Antivirus MixTape: Sugu awachana Clouds FM

Antivirus MixTape: Sugu awachana Clouds FM

Mkuu Pape mbona habari hii haileweki vizuri? ebu tujuze nini kimetokea?
 
Na hivi kajiunga na CHADEMA kajipalia makaa...hawakawii kumbambika kesi
 
So far sijasoma popote palipoprove kukamatwa kwa huyu mwanamapinduzi mpya..... Jamani kama kuna mwenye Jibu plz atuwekee hapa jamvini ili kama ni kukoment basi mtu uwe na uhakika na uandikacho........Ila lisemwalo lipo kama halipo....................
 
Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Mr. II au Sugu kama anavyojulikana na wengi, ameeleza sababu za kukamatwa kwake leo na jeshi la Polisi nchini.

j934ug.jpg


Akielezea sakata hilo, Mr II amesema kuwa alikatwa kuhusiana na mstari mmoja uliyomo kwenye wimbo wake ambao unapatikana kwenye albamu ya Anti Virus ambayo hivi sasa inasambazwa bure mtaani kwa mashabiki wa muziki huo. Katika wimbo huo, Mr. II amedaiwa kutishia kuua pale anaposema I wanna kill you, jambo ambalo amesema limemshangaza kwa sababu maneno yaliyotumika katika wimbo huo ni ya kisanii zaidi na yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Mr II, ambaye amedai kukamatwa na kuhojiwa na maofisa wa Polisi kutoka Makao makuu ya jeshi hilo kwa saa kadhaa na kisha kuachiwa kwa dhamana ya kujidhamini mwenywe, ametakiwa kuripoti tena kesho kutwa kituoni hapo.

Mr. II, pamoja na wasanii wengine wa Hip Hop nchini, wamerekodi nyimbo kadhaa za hip Hop na kuweka kwenye albamu moja ambayo wameiita Anti Virus, wakielezea hisia zao mbalimbali za kimaisha na kadhia la muziki wa Bongo. Awali, msanii mwingine wa Hip Hop, Dudubaya, naye alirekodi albamu yenye nyimbo kama hizo na kuiita NGURUWE.

Tukio la kukamtwa kwa Mr. II, limekuja siku tatu tu baada ya kutangaza kujiunga na chama cha siasa (CHADEMA) Ijumaa iliyopita na leo alitarajiwa kutangaza nia ya kugombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho mkoani Mbeya.
 
So far sijasoma popote palipoprove kukamatwa kwa huyu mwanamapinduzi mpya..... Jamani kama kuna mwenye Jibu plz atuwekee hapa jamvini ili kama ni kukoment basi mtu uwe na uhakika na uandikacho........Ila lisemwalo lipo kama halipo....................

Breking nyuzzzz: mr II akamatwa leo

image_thumb31.png


Habari iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde,inaripoti kuwa msanii mkongwe wa muziki wa hip hop nchini,Joseph Mbilinyi a.k.a mr II amekamatwa leo mapema asubuhi na watu wanaodaiwa kuwa ni wanausalama wakati anakwenda kwenye kikao cha press talk kinachofanyika kila siku ya jumatatu katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),sababu ya kukamatwa kwake bado haijajulikana na haijulikani wamekwenda nae wapi.

Globu ya Jamii inafuatilia kutaka kujua mustakabali mzima wa kukamatwa kwake na italeta taarifa kamili hapo baadae.hivyo tuvute subira.

Source: Michuzi blog
 
mhhhh-tuliyategemea,sasa hii kesi wakiishikilia cdhani kama ataruhusiwa kugombea huo ubunge
 
is this political zaidi ama?manake kama kila mwanamuziki akihojiwa,polisi watapata kazi za kutosha waache kutusumbua barabarani!
 
Hivi, leo nikikutana na kisura barabarani nikamwambia " I wanna steal you, au I wanna steal your heart away", nitakamatwa na polisi
kwa sababu wizi ni uvunjaji sheria? Let's be serious people.
 
Anything bad with this 'I wanna kill you"?

them kill us each day, we no complain
them kill us today, we feel no pain
we sing and play, them start complain
we go foray, them put us police station.
them fear a lot, what we say bout em.
 
Uhuru wa kuongea una majukumu yake, Watanzania bado hawajazoea kutumia Uhuru wao, wanaogopa sana dola...walio wengi wala hawajui kuwa katika yao na sheria nyingine za nchi zinawapa Uhuru mkubwa kiasi gani.

