kuwakamata na kuwapiga viongozi na wanachama wa Chadema waliokusanyika siku hiyo, angefanya sawa na Kamishna huyo.

"Kama mimi ningekuwa na jukumu la oparesheni maalum, ningefanya kama alivyofanya Awadhi Haji. Serikali ilishatoa agizo kuwa wasiende Mbeya, lakini bado wakaenda. Ningewakamata pia, ila nisingewafunga kwa muda mrefu. Badala yake, ningewatandika tu, lakini si sana"

View attachment 3087690
Chanzo: Jambo Tv
Upako hauchanganywi na pombe, alipouchanganya na pombe upako ukamlipukia usoni, kunawakati alimuomba sana Magufuli amteue kwa kisingizio alikuwa TYL kabla ya uhuru, Magufuli aliishia kumuwekea lami njia ya kwenda kanisani kwake, upako hana tena.
 
Anatamani kurudi mjini mzee,anauma na kupuliza ila kiki zinagoma.
 
Nimecheka vibaya, juzi nilipoona interview yake nilijua anacheza mindgames ili serekali impe chochote. Alikuwa anajifanya anafunguka dhidi ya serekali, hivyo ili lengo lake litimie, ikabidi awataje cdm ili abalance shobo!

Huyo mzee ni bonge la boya, kipindi cha dhalimu magu alikuwa anampamba kinafiki ili amtoe. Sasa hivi ameona hawamtoi hivyo ameona aingie kwenye media ili kuwatisha wanaotaka kupendwa kwa shuruti.
 
Kabla ya kufanya interview na huyo Mzee fake, inapasa apimwe kwanza kilevi.
 
Katika kipindi hiki cha vuguvugu la kisiasa nchini Tanzania, sakata la kukamatwa na kupigwa kwa viongozi na wanachama wa Chadema waliokusanyika Mbeya Agosti 11, 2024, lilizua gumzo kubwa. Mchungaji Anthony Lusekelo, maarufu kama Mzee wa Upako, naye hakuachwa nyuma katika kutoa maoni yake kuhusu tukio hilo, nakuzungumza kwa ujasiri na kuonesha msimamo wake kwa wazi.

Mzee wa Upako, alieleza kuwa endapo angekuwa na mamlaka kama ya Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadhi Haji, ambaye alihusika katika hatua ya kuwakamata na kuwapiga viongozi na wanachama wa Chadema waliokusanyika siku hiyo, angefanya sawa na Kamishna huyo.

"Kama mimi ningekuwa na jukumu la oparesheni maalum, ningefanya kama alivyofanya Awadhi Haji. Serikali ilishatoa agizo kuwa wasiende Mbeya, lakini bado wakaenda. Ningewakamata pia, ila nisingewafunga kwa muda mrefu. Badala yake, ningewatandika tu, lakini si sana"

View attachment 3087690
Chanzo: Jambo Tv
Tungekupa kibali kuwapeleka wakaandamane Moshi!
 
Akisema jambo la maana tunamsifia lakini akizungumza usengerema tunamlaani
I told you the mchungaji is not okay mentally avoid intartaining and celebrating his opinions and comments, you will cry later on,

what is this then?🐒
 
Acha kupiga, suala la kufikiria tu kupiga watu ni mawazo ya kizamani na ni ushamba.
 
hilo jamaa ni li takataka flani hivi. Jizi la sadaka, tapeli

YESU NI BWANA&MWOKOZI
 
I told you the mchungaji is not okay mentally avoid intartaining and celebrating his opinions and comments, you will cry later on,

what is this then?🐒
Nlikutana naye siku moja kayatwika kwerikweri...mpaka kupanda bajaji ilikuwa mtihani
Hawa wachungaji manabii wetu
Kweli tumewapata

Ova
 
Back
Top Bottom