SOFTWARE Application ya Katuni kwa Watoto Kujifunzia

Je ni sawa watoto wadogo (chini ya miaka 5) kutumia simu janja na mtandao?

  • Ndiyo ni Sahihi

    Votes: 12 21.1%
  • Si sahihi

    Votes: 31 54.4%
  • Inategemea, mambo yote yana uzuri na ubaya wake

    Votes: 14 24.6%

  • Total voters
    57
Habari zenu wadau. Natumai Pasaka ilienda vizuri na waliopo kwenye mfungo wa Ramadhani wako vizuri pia.

Tunashukuru sana kwa kuendelea kupakua app hii ya Tuni kwa wingi kwenye Google Play store. Msisite kuacha maoni yenu ilituweze kuzidisha ubora wa huduma yetu.
 
image-2022-04-24-20:02:46-174.jpg

image-2022-04-24-20:03:02-191.jpg

image-2022-04-24-20:03:14-965.jpg

image-2022-04-24-20:04:26-151.jpg
 
Tupo kwenye mchakato wa kutengeneza katuni mpya hivyo kaeni chonjo vitu vizuri vinazidi kuja.
 
Tunatumai mapumziko ya mwisho wa wiki yameanza vizuri. Muda huu ni mzuri kuendelea kutumia app na mtoto ili aweze kujifunza kusoma na kuandika haraka.
 
Natumai mapumziko ya Idd yanaendelea vizuri. Tumepunguza ukubwa wa katuni zetu ili ziwe rahisi kupakua na zisitumie nafasi kubwa kwenye simu.
 
Si vizuri mtoto atumie simu hasa kuingia mtandaoni. Wazazi wanakosea sana wanavyowaachia watoto wakae na simu muda mrefu huku wakicheza magemu, wakiangalia katuni, wakipita mtandaoni nk. Wataalamu wamekusanya taarifa za awali zinazodai kuwa watoto wanaotumia simu muda mrefu wanakosa umakini shuleni na kuathiri nidhamu maisha yao yote.

Sio kwamba mtoto asitumie simu kabisa ila awe na ratiba. Tulivyokuwa wadogo hatukunyimwa kuangalia katuni lakini kulikuwa na ratiba maalumu, ikifika muda fulani ndio katuni zinaanza na mpaka uangalie lazima uwe umemaliza kazi mbalimbali. Ili kumjengea mtoto msingi mzuri wa matumizi ya simu ni lazima umpe ratiba kuwa wakati fulani baada ya kufanya hiki au kile ataweza kutumia simu. Matumizi ya simu hayafai kwa mtoto chini ya miaka mitatu na yasizidi masaa 2 kwa siku, huku nusu saa tu inatosha. Na sio umuachie tu mtoto aingie mtandaoni bila uangalizi wa karibu, lazima uhakikishe mtoto anakopita ni salama. Maudhi mengi ya mtandaoni hata wanayodai ni ya watoto hayafai kabisa.

Kwa kuliona hili, nawapendekezea app itakayomfundisha mtoto, kumburudisha na kumfikirisha. Mzazi/mlezi/ndugu akisoma na mtoto katuni kwa nusu saa kila siku za Kiswahili zinazosaidia kufundisha Kiingereza atakuwa ametoka na kitu. Baada ya muda utashangaa mtoto anaweza kusoma mwenyewe bila wewe kumsomea. Inafaa zaidi kwa watoto wa miaka mitatu na kuendelea ambao hawajaanza/wameanza chekechea/darasa la kwanza. App hii inaitwa Tuni na inapatikana Google Play Store hapa . Ni rahisi kutumia na maelekezo yanapatikana hapa .
 
mpe simu isiyokuwa na laini.
Utandawazi haukwepeki.
Kama sio kwenye simu ataona kwenye TV
 
mpe simu isiyokuwa na laini.
Utandawazi haukwepeki.
Kama sio kwenye simu ataona kwenye TV
Ni kweli utandawazi haukwepeki. Cha muhimu ni kuweka misingi mizuri ya matumizi ya simu. Pia ni muhimu tukumbuke kila kitu kina umri wake. Mtoto mdogo hatakiwi akutane na mambo ya watu wazima mpaka atakapofikia huo umri.
 
Siku hizi kumezuka mtindo wa kumwaachia mtoto mdogo simu kwa muda mrefu sana ili "kumkeep busy" asiwe msumbufu. Anacheza gemu na kuangalia katuni. Hii ni hatari sana.
 
Tumeanzisha mjadala kuhusu matumizi ya simu kwa mtoto unaopatikana H a p a. Karibu kwa majadiliano na kupiga kura.
 
Siku hizi kumezuka mtindo wa kumwaachia mtoto mdogo simu kwa muda mrefu sana ili "kumkeep busy" asiwe msumbufu. Anacheza gemu na kuangalia katuni. Hii ni hatari sana.
Kuna baadhi ya wazazi/walezi wanawaachia watoto simu karibia siku nzima ili watulie. Wengi hawapo hivi lakini kuna wachache wameanza hii tabia kwa kufikiri ni wajanja na wasasa kuliko wengine.

Mtoto akianza kuhangaika tu kidogo anasukumiziwa simu. Hawaongei na mtoto wala hawachezi na mtoto. Hapa ni kujitegea bomu na kusubiria likulipukie usoni.
 
Back
Top Bottom