ANUNNAKI: Nadharia za Mungu, miungu, fumbo la sciencenscience na Teknolojia kubwa katika Dunia ya kale, kuanguka Kwa civilization na kuinuka Tena

ANUNNAKI: Nadharia za Mungu, miungu, fumbo la sciencenscience na Teknolojia kubwa katika Dunia ya kale, kuanguka Kwa civilization na kuinuka Tena

Embryology ya Allah huwa inachekesha Sana
Damu inaganda (dead blood) alafu ipo ndani ya mwanamke
Damu iliyoganda inabadilika kuwa pande la nyama ! , Pande la nyama linabadilika linakuwa mifupa tupu alafu mifupa inakuja tena kuvalishwa nyama dah!

Q 23:14. Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama.
"kuganda" ni neno alilotumia mtarjima aliyetarjim Kiswahili. Aliyetarjim Kingereza katumia manano mawili " clinging clot". Original yake unaifahamu?. Kama hauifahamu utapata shida sana kuifahamu Qur'an, nakushauri kajifunze Kiarabu.

Ndiyo raha ya Qur'an ukiweka tafsiri uweke na original yake. Ipo. si kama kile kitabu ambacho orijino yake haijulikani ilipo.
 
Original ya kiarabu ni damu iliyoganda , nimesoma kiarabu na translation zaidi ya 10 nyingi zinadanganya kuficha damu iliyoganda

Waislamu kwenye translation mnadanganya mno na mabano mengi mnaweka kupotosha
 
"kuganda" ni neno alilotumia mtarjima aliyetarjim Kiswahili. Aliyetarjim Kingereza katumia manano mawili " clinging clot". Original yake unaifahamu?. Kama hauifahamu utapata shida sana kuifahamu Qur'an, nakushauri kajifunze Kiarabu.

Ndiyo raha ya Qur'an ukiweka tafsiri uweke na original yake. Ipo. si kama kile kitabu ambacho orijino yake haijulikani ilipo.
Mutah girl tunapojadiliana kuwa mkweli ukianza kuleta uongo mtakatifu takiya utakuwa unajidanyanya mwenyewe maana Mimi naelewa kilicho andikwa

Q23:14ثُمَّ خَلَقْنَا ٱلنُّطْفَةَ عَلَقَةً فَخَلَق.....

Ipo wazi hapo sperm imekuwa damu iliyoganda (dead blood)

Alafu kwa nini Allah kasahau yai la mwanamke , anasema tu mbegu imekuwa damu mfu !?
 
"kuganda" ni neno alilotumia mtarjima aliyetarjim Kiswahili. Aliyetarjim Kingereza katumia manano mawili " clinging clot". Original yake unaifahamu?. Kama hauifahamu utapata shida sana kuifahamu Qur'an, nakushauri kajifunze Kiarabu.

Ndiyo raha ya Qur'an ukiweka tafsiri uweke na original yake. Ipo. si kama kile kitabu ambacho orijino yake haijulikani ilipo.
Tukiacha uongo wako wa damu iliyoganda

Biblia ndio kitabu ambacho vitabu vyake vina original matini na zipo unaweza kwenda kuziona na kuzishika kabisa

Koran mnayosoma imetoka kwa hafs miaka 200 baada ya Muhammad
 
WANEFILI NA JINSI WALIVYOTOKEA DUNIANI.

BWANA YESU asifiwe.
Karibu nikujize jambo hili.
Wanefili maana yake majitu au walioanguka.
Hawa walikuwa ni wanadamu walizaliwa kutokana na mahusiano ya kimapenzi kati ya wana wa MUNGU na binti wa binadamu.

Mwanzo 6:1-5 ''Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.BWANA akasema, ROHO yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa. BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.''

-wana wa Mungu hawa walikuwa ni malaika walioanguka (mapepo) ambao walioa wanawake binadamu waliopagagwa kwa nguvu za giza za mapepo hayo .
Uhusiano huu ulisababisha watoto Wanefili.

Mwanzo 6:4 '' Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.'' shetani kupita mapepo alikuwa anajaribu kuchafua damu ya binadamu ili kuzuia ujio wa MWOKOZI YESU KRISTO.
MUNGU aliahidi kwamba Masihi atakuja kutoka uzao wa Hawa ambaye ataponda kichwa cha joka hilo yaani Shetani.

