Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo atavunjika na kamwe hatapata dawa! Mithali 29:1-14

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
2,311
Reaction score
4,689
Huku kwetu Katonto mkoani Rukwa, kila aliyekuwa anapuuza chochote sasa ameanza kuzinduka usingizini! Mamia wamejitokeza kuhudhuria ibada ya Jumatano jioni, wakiwemo wanachama wa CCM ambao kwao Ufufuo na Uzima ndilo kanisa lao, wazee wasiojua chochote, akina mama ambao hawaelewi kabisa masuala ya siasa, na hata watoto waliozoea kwenda kuimba kwenye sandesukulu. Wote hawa wameshtushwa eti kwamba kanisa lao limepigwa utepe, hawaruhusiwi kusali tena!

Kosa limefanyika Dar es Salaam, wilaya ya Ubungo, lakini anayeadhibiwa ni muumini wa Ntalamila na Misunkumilo huko Mpanda Mjini. Mbaya zaidi, taarifa wanazopewa ni kwamba rais amelifunga kanisa lao, hawaruhusiwi tena kuabudu! Chuki na hasira yao wanaielekeza moja kwa moja kwa Rais wa nchi, na si kwa Msajili wala Jeshi la Polisi.

Kama kuna ushauri mbaya zaidi kuwahi kutolewa ni huu—kulifunga kanisa kwa kosa la Askofu. Makanisa mengine yote yakiwa kimya msidhani ni kwamba wamekubaliana na maamuzi haya. La hasha! Kwa sasa, waumini wa makanisa yote ya Kikristo nchini Tanzania—iwe ni Katoliki, Moravian, Lutheran, Anglican au mengineyo—habari kuu kwao ni hii: kanisa limefungwa! Hata kama hawatoi tamko lolote kwa uwazi au viongozi wao wamekaa kimya, haimaanishi wamekubali. Ni hofu tu! Hali ni mbaya huku mitaani tunakoishi.

Mbaya zaidi ni kwamba wananchi wameaminishwa kuwa aliyefunga ni Rais wa nchi. Hata kama hajahusika, wao hawajui lolote zaidi ya hilo, na chuki yao inamwelekea yeye moja kwa moja. Liponyeni taifa la Mungu kwa kuwa na mipaka katika maamuzi yenu. Mnataka kushinda uchaguzi huku nchi ikiwa imenyamazishwa? Tendeni haki, hiyo inatosha. Mungu huongea kupitia wanadamu, lakini pia shetani hufanya vivyo hivyo. Na kama kuna ushauri mbaya zaidi kuwahi kufanywa basi ni huu!
 
Huku kwetu katonto mkoani rukwa Kila aliyekuwa anapuuza chochote Sasa ameanza kuzinduka usingizini !! Mamia wameenda kuhudhulia Ibada ya jumatano jioni wakiwemo Wana ccm ambao ufufuo na uzima ndio kanisa lao ,wazee wasiojua chochote !akina mama ambao hawaelewi chochote kuhusu siasa na watoto waliozoea kwenda kuimba sandeschool eti kanisa lao limepigwa utepe hawaruhusiwi kusali !! Kosa limefanyika dar wilaya ya ubungo anaadhibiwa muumini wa ntalamila na misunkumilo huko mpanda mjini .mbaya zaidi taarifa wanazopewa ni kwamba rais amelifunga kanisa lenu hamruhusiwi kuabudu Tena !! Chuki na hasira Yao wanaielekeza Moja kwa moja kwa rais wa nchi na sio kwa msajili Wala jeshi la polisi !!kama Kuna ushauri mbaya zaidi kuwahi kutokea ni kulifunga kanisa kwa kosa la askofu ,makanisa mengine yote msione yamekaa kimya ni sawa kwamba waumini wa makanisa yote ya kikristo tz Kwa Sasa stori kubwa kwao ni hii ya kanisa kufungwa hakuna nyingine ,awe mkatoliki ,Moravian ,Lutheran ,Anglican ,na mengine yote !! Habari kuu Kwa Sasa ni kanisa kufungwa ! Hata kama hawatoi tamko lolote kwa uwazi ama viongozi wao wamekaa kimya haimaanishi wamekubaliana ni hofu tu lakini Hali ni mbaya huku mitaani tunakoishi !! Mbaya zaidi wao wameaminishwa kwamba aliyefanya hivyo ni rais wa nchi hata kama rais hajahusika wao hawajui chochote ,wanachojua ni rais na chuki ni kwa rais na so kwa msajili Wala jeshi la polisi,liponyeni taifa la mungu kwa kuwa na mipaka katika maamuzi yenu ,mnataka kushinda uchaguzi huku nchi ikiwa silence tendeni haki TU inatosha mungu anasema kupitia wanadamu lakini pia shetani husema kupitia wanadamu,,kama Kuna ushauri mbaya zaidi kuwahi kufanywa Basi ni huu
Zaburi.23:1 inatosha gentleman.

