Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo atavunjika na kamwe hatapata dawa! Mithali 29:1-14

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
2,311
Reaction score
4,689
Huku kwetu Katonto mkoani Rukwa, kila aliyekuwa anapuuza chochote sasa ameanza kuzinduka usingizini! Mamia wamejitokeza kuhudhuria ibada ya Jumatano jioni, wakiwemo wanachama wa CCM ambao kwao Ufufuo na Uzima ndilo kanisa lao, wazee wasiojua chochote, akina mama ambao hawaelewi kabisa masuala ya siasa, na hata watoto waliozoea kwenda kuimba kwenye sandesukulu. Wote hawa wameshtushwa eti kwamba kanisa lao limepigwa utepe, hawaruhusiwi kusali tena!

Kosa limefanyika Dar es Salaam, wilaya ya Ubungo, lakini anayeadhibiwa ni muumini wa Ntalamila na Misunkumilo huko Mpanda Mjini. Mbaya zaidi, taarifa wanazopewa ni kwamba rais amelifunga kanisa lao, hawaruhusiwi tena kuabudu! Chuki na hasira yao wanaielekeza moja kwa moja kwa Rais wa nchi, na si kwa Msajili wala Jeshi la Polisi.

Kama kuna ushauri mbaya zaidi kuwahi kutolewa ni huuβ€”kulifunga kanisa kwa kosa la Askofu. Makanisa mengine yote yakiwa kimya msidhani ni kwamba wamekubaliana na maamuzi haya. La hasha! Kwa sasa, waumini wa makanisa yote ya Kikristo nchini Tanzaniaβ€”iwe ni Katoliki, Moravian, Lutheran, Anglican au mengineyoβ€”habari kuu kwao ni hii: kanisa limefungwa! Hata kama hawatoi tamko lolote kwa uwazi au viongozi wao wamekaa kimya, haimaanishi wamekubali. Ni hofu tu! Hali ni mbaya huku mitaani tunakoishi.

Mbaya zaidi ni kwamba wananchi wameaminishwa kuwa aliyefunga ni Rais wa nchi. Hata kama hajahusika, wao hawajui lolote zaidi ya hilo, na chuki yao inamwelekea yeye moja kwa moja. Liponyeni taifa la Mungu kwa kuwa na mipaka katika maamuzi yenu. Mnataka kushinda uchaguzi huku nchi ikiwa imenyamazishwa? Tendeni haki, hiyo inatosha. Mungu huongea kupitia wanadamu, lakini pia shetani hufanya vivyo hivyo. Na kama kuna ushauri mbaya zaidi kuwahi kufanywa basi ni huu!
 
Zaburi.23:1 inatosha gentleman.

next time usiandike bandiko nonsense kama hilo ambalo linaashiria wazi kua wewe ni mjumbe wa shetani mzinifu πŸ’
 
Yalipaswa kutokea ili Mungu ajidhihirishe!
 
Zaburi.23:1 inatosha gentleman.

next time usiandike bandiko nonsense kama hilo ambalo linaashiria wazi kua wewe ni mjumbe wa shetani mzinifu πŸ’
Tlaatlaaa mzinifu eti sawa
 
Zaburi.23:1 inatosha gentleman.

next time usiandike bandiko nonsense kama hilo ambalo linaashiria wazi kua wewe ni mjumbe wa shetani mzinifu πŸ’
Utekaji ubakaji ufiraji mauaji pelekeni kwenu kwetu hatutaki ufirauni
 
Makenge na mashetani sisi hatuna cha kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…