ANTHONY MTAKA: Matukio ya Utekaji na uuaji hufanywa na makundi mbalimbali vikiwemo vyama vya siasa

MLIMAWANYOKA

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2019
Posts
631
Reaction score
2,247
Nakubaliana na Amiri Jeshi Mkuu, kuhusu umuhimu wa kutafakari matukio kama ya risasi kwa Donald Trump, aliyekuwa Rais wa Marekani. Ikiwa tukio kama hilo lingetokea Afrika, jinsi ambavyo ubalozi na mataifa ya magharibi wangejibu ni swali la kujiuliza.

Hivi karibuni, nguvu kubwa ya polisi ilitumika kudhibiti waandamanaji London, na ni muhimu kufikiri kama nguvu hiyo ingetumika kwenye nchi za Afrika. Kama alivyoeleza Rais, matukio ya mauaji yanatesa jamii nzima; ni bora tuwaachie vyombo vya ulinzi kufanya uchunguzi badala ya kuhukumu kabla ya ukweli kujulikana.

Dr. Slaa amethibitisha kupitia vitabu na mahojiano kwamba mauaji yanaweza kuhusishwa na makundi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, wakijaribu kuharibu taswira ya serikali. Katika siasa za kimataifa, watu wanakabiliwa na hatari kubwa kutokana na migogoro ya madaraka.

Natoa pole kwa familia zote zilizoathirika na matukio haya. Ni muhimu kuepuka kutumia matukio haya kama mtaji wa kisiasa. Hali ya kuaminiana inahitaji kujengwa katika jamii zetu, na ni vyema vyombo vya dola vikafanya kazi bila upendeleo.

Mungu abariki Taifa letu.
 
hasa chama cha siasa kinachoendelea na uchaguzi wake wa ndani hivi sasa 🐒
 
Viongozi wa Tanzania wote ni vichaa.utekaji wao wanauhalalisha Kwa kufananisha na uhalifu unaofanyika kwenye mataifa ya ulaya.Ni kichaa tu anayeweza kuwaza namna hiyo
 
Vyama vya siasa vina Majeshi yenye silaha za kivita?
 
Ulipaswa kuficha UPUMBAVU wako
 
Hayo makundi ya vyama vya siasa ni UVCCM.
Rejea utekaji uliofanyika mkoani Tanga, UVCCM na Polisi ndio waliofanya hayo matukio.
Clips za viongozi wa UVCCM ni ushahidi tosha.
 
Brain washing kwa kiswahili huitwaje , je waweza sema kusafishwa ubongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…