Tatizo la crypto currency ni volatility, yaani ni rahisi sana kupata faida ndan ya muda mfup na ni rahisi sana pia kupata hasara ndan ya muda mfupi.
Kiufupi kuwekeza kwenye crypto ni hatar kama ilivo betting.
Ngoja nikueleze kitu moja...
Crypto trading ni biashara tu kama biashara nyingine, na kawaida ya biashara huwa ina vipengele tofauti. Mfano; wewe unaweza fungua duka ukauza kwa jumla tu, mimi naweza fungua duka nikauza reja reja, lakini zote ni biashara za duka! Ndivyo ilivyo crypto, kuna aina nyingi za trading ambazo baadhi ni very risk na nyingine ni low risk, sasa maamuzi ni yako!
Wengi huoata hasara kwenye crypto sababu wana mitaji midogo, unakuta mtu ana 100K lakini anataka apate faida 10x ya uwekezaji wake tena kwa muda mfupi tu! Hapo sasa itakuwa ni betting na siyo crypto trading. Ila kuna wenye mitaji ya 10M+ ambao wana-target faida ya angalau 5% kwa wiki ambayo unaweza kuipata vizuri tu.
Mfano kuna aina ya trading inayoitwa futures, hii inafaida sana ila ni hatari mno na hasa zaidi kwa wenye mtaji mdogo! Hii aina ya trading inaweza kupa 100x return ndani ya dakika 10 tu! Lakini pia inaweza kukuacha na $0 ndani ya dakika 5 tu! Ila pia unaweza punguza hatari ya futures ukiwa na mtaji mzuri, kwasababu tunatumia kitu kinaitwa leverage, unavyoweka leverage kubwa ndio faida inakuwa kubwa zaidi na hiki ndicho kina wa-cost wenye mitaji midogo sababu wanatumia leverage kubwa wapate faida kubwa! Ila mwenye mtaji mdogo anatumia leverage ndogo maana hata akipata 2% ya mtaji wake bado anakuwa na faida nzuri tu!
Kuna aina nyingine ya trading inaitwa Day trading au Spot trading. Hii pia sio hatari sana, hapa huwa tuna-target sarafu zinazopanda na kushuka kila siku, unasoma charts za sarafu husika kisha unafanya technical analysis (unaweza tumia Trading View) na hapo utapata jibu either ununue sarafu hiyo au usinunue. Kwenye spot trading unaweza nunua sarafu saa 1 asubuhi na ukauza saa 7 mchana na ukapata faida yako nzuri tu, na hii haina risk sana uki-target sarafu nzuri.
Pia kuna arbitrage trading! Hii naipenda sana, nadhani kuliko zote (ingawa napenda futures pia). Kwenye arbitrage ni unanunua sarafu kutoka kwenye exchange moja na kuiuza kwenye exchange nyingine kwa faida kidoooogo tu! Yaani unaangalia labda $TRX Binance ni $0.1442 na $TRX hiyo hiyo KuCoin ni $0.1447 kwahiyo hapo pana difference ya $0.0005 ambayo faida yako inaweza range Kati ya $0.0002 - $0.0005 kulingana na kubadilika kwa soko pamoja na cost za ununuzi, uuzaji, na TX fee. Sasa hapo utapata faida bila risk yoyote, ingawa utahitaji mtaji mkubwa, na pia utatakiwa utulize kichwa haswa kupitia utofauti wa bei kwenye walau exchanges 3/5.
Na nyingine isiyo na risk kubwa ni P2P trading (peer to peer) hii trading inafanywa na waTZ wengi sana pale Binance, kuna watu wana pesa aise! Hapa ni unafanya biashara ya kubadilisha sarafu locally, yaani mimi nna $1000 USDT na wewe una 3M TZS, kwahivyo nakuomba wewe nikuuzie USDT zangu kwa bei ya juu kidogo ya soko ili upate faida, na kisha wewe unanitumia pesa ya TZ kwenye account zangu za pesa kulingana na kiasi cha USDT nilichokuuzia, hii ni sawa pia kwa upande kununua USDT.
Yoooote kwa yote, kuna aina zaidi ya tajwa hapo za ku-trade crypto, la kuzingatia zaidi ni kufanya uchambuzi wa masoko na sarafu unayotaka kununua ili usijikute kwenye hasara!
Unaweza ukaogopa kununua crypto ukihofia itashuka upate hasara, ila ukanunua mahindi gunia 100 kwa Tsh 35,000 kwa gunia na ukaweka stoo ili uuze kwa 50K kwa gunia, na mwisho wa siku soko likashuka ukaja kuuza kwa hasara ya 20K kwa gunia! Mafuta, mchele, sukari, na hata mazao mengine kama vitunguu, nyanya, tikiti... zooote hizo hupanda/hushuka/na huweza kuharibika ukapata hasara kubwa! Kiufupi ni kwamba hakuna biashara isiyo na hasara! Muhimu ni kufanya biashara yako kwa umakini mkubwa ili kupunguza hasara na kuongeza faida.