April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

Hifadhi ya silaha ya mbagala inalipuka. Watu wanahamishwa kwa nguvu, ITV wanaandika kwa chini, kama kawa hakuna breaking news bongo.
 
--------------------------------------------------------------------------------

kwani hii ya leo inatofauti na ile ya jana?

maana jana i was so uncomfortable..unajua tena you never know hawa CHADEMA hawaaminiki

u can easily know the hopeless thoughts,watu wako kwenye mtikisiko mkubwa na inasemekana someone has lost life and someone else anadisrupt thread.
 
Poleni wakazi wa Mbagala. TzPride usipate presha sana kwa kuwa uko mbali na Familia. So far haitishi sana ila mwambie mama watoto afunge nyumba (maana vibaka hapa watafaidi sana) aende na watoto sehemu yoyote mbali na Mbagala kwa usalama zaidi.
 
Tahadhari imetolewa kutoka jeshini kuwa ghala kubwa la silaha hapo mbagala base huenda likalipuka, watu wanatakiwa kuwa mbali ya radius ya kilometer 25! Tafadhali wajulisheni wengine!

Pia ninataarifa kuwa hospitali ya temeke imejaa watu waliojeruhiwa na wengi wamezimia hasa watoto wa shule.

Barabara kwenda mbagala imefungwa pia!
 
Ni kweli kuwa kuna tatizo la kupata simu baada ya milipuko hii?

Fundi, ni watu wanajenga karibu na kambi za jeshi au silaha zinahifadhiwa kwenye makazi ya watu?

Ni hilo hilo. Kama kuna mahali penye ghala ya silaha, kwa nini watu wanaruhusiwa kujenga karibu napo? Nasikia Kimara Baruti ni hivyo hivyo!

Amandla.....
 
Poleni wakazi wa Mbagala. TzPride usipate presha sana kwa kuwa uko mbali na Familia. So far haitishi sana ila mwambie mama watoto afunge nyumba (maana vibaka hapa watafaidi sana) aende na watoto sehemu yoyote mbali na Mbagala kwa usalama zaidi.

Asante sana
 
Wamekata na simu hao.

Fundi Mchundo umesema unatumaini si uzembe? Kila kitu kinaonyesha kuwa haya ni matokeo ya uzembe, kama hii account ni ya kuaminiwa.Uzembe wao wa kusababisha mabomu yalipuke unawasababishia incovenience watu kuwakatia simu, watasema kwa sababu za usalama, yote hii ni katika kutapatapa waonekane wanafanya kazi.

Either that, or I fear...

Isije kuwa wamefanya makusudi kutoa statement kwamba "Jamani eeeh, na sie tupo, na midude inayotikisa mji mzima tunayo, sasa mkifanya ufisadi wakati sie tunakaa kwenye mikambi isiyo na hadhi ya kibinadamu wakati wowote tunaweza kufanya chochote"
 
hapa nilipo ppf tower jengo lilitingishika kidogo na kutoka hapa nilipo naona moshi mzito upande wa huko temeke/mbagala
 
Ni hivi. Hauhifadhi vitu vinavyoweza kulipuka kwenye kibuyu. Kama uwezo wa kuzijengea hifadhi ya uhakika hatuna basi kwa nini zisihifadhiwe mbali na makazi ya watu? Mabomu ya kuweza kusababisha uharibifu katika radius ya kilometa 25 si mchezo! Tunachezea mno maisha yetu.

Amandla......
 
kwani hii ya leo inatofauti na ile ya jana?

maana jana i was so uncomfortable..unajua tena you never know hawa CHADEMA hawaaminiki

We unatakiwa ukapimwe akili inawezekana sio kosa lako. Sasa CHADEMA hapa inahusikaje?
 
mbagala mpaka boko? shughuli ni pevu! poleni sana wakazi wa mbagala.
 
Temeke Hospitali pametapika watu, wakazi wengi wa mbagala wamekimbilia Maeneo ya tandika kuna wengine sidhani kama watarudi kuishi tena mbagala.

Jamani Mogadishu wanaishije?
 
HApa sasa tujiwekee picha kuwa tuko katika nchi ya vita. ni nafasi yetu ya kujua yale ambayo wenzetu wa mogadishu, Palestina, Irak r.t.c wanaishije kwa kihoro kama hiki, tena kwao kiukwelii na si kama hapa.
 
kwa wanaofahamu hiyo kambi iko jirani na makazi ya watu?
 
Jamani watu wanaokimbia mlipuko wanakimbilia kwenye Mto kizinga mpaka sasa kuna maiti 3 zilizopatikana ila bado haijafahamika watu wangapi wamekimbilia mtoni hasa watoto.
 
Hapa ofisini Samora kuna kijana karibu azimie kwa kishindo na hapo jengo la TTCL Extelecoms vioo vya pale ground floor vimepasuka kwa impact hiyo na watu wamekimbia ovyo. Yaani jengo lilikuwa linayumba kwa kishindo hicho. Halafu GT analeta upuuzi wake...how disgusting of GT!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…