Mwanzo 3:15 '' nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.''
Hivyo, mapepo au malaika walioasi walitumika ili kujaribu kuzuia hili na kuchafua ukoo wa binadamu, na kufanya ugumu kwa ajili ya Masihi asiye na dhambi kuingia duniani kupitia mwanamke.

Wanefili walikuwa walikuwa kizazi kikubwa cha mashujaa maarufu ambao walifanya vitendo vya uovu mkubwa ukubwa na nguvu zao zilitokana na mchanganyiko wa “chembe cha za damu” ya mapepo na zile za binadamu. Biblia inasema kuhusu wao ni kwamba walikuwa "mashujaa wa zamani, watu wenye sifa" (Mwanzo 6:4 ).

Wanefili walikuwa si wageni, walikuwa halisi, viumbe wa kimwili zinazozalishwa kutoka muungano wa malaika waasi na binti wa watu mapepo walirudia tendo la dhambi wakati mwingine baada ya mafuriko. Hata hivyo, ilifanyika kwa kiasi kidogo kuliko ilivyokuwa kabla ya mafuriko. Wakati wana wa Israeli walipeleleza nchi ya Kanaani wao walimpasa Musa taarifa:

Hesabu 13:33 "Kisha huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona''.
Na hata sasa ndio maana ni lazima sana kila mwanadmu kuokoka kwa kumpokea YESU KRISTO na kuomba maombi au kuombewa maombi ya kujitenga na kila nguvu za Giza.
Mchakato wa BWANA YESU kutuokoa una maana kubwa sana.
Maana mojawapo ya BWANA YESU kutuokoa, Biblia inasema kwamba MUNGU alituhamisha kutoka nguzu za giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake wa pekee YESU KRISTO.
Wakolosai 1:13 ''Naye(MUNGU) alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake(YESU ); ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;''

Kizazi cha manefili kilikuja baada ya adamu, kilikuja wakati Wa kabla ya gharika ya Nuhu . ni baada ya baadhi malaika kuacha enzi yao na kuja kufanya dhambi na wanadamu hivyo vilivyozaliwa hakikuwa wanadamu Wa kawaida bali ni wanadamu Wa ajabu wakiwemo wanefili.

Ufunuo 12:17 ''Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za MUNGU, na kuwa na ushuhuda wa YESU; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.''

-Tangu zamani shetani amekasirika dhidi ya mwanamke na amedhamiria kufanya vita juu ya uzao wa mwanamke, vita hiyo ni kuhakikisha uzao wa mwanamke haumpendezi MUNGU.
Wanefili ni zao la hasira ya shetani kwa uzao wa mwanamke.
Lakini ashukuriwe MUNGU kwa BWANA wetu YESU KRISTO kuja kutuokoa.
Kitendo cha Malaika kuasi mbinguni na kuja kufanya uasherati na wanadamu ili kupelekea kuzaliwa kwa watu walio na ushetani ndani yao Lilikuwa ni kosa kubwa kwa MUNGU.
malaika kuacha enzi yao na kuja kufanya dhambi, malaika hao waliadhibiwa na wako kifungoni wakisubiri jehanamu.

Yuda 1:6 " Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. "
Unefili ulikuwa ni mkakati wa kuhakikisha wanadamu hawaendi kuishi katika uzima wa milele lakini ashukuriwe BWANA YESU kwa kuja kutukomboa na kututoa katika kila nguvu za giza na tunawekwa huru kwa damu ya YESU KRISTO.
Warumi 6:22-13 ''Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa MUNGU, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA wetu.''

Damu ya YESU KRISTO ina uwezo wa kututenga na kila nguvu za giza.
BWANA YESU akikuweka huru hakika utakuwa huru.
Yohana 8:36 '' Basi Mwana(YESU) akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.''
Mapepo ni wanefili ambao hawatakiwi kuishi ndani ya mtu.
mapepo yako kifungoni sasa maana yake kuna vitu MUNGU ameyazuilia kufanya kwa wanadamu lakini mwanadamu akiwa mbali na KRISTO anaweza kuvamiwa na mapepo na mapepo hayo yatamfanya mwanadamu huyo kuwa shujaa katika kutenda dhambi.
Kuna watu leo ni mashujaa wa kipepo(kinefili) wa kunywa pombe nyingi.
Kuna watu leo ni mashujaa wa kipepo wa kubadili wanawake/wanaume kama nguo. huo ni unefili unaotakiwa kuondolewa kwa jina la YESU KRISTO ndipo mtu atakuwa huru tena bila kuongozwa na nguvu za giza.