Hilo ndio tatizo...Sugu ni msanii, chochote anachoimba kwenye rekodi zake zinachukuliwa kama sanaa.
 
Keshatangaza kuwa yeye ni Chadema vitisho havina nafasi tena. Let them be careful kwani wanaweza kujikuta wanalipa compesation kubwa kwa ajili ya ignorance yao ya kushabikia siasa kwa kila kitu.
 
Kama polisi wanapolisi ushairi basi Amiri Akida Andanenga na wenzake waliokuwa wakijibizana katika malumbano wangefungwa siku nyingi.

Mimi nilifikiri wamemkamata kwa mambo ambayo yanaweza kusimama mahakamani katika mashtaka solid, kumbe mambo ya pure censorship.

Alichosema ni "I wanna kill right now" kitu ambacho kinaweza kutafsiriwa a thousand and one ways, I wanna kill this track, I wanna kill mediocrity, I wanna kill my opponents lyrically etc etc.

Hawa polisi akili mgando sana.
 
Kama polisi wanapolisi ushairi basi Amiri Akida Andanenga na wenzake waliokuwa wakijibizana katika malumbano wangefungwa siku nyingi.

Mimi nilifikiri wamemkamata kwa mambo ambayo yanaweza kusimama mahakamani katika mashtaka solid, kumbe mambo ya pure censorship.

Alichosema ni "I wanna kill right now" kitu ambacho kinaweza kutafsiriwa a thousand and one ways, I wanna kill this track, I wanna kill mediocrity, I wanna kill my opponents lyrically etc etc.

Hawa polisi akili mgando sana.

Polisi Vilaza sana yaani. Mbona Nyimbo kibao tu za Bongo Fleva maneno Kama Nitakuchinja yanatumika sana. Kwa hilo Polisi wamechemsha big tyme
 
MSANII wa Kizazi Kipya, Joseph Mbilinyi, al maarufu kama Mr II leo alikamatwa kama Breking Nyuuuzzzzz yetu ilivyoeleza awali, na kushikiliwa kwa zaidi ya masaa matano na Jeshi la Polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutishia kuua kwa kutumia muziki wake.

Mr II alikumbwa na mkasa huo majira ya saa tano asubuhi kwenye viunga vya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), wakati akijiandaa kuwasilisha mada ya Muziki wa bongo fleva ulipotoka na hatma yake kwenye jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye ukumbi wa Baraza hilo.

Globu ya Jamii ambayo imeshuhudia Mr II akiwa chini ya ulinzi Makao Makuu ya Jeshi 'Wizara ya Mambo ya Ndani' kwa mahojiano. Hata hivyo jeshi hilo halikuwa tayari kutoa taarifa zozote kwa madai kuwa upelelezi bado unaendelea na utakapokamilika utaweka wazi suala hilo.

Hata hivyo habari kutoka kwa watu wa karibu na Mr II zinasema kuwa mwanamuziki huyo aliitwa kwa mahojiano tangu Alhamisi iliyopita na watu walinzi hao wa usalama wa raia lakini hakuitikia wito.


Inadaiwa Mr II amesambaza CD yenye nyimbo 14 aliyoipa jina la "Anti Virus Mix Tape" ambayo amekikashifu kituo kimoja cha redio ikiwa ni pamoja watangazaji na wakurugenzi wa kituo hicho.

Katika CD hiyo Mr II ameshirikiana na wasanii zaidi ya 10 akiwemo kama G – Solo, Mapacha na Mkoloni.

Akizungumza na Blog ya Jamii mara baada ya kuachiwa kwa dhamana majira ya saa 11 jioni Mr II alisema: "Nashukuru nimeachiwa kwa dhamana.


"Nimejidhamini mwenyewe. Nchi hii ina uonevu sana. Eti wanasema wamenikamata kwa tuhuma za kutishia kuua kwa maneno kwa kutumia mziki wangu.

"Wameniambia niripoti tena Polisi siku ya Jumatano kwa mahojiano zaidi na kwamba upelelezi wao bado unaendelea."alisema Mr II.

MICHUZI

 
Niligundua siku nyingi polisi wetu hamnazo kabisa. Wanafanya kazi zao kwa hisia za kisiasa.

Nchi imejaa majambazi na vibaka kila kona na hakuna wanalofanya zaidi ya kushinda wanashughulikia mambo yasiyo na sababu.

Hawana lolote hawa.
 
Back
Top Bottom