Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,556
- 1,385
Ukitoa maoni yako kwa kipeperushi, kama alivyofanya Mtikila, unakamatwa.
Ukitoa hisia zako kwa mziki, kama alivyofanya Sugu, unakamatwa.
Ukionyesha ishara ya Chadema, kama walivyofanya wananchi huko Moshi, unapigwa na vijana wa CCM, na polisi wakitazama.
Utakimbilia mahakamani? Kwani hicho bado ni chombo huru?
Nabashiri kwamba kukaribia uchaguzi mkuu, ukionekana barabarani, kama wewe sio CCM, utapigwa au utakamatwa. Si Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa CCM wameshatangaza rasmi kwamba serikali ni yao, wanaweza kufanya lolote na hakuna mtu wa kuwauliza?
Nikiwa JKT Mafinga na Masange, tulikuwa tunaimba: "Kaburu wee, wacha matata, hiye hiye, wacha matata!" Sasa itabidi tuanzishe mchakamchaka mitaani tukiimba: "CCM wee, wacha matata, hiye hiye, wacha matata!".
Ila tuwe tayari kukamatwa, kunyanyaswa na hata kupigwa. There are no free lunches. Freedom costs!
Nampongeza Sugu na kumpa pole kwa ushujaa wake. Lazima hata hii Bongo iwe na akina Mandela na Sisulu wake, ndipo itoke hapo nchi. Bravo Sugu, bravo Mtikila, Aluta continua.