2 Kor 5:17 '' Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.''
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.

Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.

4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.

5 Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
....wengi wamejifungia milango ya elimu kwa kutosoma vitabu vingine au kufanya utafiti wa kila kitu ambacho kimeandikwa kweny...
Tabia ya kutosoma vitabu vingine inaathiri maendeleo ya akili sana. Na kusoma hakujakatazwa, wote waislamu na wakristu wameaswa kuitafuta elimu sema wafia dini wanapotosha eti ni elimu ya dini tu[wakati ni elimu kwa ujumla]. Mi nakuambia ukiwa na Mungu, unaweza hata kusoma kitabu cha uchawi kabisa na ukaishia kumtukuza Mungu kupitia kitabu hichohicho. Ukasoma sayansi na ukamtukuza Mungu. I couldn't agree more.

Sema angalizo ni kwamba: kama wewe ni mtoto kiimani, baki na vitabu vya dini tu [kunywa maziwa] ila ukikua karibu tule makande na maugali, ila tahadhari usijione mkubwa uangukie kwenye madawa ya kulevya [elimu za uongo za kujidanganyadanganya maana nazo zipo]
 
Hahhahhaha.

Unaweza ukajiona umekuwa kiimani kumbe hujakutana na hoja zenye nguvu.

Mimi naona njia bora mtu asiridhike na itikadi yake bali ajaribu kuchungulia upande wa pili wa wenzie kisha achanganye akili yake na sio kuishia kusikiliza tu.

Kama katika uislamu mtu akiwa shia basi ni shia hataki kuskiliza watu wengine.
Mtu akiwa salafi ni salafi hataki kuskiliza upande mwingine.
Mtu akiwa ibadhi ni ibadhi hataki kuskiliza watu wengine.

Hii ni shida sana kwa sabbabu inaleta ushabiki wa kipuuzi tu ambao hauna maana.
 
....Mimi naona njia bora mtu asiridhike na itikadi yake bali ajaribu kuchungulia upande wa pili wa wenzie kisha achanganye akili yake na sio kuishia kusikiliza tu....
Umenena vema kabisa, samtaimu huwa nawazaga hata huu mgawanyiko tulionao ni mpango wa shetani. Na yeyote anayepinga sisi wote kuungana na kuelewana[kwa kudai kwamba ni mpango wa shetani] ndo anatekeleza huu mpango wa shetani.

Tukiacha kuogopana, tukajifunza ya wenzetu kila watu, tutapendana halafu tutaungana. Hatua ya kwanza ya kujifunza ni kukubali kuwa 'tuko na ujinga' tuna mapungufu.
 
Tena tuna mapungufu makubwa mno mkuu.
Tunatakiwa taratibu tuwaelimishe wenzetu na wataelewa tu.
 
Tukiacha uongo wako wa damu iliyoganda

Biblia ndio kitabu ambacho vitabu vyake vina original matini na zipo unaweza kwenda kuziona na kuzishika kabisa

Koran mnayosoma imetoka kwa hafs miaka 200 baada ya Muhammad
Na kabla ya hapo ilikuwa treated kama mali binafsi ya hafsa na sio official codex
 
Na kabla ya hapo ilikuwa treated kama mali binafsi ya hafsa na sio official codex
Qurani kama maneno yalishakuwa vifuani mwa watu tokea wakati wa mtume.

Hakuna ambae alijimilikisha Qurani ikawa ya kwake wakati ilishakuwamo vifuani mwa watu kibao.
 
Qurani kama maneno yalishakuwa vifuani mwa watu tokea wakati wa mtume.

Hakuna ambae alijimilikisha Qurani ikawa ya kwake wakati ilishakuwamo vifuani mwa watu kibao.
Waliohifadhi Quran kifuani kikamilifu walikufa kwenye vita ha Yamama, the rest walikuwa wame hifadhi vifungu vifungu na ndio maana ikatolewa agizo ifanyike collection sehemu tofauti tofauti hadi kwenye mbavu za wanyama
 
Na ile unayosema aliihodhi hafsa akaimiliki,wakati ameimiliki ilikuwa ni baada ya vita au kabla ya hivyo vita mkuu ?
 
Na ile unayosema aliihodhi hafsa akaimiliki,wakati ameimiliki ilikuwa ni baada ya vita au kabla ya hivyo vita mkuu ?
Hiyo ni baada ya kufanyiwa collection, collection ilifanyika baada ya vita
 
Back
Top Bottom