Anyongwe mtu aliyemdanganya Simon Sirro hadi akamfukuza Kazi Afande Meshack Samson Laizer pamoja na kushambuliwa na risasi na Askari wenzie

Anyongwe mtu aliyemdanganya Simon Sirro hadi akamfukuza Kazi Afande Meshack Samson Laizer pamoja na kushambuliwa na risasi na Askari wenzie

Uovu hauna kwao. Raia wamelalamika sana na wamedhulumiwa sana. Sasa uovu umehamia kwa polisi wenyewe.

Huyu ni polisi wa pili baada ya yule wa Mtwara aliyetoa habari za wale waliomuua mfanyabiashara na kisha yeye mwenyewe (kufariki mahabusu kwa kile kilichoelezwa kuwa amejinyonga na dekio).
 
Hapa Tanzania jeshi la polisi ni chafu sana. Kwanini Sirro mpaka leo uko pale hakuna mtu mwingine kwa hicho cheo?
 
Mimi sikuzote huwa nasema suala lolote la kipolisi huwa hela inatangulia mbele...
Polisi wetu ukiwa huna kosa na ukajidai mjuaji wa sheria basi jua ni rahisi sana kufungwa jela.. Polisi wakipewa chochote na mtu mashtaka yanatengenezwa na unakwenda na maji ukijiona..

Watu wengi wenye makosa huwa wanajidai sana kwakuwa wanajua kucheza vizuri na polisi... Hata uwe na ushahidi wa CCTV.. Mtu kama anawapa chochote.. Huwezi kufungwa... Ukitoa kesi za kisiasa zenye mikono ya wakubwa

Nilishatoa kisanga kimoja.. Jamaa kakamatwa bar usiku saa 8, akapelekwa kituoni akaambiwa una kiasi gani? Akajibu mi sina kosa na sitoi kitu...
Akazamishwa ndani.. Asubuhi akaomba msaada wa mawasiliano kutoka kwa askari ili ndugu zake wajue yupo wapi..
Baada ya masaa mawili ndugu hao.. Akatolewa mahabusu ooh mi sina kosa.. Mara wananionea tuu..
Akaletwa mpelelezi akawaambia ndugu.. Suala la huyu mtu ni kubwa sana.. Subiri kuna askari kutoka makao wanakuja.. Njooni kesho

Usiku akiwa mahabusu akaitwa akaambiwa chagua silaha mojawapo hapo.. (zina vumbi zimetoka store)
Akaambiwa hii silaha ni yako.. na wewe ni jambazi..
Ndugu kuja asubuhi wakapewa info.. Mtu wenu anamiliki gobore.. Na tunajiandaa kumpeleka kwa pilato.

Ndugu walijichanga vya kutosha.. Akatoka...

Funzo askari wetu wapo kimaslai zaidi.. Na hili haliishi leo au kesho..
Bila kutoa chochote.. Unajidai unafuata sheria.. Utakula Mvua za kutosha kimasihara hata kama huna kosa..

Tayari tabia hii imekuwa mfumo rasmi
Kwahyo unataka kusema mwalifu pia analindwa Kama tkk kesi yangu ya madale
 
Uovu hauna kwao. Raia wamelalamika sana na wamedhulumiwa sana. Sasa uovu umehamia kwa polisi wenyewe.

Huyu ni polisi wa pili baada ya yule wa Mtwara aliyetoa habari za wale waliomuua mfanyabiashara na kisha yeye mwenyewe (kufariki mahabusu kwa kile kilichoelezwa kuwa amejinyonga na dekio).
Hatar Sana yaan nipokee taarifa kuwa mwanangu kajinyonga na dekio hpn sipokei mwili
 
Anapigana a 'losing battle' ahame aliko ajifiche tayari kuyaanza maisha mapya otherwise atakufa huku anajiona. Police dunia nzima wako hivyo....tatizo LA kuwa na mdomo kazini
 
Anapigana a 'losing battle' ahame aliko ajifiche tayari kuyaanza maisha mapya otherwise atakufa huku anajiona. Police dunia nzima wako hivyo....tatizo LA kuwa na mdomo kazini
Uovu kwao umehalalishwa
 
Hii habari bado vyombo vya usalama vimeshindwa kuchukua hatua pamoja na uonevu wote huu?
 
Waziri Masauni hiki kilio cha siku nyingi ni mara ya pili nasoma uzi humu, hivi Sirro na mabeyo nani mkubwa kiumri haondoki yeye.
 
Duniani hakunaga haki Jamaa watakuja wammalizie kabisa maana anapambana ma mfumo mgumu kama ilivyo mfumo wa ccm kujiweka madarakan hayataki kutoka na ukitaka kuyatoa yanakukuta ya Lissu

Polisi dunian kote wako hivyo wakigundua wewe ni kikwazo kwao utawaweza kwa muda fulani ila bifu lao hata akihama mmoja wanarithishana na wanamtindo wa kukuacha muda mrefu uone bahari iko shwari unaishi kwa amani hata miaka 10 badae kitakacho kukuta Kama hawajakumaliza watahakikisha kuna kesi inakufunga muda mrefu.
 
Uovu hauna kwao. Raia wamelalamika sana na wamedhulumiwa sana. Sasa uovu umehamia kwa polisi wenyewe.

Huyu ni polisi wa pili baada ya yule wa Mtwara aliyetoa habari za wale waliomuua mfanyabiashara na kisha yeye mwenyewe (kufariki mahabusu kwa kile kilichoelezwa kuwa amejinyonga na dekio).
Hivi kamati ya uchunguzi wa mtwara ilifikia ilishatoa majibu ya kueleweka na wale majambazi wenye manyota wanapelekwa lini mahakamani?
 
Back
Top Bottom