The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Waziri wa Madini ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amesema suala la kuanza ujenzi wa uwanja mkubwa wa mpira wa Dodoma ulizungumzwa kwa kipindi kirefu na michakato yake ilikuwa mingi ambayo haikufanikiwa hadi pale Rais Samia Suluhu Hassan alipoingilia ndipo likawezekana kufanyika.
Akizungumza wakati wa Hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi huo iliopo eneo la Changamani jijini Dodoma mwanzoni uwanja huo ulitakiwa ujengwe na watu kutoka Falme ya Morocco jambo ambalo halikufikia muafaka ambapo maamuzi yakafikiwa ujengwe kipitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR).
"Baada ya mchakato huo kuwa mrefu sana, Rais Samia Suluhu Hassan akatoa maelekezo kuwa Serikali chini ya uongozi wake watajenga wenyewe uwanja huo na hatimae leo Februari 13, 2025 mkataba wa ujenzi wa uwanja huo umetiwa saini" amesema Mavunde