Naam wakuu,
Kwa mara nyingine tumeona tuboreshe huduma ya JF ili izidi kuwa rahisi kutumia.
Kwa sasa unaweza ku-Install JF App kwa PC au Tablet (iPad zikiwemo) na Simu za Mkononi (Android na iPhones).
FAIDA:
1) Ni rahisi kutumia na haina tofauti yoyote na main site, hakutakuwa na malalamiko tena kuwa kuna kukosa notifications au kushindwa kufanya actions kadhaa
2) Ni rahisi kufunguka kuliko unavyodhania. Installation yake inachukua sekunde moja au pungufu. Haichukui space kwenye simu yako au kifaa chako
3) Ukiwa offline, bado kuna content utakuwa na access nayo kwa urahisi zaidi. Hulazimiki kuwa mtandaoni
4) na mengine mengi
Hatua za kufuata:
Kwa wanaotumia PC:
Tembelea JF kwa kutumia Google Chrome Browser, kisha utaona sehemu kama hii kwenye browser yako:
View attachment 1791283
View attachment 1791292
Kisha bonyeza Install kama inavyoonekana hapa chini:
View attachment 1791284
Utaona tayari unayo App kwenye PC yako. Kuanzia hapo hutokuwa ukilazimika kutembelea tovuti kwa njia ya browsing ya kawaida.
Mfano, mwenye Macbkook ataona icon ya App ya JF ikiwa hivi:
View attachment 1791290
Kwa wanaotumia Android Devices:
Tumia Google Chrome (au native browser ya simu yako):
Bonyeza mistari mitatu iliyo kushoto mwa LOGO ya JamiiForums, utaona kitu kama hiki chini:
View attachment 1791285
View attachment 1791286
Bonyeza
INSTALL kisha utaona hivi (itachukua sekunde 1 ku-Install)
View attachment 1791287
Kwa wanaotumia iPhone au iOS devices:
Tumia Safari Browser, bonyeza sehemu hizi zilizozungushiwa na fuata maelekezo kwenye simu... Just add to your device's home screen.
View attachment 1791288
View attachment 1791289
Ukikwama usisite kuuliza, tupo kwa ajili yako.
TAKE NOTE: Siku zijazo tutaondoa App zilizopo kwenye Google na Apple stores!
Karibuni