next time usiandike bandiko nonsense kama hilo ambalo linaashiria wazi kua wewe ni mjumbe wa shetani mzinifu 🐒
 
Huku kwetu Katonto mkoani Rukwa, kila aliyekuwa anapuuza chochote sasa ameanza kuzinduka usingizini! Mamia wamejitokeza kuhudhuria ibada ya Jumatano jioni, wakiwemo wanachama wa CCM ambao kwao Ufufuo na Uzima ndilo kanisa lao, wazee wasiojua chochote, akina mama ambao hawaelewi kabisa masuala ya siasa, na hata watoto waliozoea kwenda kuimba kwenye sandesukulu. Wote hawa wameshtushwa eti kwamba kanisa lao limepigwa utepe, hawaruhusiwi kusali tena!

Kosa limefanyika Dar es Salaam, wilaya ya Ubungo, lakini anayeadhibiwa ni muumini wa Ntalamila na Misunkumilo huko Mpanda Mjini. Mbaya zaidi, taarifa wanazopewa ni kwamba rais amelifunga kanisa lao, hawaruhusiwi tena kuabudu! Chuki na hasira yao wanaielekeza moja kwa moja kwa Rais wa nchi, na si kwa Msajili wala Jeshi la Polisi.

Kama kuna ushauri mbaya zaidi kuwahi kutolewa ni huu—kulifunga kanisa kwa kosa la Askofu. Makanisa mengine yote yakiwa kimya msidhani ni kwamba wamekubaliana na maamuzi haya. La hasha! Kwa sasa, waumini wa makanisa yote ya Kikristo nchini Tanzania—iwe ni Katoliki, Moravian, Lutheran, Anglican au mengineyo—habari kuu kwao ni hii: kanisa limefungwa! Hata kama hawatoi tamko lolote kwa uwazi au viongozi wao wamekaa kimya, haimaanishi wamekubali. Ni hofu tu! Hali ni mbaya huku mitaani tunakoishi.

Mbaya zaidi ni kwamba wananchi wameaminishwa kuwa aliyefunga ni Rais wa nchi. Hata kama hajahusika, wao hawajui lolote zaidi ya hilo, na chuki yao inamwelekea yeye moja kwa moja. Liponyeni taifa la Mungu kwa kuwa na mipaka katika maamuzi yenu. Mnataka kushinda uchaguzi huku nchi ikiwa imenyamazishwa? Tendeni haki, hiyo inatosha. Mungu huongea kupitia wanadamu, lakini pia shetani hufanya vivyo hivyo. Na kama kuna ushauri mbaya zaidi kuwahi kufanywa basi ni huu!
Yalipaswa kutokea ili Mungu ajidhihirishe!
 
Zaburi.23:1 inatosha gentleman.

next time usiandike bandiko nonsense kama hilo ambalo linaashiria wazi kua wewe ni mjumbe wa shetani mzinifu 🐒
Tlaatlaaa mzinifu eti sawa
 
Makenge na mashetani sisi hatuna cha kufanya.
 
Back
Top Bottom