Anyongwe mtu aliyemdanganya Simon Sirro hadi akamfukuza Kazi Afande Meshack Samson Laizer pamoja na kushambuliwa na risasi na Askari wenzie

Anyongwe mtu aliyemdanganya Simon Sirro hadi akamfukuza Kazi Afande Meshack Samson Laizer pamoja na kushambuliwa na risasi na Askari wenzie

Wakuu,

Nahisi Jeshi letu la Polisi limenajisiwa. Bora IGP Sirro ajiuzulu kama ameshindwa kuwatetea na kuwalinda Askari wake. Namshauri Sirro awatetea Askari wake Wanyonge kuliko kujipendekeza kwa Wanasiasa. Nilikuwa Nasikia Sirro ni Mlokole, lakini Ulokole wake nina mashaka nao sababu anautumia kama Kivuli kuficha maovu.

Meshack Samson Laizer, amefukuzwa kazi sababu ya kuwataja Viongozi wa Polisi wanaofanya kazi kinyume na kiapo chao. Kumbe kuna Askari Polisi hadi Vibaka wauaji na Wahujumu uchumi. Afande Samson Baada ya Kuwataja Majina akaanza kuwindwa.

Afande Samson Laizer akatekwa na kuteswa. Baada ya kupona akaanza kuwindwa ili auawe, Askari Polisi wa Sirro wakamfuata kwake wakamfyatulia risasi nyingi bahati nzuri akawahishwa Hospitali akapona.

Akiwa Hospitali akafukuzwa kazi kwa sababu ya Utoro wakati Polisi wenyewe ndo Waliompeleka Hospitali na kumpa PF3.

Hakuna anayemsikiliza. Si Sirro wala Mkuu wake wa Polisi.

MESHACK SAMSON LAIZER NI NANI?

Alikuwa Askari Polisi Arusha Mjini.

Mwaka 2019, Walitembelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Masauni kuzungumza na Askari Polisi na Askari Magereza. Akawataka Askari Watoe Kero zako. Samson akasimama akawataja Askari Pilisi Viongozi wanaofanya Vitendo kinyume cha maadili ya Kiapo chao. Alipoanza kutaja Majina akakatishwa kusema Masauni akataka amtumie majina.

Samson akaandika taarifa ikapokelewa na Kamishina Msaidizi Mwansasu. Likafunguliwa file kwaajili ya Uchunguzi. Wakapatikana Askari 22 kwamba walikuwa wanajihusisha na Vitendo hivyo na Wakahamishwa sehemu mbalimbali.

Baada ya Siku kama 22, nikaitwa na mbele ya Maofisa wa Polisi kumpongeza. RPC Ramadhan Hanje alimuita na kumpongeza kwa Mdomo na akampa kalamu nyeupe na kumwambia Utanikumbuka. Akamuuliza kwanini? Akamjibu wewe nenda tu utakuwa rafiki yangu.

Baada ya hapo alikamatwa na Viongozi wa Polisi Wakaguzi akawekwa Korokoroni siku tatu akateswa sana hadi Figo la kushoto likaharibika sana. Akatengenezewa kesi ya Utovu wa nidhamu, akaambiwa baada ya Saa 24 aende kufuatilia kesi yake.

Polisi Wakaendelea kumuwinda kwa Bunduki hospitali anapofanyiwa Matibabu akawa anajificha. Hadi alipopata namba ya Usalama wa taifa Dar Es Salaam, baadaye Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Masauni akampigia simu akamwambia ameshaongea na RPC Ramadhani. Alipoenda kwa RPC alibambikiziwa Kesi tatu za kutoa lugha chafu lengo likiwa kumnyanyasa sababu kasema Ukweli. Pia wakamvua Cheo chake Corporal.

Baada ya kuendelea kulalamika, tume ikaundwa ikaonekana hana kosa. Baadaye Waziri Lugola akamhamisha RPC kwa kosa la kumnyanyasa askari aliyejitolea kutetea Nchi yake.

Tume baada ya kuona nimeonewa na kunyanyaswa, nikapewa cheo cha Ushujaa cha Sergeant.
View attachment 2254022
Baada ya hapo nikaletewa Rushwa Mil 10, kwa sababu alikuwa Askari mwenzangu, nikatoa taarifa TAKUKURU, yule Askari Akafukuzwa. Nikapandishwa tena cheo changu hadi Staff Sergeant. IGP Sirro hakufurahishwa na mi akanipigia simu akasema Hafurahishwi na vile ninavyo fanya na hakufurahishwa na Askari aliyefukuzwa pia" anasema Afande Samson

Akaambiwa aende kusomea Cheo chake. Lakini walimnyima barua ya kwenda kusoma Chuo. Huwezi kwenda nje ya Mkoa bila barua ya Mkuu wako wa kazi lakini akanyimwa barua. Na baadaye ikaripotiwa kwamba amevuliwa vyeo alivyopewa sababu kakataa kwenda kusoma.
View attachment 2254012

Wakaanza kumuwinda ili Wamuue sababu alikataa rushwa ya Mil 10.

Akaenda kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu akaagiza apewe Ulinzi na kifuatilia swala langu.

"Sijawahi lipwa Mshahara unaoendana na cheo changu" anasema Sam.

Alivamiwa Usiku nyumbani kwake na Askari anaowamu wakampiga risasi na kumpiga akaokolewa na Majirani.

Damu zikiww zinamtoka Nyingi Polisi wengine wakaja wakamoeleka Hospital Mount Meru.

Baadaye Polisi wakamfuata Hospital wakamsomea shitaka la Utoro kazini. Baadaye akaja OCD wa Karatu akanisomea hukumu kwamba nimeoatikana na hatia. Baadaye akaja Ssp Almatus Mchunguzi kwamba nimefukuzwa kazi kwa fedheha kwamba nilitoroka jeshini. Wala hawakunipa barua.

Samson Meshack anaomba Waziri wa Mambo ya ndani amsaidie. Na mateso anayo yapata.

Kosa lake ni kufichua matendo mabaya ya jeshi la Polisi anasema Samson
View attachment 2253948
Daah
 
Back
Top Bottom