Apartments kali zagundulika kuwepo kinyume cha sheria ndani ya gereza huko Indonesia

Apartments kali zagundulika kuwepo kinyume cha sheria ndani ya gereza huko Indonesia

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,864
Reaction score
5,254
Maafisa watano wa gereza Nchini Indonesia wamesimamishwa kazi baada ya uchunguzi kubaini uwepo wa vyumba vya kifahari vinavyofanana na ‘apartments’ ndani ya Gereza la Cibinong, lililopo Bogor karibu na Jakarta, ambavyo vinadaiwa kutumiwa na baadhi ya Wafungwa.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika katika gereza hilo, zaidi ya vyumba 10 vilibainika vikiwa vimetenganishwa na seli za kawaida za wafungwa na kuwa na huduma mbalimbali za kifahari, ikiwemo viyoyozi, televisheni kubwa, sofa pamoja na maeneo maalumu ya chakula.

Syafrida Rachmawati Rasahan kutoka Taasisi ya Ombudsman ya Indonesia amesema wakati wa ukaguzi huo, Wachunguzi walikutana na Wafungwa ndani ya eneo hilo na kubaini mazingira yanayofanana zaidi na nyumba za kulala wageni au apartments kuliko seli za kawaida za gerezani.

Uchunguzi huo pia umebaini kuwa gym pamoja na kifaa cha kuchezea gofu kwa njia ya kuiga (golf simulator) vilikuwa vinaendelea kujengwa katika eneo hilo.

Kwa upande wake, Inspekta Jenerali wa Wizara ya Uhamiaji na Marekebisho ya Tabia, Rudi Setiawan amesema makumi ya Wafungwa pamoja na Wafanyakazi wa gereza hilo wamehojiwa kufuatia sakata hilo.
#MillardAyoUPDATES
 

Attachments

  • HTuEBiwWoAABiQd.jpg
    HTuEBiwWoAABiQd.jpg
    251.5 KB · Views: 14
Back
Top Bottom