Anthony Mtaka: Una Miaka 59 unatukana Serikali saruji imepanda sana, wakati inauzwa Tsh. 4,000 ulikuwa wapi kujenga?

View attachment 3604336
Mkuu wa Mkoa wa Njombe RC Anthony Mtaka akiongea kuhusu Watumishi wa Umma kuhusu nidhamu na mshahara amesema kuwa watumishi wa Umma wanajisahau kuanza ujenzi mapema wanakuja kujenga wakati ambao wanakaribia kustaafu.

Wakianza ujenzi wanatukana bei za saruji kupanda hali ambayo wakati wanaanza kazi ilikuwa bei ya chini.

Yapi maoni yako?

ANAONGEA SANA MPAKA ANAONGEA PUMBA.
 
Kwani mwisho wa mtu kujenga ni Nyumba moja tu?
Vipi kama alisha jenga na anataka kujenga Nyumba nyingine sasa hivi?

Au mimi ndio sijauelewa huu uzi?
 
Ameongea ukweli, watumishi wengi wa umma wanajisahau wakiwa kazini. Mtu anapata pesa anaishia kuvaa visuti uchwara na kagari ka kutembelea ili aunekane. Akitoka hapo anajitutumua kupeleka watoto shule za gharama wakati msingi mzuri wa vipato hana. Akili zinawakaa sawa wakistaafu……
 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe RC Anthony Mtaka akiongea kuhusu Watumishi wa Umma kuhusu nidhamu na mshahara amesema kuwa watumishi wa Umma wanajisahau kuanza ujenzi mapema wanakuja kujenga wakati ambao wanakaribia kustaafu.

Wakianza ujenzi wanatukana bei za saruji kupanda hali ambayo wakati wanaanza kazi ilikuwa bei ya chini.

Yapi maoni yako?
Mtaka ana jionyesha kama mjinga. Kwani wakati cement shs 4000, mshahara ulikua shilingi ngapi? Kuna miaka baada ya uhuru mshara mkubwa kabisa uliitwa four figure yaani Shs 1000. Enzi hizo mfuko wa cement inawezekana ilikua shs 30. Kwa hivyo hakuna muda eti cement ndio bei ilikua rahisi. Thamani ya fedha yetu imekua inashuka huku malipo yakipandishwa kulingana na thamani halisi ya bidhaa ikiwa ni pamoja na malipo kwa nguvukazi.
 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe RC Anthony Mtaka akiongea kuhusu Watumishi wa Umma kuhusu nidhamu na mshahara amesema kuwa watumishi wa Umma wanajisahau kuanza ujenzi mapema wanakuja kujenga wakati ambao wanakaribia kustaafu.

Wakianza ujenzi wanatukana bei za saruji kupanda hali ambayo wakati wanaanza kazi ilikuwa bei ya chini.

Yapi maoni yako?
Mtu mwenye 59yrs kuna Sheria inayomkataza kujenga nyumba au kuna miili yoyote anayoivunja akijenga nyumba au ni kinyume na mila za Kitanzania kujenga katika umri huo?
Vipi kama hata alishakuwa na nyumba zaidi ya moja za kuishi ni makosa aliamua kujenga nyumba nyingine?
Huyo Antony Mataka/Matako/Matakataka ni mpuuzi asiyejitambua, asipangie watu maisha kwani mtu ana uhuru wa kujenga hata akiwa na 80yrs au zaidi.
NB: Anajua wakati cement ikiwa 4,000/- TSh mishara ya watumishi wa umma ilikuwaje.
 
Soda ilikua inauzwa Tsh150 lakini tulikua tunakunywa Mara 2 au 3 kwa mwaka christmas na Pasaka tu.

Ukimhadithia Gen Z hawezi kuamini... 4000 ya "1996" na 4000 ya "2026" Hazifanani kabisa.
 
Safari ya maisha ina changamoto nyingi sana hapo kati kati......tusiwe wepesi wa kuwahukumu watu na kuwatoa akili.......

Kama wewe umebahatika kupiga hatua kadhaa mbele mapema basi usimsimange uliyemuacha nyuma......

Hayo maneno ni ya mtu aliyeshiba na kuanza kumkejeli mwenye njaa!!

Watumishi wengi wa umma hali zao duni kiuchumi vipato vyao vinatosha kuendesha maisha ya kila siku na sio kukusanya kufanya hicho anachosema......

Kwanza wawaboreshee mishahara ili angalau kubakie chochote cha kuwafanya wafikirie kuwekeza!!!
 
Kwani mwisho wa mtu kujenga ni Nyumba moja tu?
Vipi kama alisha jenga na anataka kujenga Nyumba nyingine sasa hivi?

Au mimi ndio sijauelewa huu uzi?
KAMA UZI UNA WALENGA WATUMISHI WA UMMA
TUJIULIZE MTUMISHI WA UMMA WA KAWAIDA KABISA UNAPATA WAPI PESA ZA KUJENGA NYUMBA MOJA NA ZAIDI ?
WAKATI WANAOKULIPA WENYWE WANATARAJIA UKOSE UWEZO WA KUNUNUA TOFALI
 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe RC Anthony Mtaka akiongea kuhusu Watumishi wa Umma kuhusu nidhamu na mshahara amesema kuwa watumishi wa Umma wanajisahau kuanza ujenzi mapema wanakuja kujenga wakati ambao wanakaribia kustaafu.

Wakianza ujenzi wanatukana bei za saruji kupanda hali ambayo wakati wanaanza kazi ilikuwa bei ya chini.

Yapi maoni yako?
Maneno kama haya ndo chanzo Cha chuku dhidi ya watawala. Kunahaja ya viongozi kufunzwa jinsi ya kuongea na sio kuongea na uma wa lika mbalimbali kwa lugha za gen z au za watu wa baby boomers, millennials. Unatakiwa kubalance lugha yako kuendana na audience na ujumbe unataka kufikisha bila kuwa beza, kuwa tweza na kubagazanwengine.
Ni maoni yangu kwa viongozi hasa viongozi vijana
 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe RC Anthony Mtaka akiongea kuhusu Watumishi wa Umma kuhusu nidhamu na mshahara amesema kuwa watumishi wa Umma wanajisahau kuanza ujenzi mapema wanakuja kujenga wakati ambao wanakaribia kustaafu.

Wakianza ujenzi wanatukana bei za saruji kupanda hali ambayo wakati wanaanza kazi ilikuwa bei ya chini.

Yapi maoni yako?
Mtaka yupo sahihi 100% :NoGodNo:
 
Kama ameongea hivi Kwa ku zamiria basi , hafai kuwa mshauri wa Mzee
 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe RC Anthony Mtaka akiongea kuhusu Watumishi wa Umma kuhusu nidhamu na mshahara amesema kuwa watumishi wa Umma wanajisahau kuanza ujenzi mapema wanakuja kujenga wakati ambao wanakaribia kustaafu.

Wakianza ujenzi wanatukana bei za saruji kupanda hali ambayo wakati wanaanza kazi ilikuwa bei ya chini.

Yapi maoni yako?
Ni sawa na mimi mwaka 2060 cement mfuko mmoja ukiwa 100,000 uniulize kwanini sikujenga 2026 kipindi cement ni 17,000
 
Back
Top Bottom