Apigwa shoti na kupoteza nguvu akiiba Transfoma ya TANESCO Manyoni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Vijana wameombwa kujitafutia kipato kwa njia ya halali ili kuepusha madhara yanayo tokana na wizi kama ambavyo alivyofanya Rajabu Jumanne Mkazi wa kijiji cha Njilii Halmashauri ya Itigi Wilaya ya Manyoni aliyepigwa na shoti ya umeme na kupoteza nguvu ya kutembea baada ya kuiba baadhi ya vifaa vya Transfoma ya TANESCO.

1748419089019.png
Hayo ameyasema leo Emanuel Soghweda, Diwani wa Kata ya Aghod Halmashauri ya Itigi wilaya ya Manyoni Mkoani Singida baada ya kufika Kijiji cha Njilii ambapo Rajabu Jumanne alikuwa anaiba miundombinu ya Tanesco majira ya saa nane usiku ndipo akapigwa na shoti ya umeme na kupoteza fahamu hivyo Diwani huyo amewaomba watumie nguvu zao katika kutafuta vilivyo vya halali.

"Nimepata taarifa hii kutoka kwa wananchi nimefika hapa namuona kijana huyu aliyekuwa anaiba miundombinu ya umeme na kupigwa shoti hivyo niwaase vijana watumie nguvu zao kutafuta vilivyo vya halali," Soghweda. Katika hatua nyingine diwani huyo amesema kuwa tukio limetokea saa nane usiku kwa mujibu wa mahojiano na mhalifu ambapo pia amethibitisha kuwa amezoea kuiba.

1748419438166.png
Mhandisi wa Tanesco Wilaya ya Manyoni Vicent Temba amesema kuwa watu wasiokuwa na nia njema wameiba miundombinu ya Tanesco ambapo wamefanya uharibifu ambao ni mkubwa, huku zaidi ya Transfoma tatu zimeharibiwa na wahalifu kwa kuiba baadhi ya miundombinu yake ikiwemo waya wa kopa.

Aidha kwa upande wake Sudi Rashid Mjomba wa Mjomba mhalifu huyo amewaomba vijana kujituma kawaida ili kuepuka madhara kama hayo yaliyotokea kwa mjomba wake. “Niwaombe vijana wasiibie watafute maisha kwa njia ya halali ili wasipatwe kama yaliyotokea kwa ndugu yangu huyu,” Sudi

Deus Migulu ni mwanakijiji wa Njilii amesema kuwa tukio hilo limemfundisha mengi moja wapo ni kuacha wizi. “Mie nimejifunza kutafuta vilivyo vya halali ili tusipate madhara kama haya,”
 
Vijana wameombwa kujitafutia kipato kwa njia ya halali ili kuepusha madhara yanayo tokana na wizi kama ambavyo alivyofanya Rajabu Jumanne Mkazi wa kijiji cha Njilii Halmashauri ya Itigi Wilaya ya Manyoni aliyepigwa na shoti ya umeme na kupoteza nguvu ya kutembea baada ya kuiba baadhi ya vifaa vya Transfoma ya TANESCO.

Hayo ameyasema leo Emanuel Soghweda, Diwani wa Kata ya Aghod Halmashauri ya Itigi wilaya ya Manyoni Mkoani Singida baada ya kufika Kijiji cha Njilii ambapo Rajabu Jumanne alikuwa anaiba miundombinu ya Tanesco majira ya saa nane usiku ndipo akapigwa na shoti ya umeme na kupoteza fahamu hivyo Diwani huyo amewaomba watumie nguvu zao katika kutafuta vilivyo vya halali.

“Nimepata taarifa hii kutoka kwa wananchi nimefika hapa namuona kijana huyu aliyekuwa anaiba miundombinu ya umeme na kupigwa shoti hivyo niwaase vijana watumie nguvu zao kutafuta vilivyo vya halali,”Soghweda

Katika hatua nyingine diwani huyo amesema kuwa tukio limetokea saa nane usiku kwa mujibu wa mahojiano na mhalifu ambapo pia amethibitisha kuwa amezoea kuiba.

Mhandisi wa Tanesco Wilaya ya Manyoni Vicent Temba amesema kuwa watu wasiokuwa na nia njema wameiba miundombinu ya Tanesco ambapo wamefanya uharibifu ambao ni mkubwa, huku zaidi ya Transfoma tatu zimeharibiwa na wahalifu kwa kuiba baadhi ya miundombinu yake ikiwemo waya wa kopa.

Aidha kwa upande wake Sudi Rashid Mjomba wa Mjomba mhalifu huyo amewaomba vijana kujituma kawaida ili kuepuka madhara kama hayo yaliyotokea kwa mjomba wake.

“ Niwaombe vijana wasiibie watafute maisha kwa njia ya halali ili wasipatwe kama yaliyotokea kwa ndugu yangu huyu,” Sudi

Deus Migulu ni mwanakijiji wa Njilii amesema kuwa tukio hilo limemfundisha mengi moja wapo ni kuacha wizi. “Mie nimejifunza kutafuta vilivyo vya halali ili tusipate madhara kama haya,”
Vijana wameombwa kujitafutia kipato kwa njia ya halali ili kuepusha madhara yanayo tokana na w...jpg
 
mbona anaonekana kama mwenye changamoto ya afya ya akili? yaani unataka kutuhadaa mchana kweupe hivi, wanaoiba hizo kitu ni mafundi tena wenye weledi wakutosha na isitoshe hilo dude halibebeki kirahisi bila crane cheni sanaa ni yaleyale ya unaua ama unateka mtu baadaye unadai kajiteka.
 
Safi sana kijana rijali kapata anachostahili.
Kumbe wizi ni tabia yake, ila kukanywaa aah.

Angekua na tabia ya ushoga, bas angesakamwa hatari, kulaa chuma hikooo.
😂😂😂😂😂😂
 
Kuna picha nyingine umeziona zenye dalili za ugonjwa wa akili au umetumia mbinu gani kuthibitisha hilo? Kwa sababu mjomba wake hajasema ni mgonjwa wa akili. Pia, mtuhumiwa mwenyewe kasema amezoea kuiba au mwandishi wa habari kaleta habari nusu?
 
Niwaombe vijana wasiibie watafute maisha kwa njia ya halali ili wasipatwe kama yaliyotokea kwa ndugu yangu huyu,” Sudi
Mbona viongozi wetu huko juu wanaiba sana na ndo hao wanafanya maisha ya wananchi huku chini yanakuwa magumu kupindukia?
Hiyo keki ya Taifa ingefika huku chini matatizo na umaskini wa wengi ungepungua
 
kabisa na kuna chawa wengi wana guts kabisa za kuwatetea , uaambiwa kuna mkuu wa chombo flani kaingiziwa bilioni moja kwwenye akaunti yake ya benki watu badala wahoji kwa kipato kipi kwa kazi ipi wanatishaiana oohhh utapotezwa yaani Bongo imerudi nyum miaka 1000 kuliko hata enzi za utumwa.
 
Safi sana kijana rijali kapata anachostahili.
Kumbe wizi ni tabia yake, ila kukanywaa aah.

Angekua na tabia ya ushoga, bas angesakamwa hatari, kulaa chuma hikooo.
😂😂😂😂😂😂
Mtetezi wa upinde 🌈 kwenye moja na mbili

Huyo shujaa akifa kafa kiume kuliko angetoa doughnut kizembe
51160200_glazed-doughnuts_1x1.jpg
 
Back
Top Bottom