Apple imekuwa kampuni ya kwanza kufikia thamani ya soko ya dola trilioni tatu

Apple imekuwa kampuni ya kwanza kufikia thamani ya soko ya dola trilioni tatu

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Kampuni kubwa ya kiteknolojia ya Marekani Apple imekuwa kampuni ya kwanza kupata hesabu ya soko la hisa ya $3tn (£2.2tn).

Bei ya hisa za kampuni hiyo ilipanda kwa karibu asilimia The firm's share price has 5,800 tangu mwanzilishi mwenza na mtendaji mkuu wa zamani Steve Jobs kuzindua iPhone ya kwanza mnamo 2007.

Hata hivyo, thamani yake ilishuka kidogo kutoka kwa hatua hiyo muhimu, hadi kumaliza kikao cha biashara cha Jumatatu huko New York kwa $2.99tn.

Apple imekuwa mmoja wa washindi wakubwa wa janga hili, kwani athari za amri ya kutotoka nje iliyosababishwa na virusi vya corona ilifanya matumizi ya vifaa vya rununu kuongezeka.

Ilichukua zaidi ya miezi 16 kwa thamani ya hisa za Apple kupanda kutoka dola trilioni mbili hadi dola trilioni tatu, baada ya uhitaji wa bidhaa za kampuni hiyo kubwa ya teknoojia duniani kuongezeka wakati amri ya kutotoka nje ilipowekwa ili kudhibiti maambukizi ya corona.
 
Siipendi iphone, siipendi kwasababu inamaliza chaji, na gharama zake zipo juu, habari ya mjini ni oppo sasaivi
Mkuu uliwahi kutumia brand new au used?

Kwa upande wangu nilikuwa na mawazo hayohayo kumbe hii ilisababishwa na kutumia vitu used. Nilinunua Ipad air3 mpya hadi leo inaelekea mwaka wa pili sijakutana na hiyo shida.
 
Siipendi iphone, siipendi kwasababu inamaliza chaji, na gharama zake zipo juu, habari ya mjini ni oppo sasaivi
Nadhani sasa hivi wanakuja vizuri kwenye betri. Niliona mkbh anareview simu akasema iphone 13 pro max ndiyo simu inayokaa na chaj sana kuliko hata flagships nyingine ukiondoa moto G
 
Wanasumba kwenye midrange tu,kwa flagships bado sana.
Kuna simu ya vivo X70 pro plus, niliona kwa unboxing therapy. Ina camera ambayo hata kwenye giza pasipo kuwasha flash inatoa kitu. Inatumia tech jina nmelisahau. Alisema hajawahi kuona camera ya simu ambayo ina uwezo hup kwenye giza.
Oppo wametoa simu ya kupamba na z phone za samsung iko vizuri sana.
With time samsung ataanza pata tabu sana.
Iphone huyo ana soko lake kupoteza watumiaji siyo sana. Ni sawa na kufikiria wahindu watanyanganywa waumini na makanisa ya walokole, ila wakatoliki ndiyo wanapata tabu.
 
Back
Top Bottom