Anzeni michakato ya kuwatengenezea Gen Z fursa. Labda hasira yao itapungua

Anzeni michakato ya kuwatengenezea Gen Z fursa. Labda hasira yao itapungua

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Millenials tulipoingia kwenye uwanja wa ajira tulikuta fursa zipo zipo kidogo. Fursa za serikalini, biashara na hata zikajitokeza za boda boda na bajaji. Leo hii fursa hizo zimejaa na wala hakuna mpya zinazoonekana. Gen Z wanaingia uwanja wa ajira na hawaoni fursa zozote. Biashara kuna frame kila kona na zimejaa. Bajaji na boda boda zipo tele, siyo fursa tena. Serikalini ajira ndiyo zimekauka kabisa. Ajira za sekta binafsi ni adimu na ni chache zinazolipa hata kima cha chini. Gen Z hawaoni kabisa matumaini mbele yao.

Hili siyo Tanzania tu. Ni dunia nzima.

Kwa sasa kipaumbele kikubwa cha serikali kinatakiwa kiwe kutengeneza fursa kwa hawa Gen Z. kutangaza ajira 10K au 50K hakutoshi. Kunahitajika mamilioni ya ajira. Hasa ajira za ambao hawajafika huko vyuoni. Nyerere alikazia kwenye elimu ya kujitegemea kuwa sera zilenge walio wengi. Sehemu pekee za kutengeneza mamilioni ya ajira nchi hii ni kwenye manufacturing na kilimo cha kueleweka.

Tuache business as usual na janja janja. Wakati wa viongozi kustarehe huku wakitoa majibu mepesi umepita. Tukunje mashati mikono na kutengeneza fursa kwa Gen Z. Pengine hasira yao itaacha kuwaka.
 
Kwenye demands za Gen Z suala la fursa ni less than 10%

Wao wanataka Katiba Mpya, Utawala wa Sheria na haki ya kuishi wasitekwe na kuuliwa

Fursa za kiuchumi sio a hot factor kwenye hii sintofahamu
 
Kwenye demands za Gen Z suala la fursa ni less than 10%

Wao wanataka Katiba Mpya, Utawala wa Sheria na haki ya kuishi wasitekwe na kuuliwa

Fursa za kiuchumi sio a hot factor kwenye hii sintofahamu
Ukiangalia kijuu juu utaona hivyo. Hizo zilikuwa trigger tu za hasira iliyojaa kwa muda mrefu. Shida ya Gen Z kwa sasa ni ya kidunia. Ufisadi na ukosefu wa fursa za kiuchumi ndizo changamoto zao kubwa.

Pia ufahamu kuwa wengi wanaodai katiba mpya na uchaguzi huru, huwa wanafanya hivyo wakitegemea mambo hayo yatawaletea fursa nzuri za kiuchumi na maisha bora. Harakati zote za kisiasa kwenye kiini chake ni harakati za kiuchumi.

Suala la katiba mpya, kuuawa na ukosefu wa haki ni ya muhimu sana kutatuliwa. Lakini hata ukisolve hayo bila kuwapatia fursa za kiuchumi na kupambana na ufisadi bado tatizo la Gen Z litaendelea.
 
Back
Top Bottom